Jumatatu, 7 Aprili 2014

Osteoporosis:Mifupa milaini, myepesi na kusagika


Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi. Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.
Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa. Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi aba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume. Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.
Nini cha kufanya
  1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umriu mepiga hatua
  2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza
  3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani)
  4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua)



   Virutubishi
Kwa ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubishi ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu.
Virutubishi vifuatavyo vimewasaidia wengi wenye tatizo hili.

WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA MAELEZO ZAIDI.




Aina ya ugonjwa na Suluhishi

SOMA KWA UMAKINI MKUBWA HAPA....

Ni vema tukafahamu ugonjwa unaosumbua mwanadamu, na vilevile tukatambua aina ya vyakula ambavyo tukila vitatusaidia kuondokana na tatizo.
Mwili wa mwanadamu ulivyoumbwa: Mwili wa mwanadamu umeumbwa ukiwa mkamilifua, usiokuwa na tatizo lolote. Siku mtu anapozaliwa, wengi wetu tunazaliwa tukiwa hatuna tatizo lolote.
Kawaida mwili wa mwanadamu umeumbwa  ukiwa mkamilifu kwa maana ya kwamba unatakiwa kujimudu wenyewe, pia kuwa na uwezo wa kujirejeshea afya ya mwili wake mwenyewe na kuweza kuishi maisha yasiyo na magonjwa.
Mwanadamu ameumbwa na anazaliwa na seli muhimu ndani ya mwili ambapo zina kazi kubwa ya kuhakikisha mwili upo sawa siku zote.
Seli hizi muhimu zinajulikana kwa jina la kitaalamu kama "adult stem cells"
Kadri tunavyokua hasa kuanzia miaka zaidi ya 25, uwezo wa mwili wa mwanadamu kuzalisha hizi seli hupungua. Hii husababishwa na stress (kimwili, kihisia, kimazingira) na lishe duni (vyakula na vinywaji vingi vimewekwa madawa kutoka mashambani hata viwandani). 

Utumiaji wa dawa za magonjwa kwa muda mrefu, utumiaji wa sigara na vinywaji vikali huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu na kuua hizi seli.
Umwagaji wa damu kwa njia ya ajali au aina yeyote ile husababisha upotevu wa seli mwilini.
Seli hizi hutambulika kama "masta seli”ndani ya mwili wa mwanadamu ambazo baadae hubadilika jina kutokana na sehemu ambapo zimesafiri na kuweka makao. Kwa mfano zikifika kwenye ini zinaitwa “Liver cells”, kwenye ubongo zinaitwa “Brain Cells, kwenye macho zinaitwa “Eye cells… n.k 
Bone Marrow:Seli hizi zinazalishwa na kiungo kijulikanacho kama bone marrow
Seli hizi kipingua kwenye kiungo cha ndani ya mwili husababisha kiungo hicho kutofanya kazi vizuri na kisha kiungo kupata tatizo. Mfano seli za kwenye kongosho zikifa au kupungua husababisha kongosho kutofanya kazi vizuri na hapo tatizo la sukari kwenye damu hutokea.
Kwa hiyo tukipata elimu ya vyakula itatusaidia kuwa makini na ulaji wetu ili tuishi mbali na magonjwa.

Jumamosi, 5 Aprili 2014

SHINIKIZO LA DAMU(HYPERTENSION)

Ni msukumo wa damu ulioko juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huitajika mwilini ili kusambaza chakula,oksijeni na kutoa uchafu.
Uanishaji wa shinikizo la damu

Uanishaji
Systolic BP
Diastolic BP
Kawaida (normal)
<120
<80
Prehypertension
120-139
80-89
Kali (mild hypertension)
140-159
90-99
Kali kiasi (moderate hypertension)
160-179
100-109
Kali sana (severe Hypertension)
≥180
≥110
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Aina ya kwanza: Asilimia 90-95 sababu huwa hazijulikani na kitaalamu huitwa primary or essential hypertension. Ingawa vitu vifuatavyo vimehusishwa kupelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu. Navyo ni:
  1. Uvutaji sigara
  2. Unene (visceral obesity)
  3. Unywaji wa pombe
  4. Upungufu wa madini ya potassium
  5. Upungufu wa vitamin D
  6. Kurithi
  7. Umri mkubwa
  8. Chumvi na madini ya sodium kwa ujumla
  9. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
  10. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Aina ya Pili: Asilimia 5 huwa na sababu dhahiri zinazopelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu na huitwa kitaalamu secondary hypertension. Na sababu hizi ni:
  1. Hali ya kukosa hewa usingizini (sleep Apnea)
  2. Kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu (Coarctation of Aorta)
  3. Saratani za figo (wilm’s tumor, renal cell carcinoma)
  4. Saratani ya tezi iliyo juu ya figo (pheochromocytoma)
  5. Ujauzito – wapo wakina mama wajawazito ambao hupata shinikizo la damu na huwa hatarini kupata kifafa cha mimba (eclampsia)
  6. Magonjwa ya figo (renal artery stenosis, glomerulonephritis)
Dalili
Mara nyingi huwa hamna dalili zozote, na kama zikiwepo mgonjwa huwa na dalili zifuatazo:
  1. Uchovu
  2. Maumivu ya kichwa
  3. Kuhisi mapigo ya moyo kwenda haraka
  4. Kichefuchefu
  5. Kutapika
  6. Damu kutoka puani
  7. Kutoweza kuona vizuri (blurred vision)
  8. Kusikia kelele masikioni
  9. Na mara chache kuchanganyikiwa 
Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu
  1. Kiharusi
  2. Moyo kushindwa kufanya kazi ( congestive heart failure)
  3. Madhara katika mshipa mkubwa wa damu ambapo ukuta wa ndani huchanika na damu hukusanyika katika ukuta wa mshipa huo(aortic dissection)
  4. Magonjwa ya mishipa ya damu
  5. Kushindwa kuona
  6. Athari katika ubongo 

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389

Sigara huharibu DNA mwilini na kuongeza hatari ya kupata kensa!




Kemikali za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu kupata kensa. Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli mwilini au kufanya mutation, kitendo ambacho huweza kusababisha kensa. Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho hufanyika kwa haraka sana kama vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa sindano. Habari hii ni tahadhari kwa watu wanaotaka kuanza kuvuta sigara, kwani takwimu zinatuonyesha kwamba, watu 3,000 hufariki dunia kila siku umwenguni kutokana na kensa ya mapafu, maradhi ambayo husababishwa kwa asilimia 90 na uvutaji sigara. Madhara ya kuvuta sigara kwa muda mrefu yanajulikana na wengi, ambayo ni pamoja na magonjwa ya moyo na kensa mbalimbali, lakini wataalamu wanatuasa ya kuwa, madhara ya sigara huanza pale tu mtu anapoanza kupiga pafu ya kwanza na kuingiza moshi wa sigara mwilini. Hivyo bado hujachelewa na unaweza kuacha sigara hii leo!

Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu.



Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.
Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Neno 'Afya' linamaanisha nini?



Kwa mujibu wa  ufafanuzi uliotolewa na kutangazwa na Shirika la Afya Duniani WHO katika mkutano wake wa tarehe 19-22 Juni 1946 na kusainiwa na wawakilishi wa nchi 61 duniani, 'afya ni hali ya mtu kuwa vizuri kimwili, kiakili na kijamii na sio tu kutokuwa na ugonjwa au udhaifu.' Ufafanuzi huo ulianza kutumika Aprili mwaka 1948 na hadi hii leo maana hiyo ya afya haijabadika. Ufafanuzi huo unamaanisha kwamba, tunaposema mtu ana afya sio tu tunakusudia kuwa mwili wake hauna maradhi, upungufu au udhaifu bali pia mtu huyo anatakiwa asiwe na matatizo ya kimwili, kiakili na hata kijamii. Kwa mujibu wa tafisri hiyo pana ya neno 'afya' tunaona kuwa watu wengi wanaamini kuwa afya imeganyika katika makundi mawili muhimu ambayo ni afya ya kimwili na afya ya kiakili. Afya ya mwili kwa binaadamu ina maana, kuwa na mwili wenye afya usiokuwa na maradhi, afya ambayo kwa kawaida hutokana na kuupa mwili mazoezi ya mara kwa mara, lishe bora na mapumziko ya kutosha. Katika nchi au maeneo ambayo watu wanapata lishe bora, huduma nzuri za afya na kuishi katika hali ya kimaisha inayoambatana na viwango vinavyotakiwa, kwa kawaida vimo na uzito wao huongezeka. Ukweli ni kuwa, ukiwauliza watu wengi afya ni nini, watasema kwamba inahusiana na  mwili kuwa salama bila ya kuathirika na ugonjwa. Lakini tukienda ndani zaidi, kitiba afya ya mwili inaamanisha ustawi wa mwili hali ambayo mtu anaipata kwa kutekeleza vipengee vyote vinavyohusiana na afya katika maisha yake. Uzima wa mwili unaakisi kufanya kazi vizuri moyo na mfumo wa kupumua, uwezo wa misuli, viungo pamoja na mwili kuweza kukubali mabadiliko tofauti na muundo wa mwili kwa ujumla. Masuala mengine ni pamoja na lishe bora, uzito wa mwili, kutokuwepo uraibu wa madawa ya kulevya, pombe, mahusiano salama ya kimwili, usafi kwa ujumla na pia kulala na kuamka kwa wakati unaotakiwa.

 Afya ya akili au uzima wa kiakili ni utambuzi wa mtu na uzima wake kisaikolojia. Mtu ambaye ana afya nzuri ya kiakili hana matatizo ya kiakili au kichaa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, 'afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahamili mfadhaiko (stress) unaotakana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha. Aweze kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.'

Ni rahisi watu kuelezea maana ya ugonjwa wa akili kuliko afya ya akili. Watu wengi wanakubali kwamba afya ya akili ni kutokuwepo ugonjwa wa akili lakini maana hiyo haitoshi. Hii ni kwa sababu kama tutachagua watu 100 ambao hawana kichaa au ugonjwa wa akili unaoweza kutambuliwa na daktari wa akili, lakini miongoni mwao tunaweza kuona kwamba afya ya baadhi yao kiakili imeimarika kuliko wengine.Tunaweza kusema kuwa, afya ya akili inajumuisha masuala kadhaa kama vile uwezo wa kuishi kwa furaha, uwezo wa kuvumilia shida na kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupatwa na matitizo, uwezo wa kuwa na uwiano katika maisha,  uwezo wa kubadilika kwa urahisi na kuzoea mazingira mapya, kujihisi salama na kujitambua.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389



Jumamosi, 11 Januari 2014

MATUMIZI YA CHUMVI NYINGI NI HATARI.

Miili yetu inahitaji chumvi kiasi kidogo sana. Kwa wastani tunahiaji kama gramu 1.25 (kama robo kijiko cha chai) kwa siku. Kwa bahati mbaya tunatumia chumvi kupita kiasi. Wataalamu wa Afya wanahusisha matumizi ya chumvi nyingi na uwezekano wa kupata msukumo mkubwa wa damu (High Blood Pressure), ambayo pia inaongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo, ikiwepo “stroke” na pia ya mifupa kama “osteoporosis”.

Hivi karibuni tafiti zimeonyesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo.
Sasa kazi kwetu!! Tujitahidi kupunguza uwezekazo wa kupata magonjwa sugu. Pungunguza matumizi ya chumvi na vyakula vyenye chumvi nyingi. Yafuatayo yatasaidia kufikia lengo hilo:
  • Punguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa kupika.
  • Usiweke chumvi mezani (wengine huongeza hata bila kuonja chakula)
  • Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa kutumia au kuongezwa chumvi
  • wapo unanunua vyakula vilivyosindikwa, kama vya makopo au paketi, soma lebo kwa makini. Chagua vilivyoandikwa “hakuna chumvi iliyoongezwa”(“no salt added”)
  • Tumia zaidi vyakula freshi unavyopika mwenyewe kwani unaweza kuthibiti kiasi cha chumvi unachotumia.
Kama tayari umezoea kutumia chumvi nyingi itakuchukua muda kidogo kujizoesha chakula chenye chumvi ndogo au kisicho na chumvi. Jizoeshe kidogo kidogo na utazoea, tena utafurahia vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi.

Kumbuka ni maisha yako na ufunguo wa kuingia katika mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako. Jipende!