Jumanne, 21 Oktoba 2014

NAMNA YA KUONDOA ASIDI INAYOSABABISHA KIUNGULIA KWENYE MAHARAGE-Epukana na kiungulia na tumbo kujaa gesi.


DSC07063
Maharage ni moja ya vyakula ambavyo mimi hukwepa kula nje ya nyumbani ,naweza kula maharage nje ya nyumbani kwangu endapo tu ninauakika na ambavyo mpishi  kaandaa maharage hayo,kwa maana nyingine nakula kama yameandaliwa na ndugu,jamaa na marafiki ambao ninauhakika na uandaaji wao. Hii yote ni kwasababu maharage yasipoandaliwa vizuri hunipa kiungulia kikali sana kwa muda mrefu na wakati mwingine tumbo hujaa gesi na kuninyima raha.
Maharage ni chanzo kizuri cha protini daraja B(protini itokanayo na mimea)na Nyuzinyuzi.Asidi aina ya  Phytic au phytates ipatikanayo kwenye maharage ikutanapo na madini mwili kama zinc,copper,calcium,magnesium namadini  chuma husababisha tatizo la kiungulia na tumbo kujaa gesi kwa baadhi ya watu,tatizo hili huwasumbua zaidi wale wasiokula Nyama na vyakula vitokanavyo na wanyama(vegeterians)kwani vyakula  vyao  hua na aside nyingi ya phytic.Tafiti zilizofanywa na American Dietetic Association zinaonyesha kwamba huwezi toa aside yote ya phytic kwenye maharage ila unaweza kuipunguza kwa kiasi kikubwa  kwa kuloweka maharage kwenye maji.
Wengi mnaloweka maharage kwenye maji ili kuyalainisha na kufanya yaive haraka wakati wakupika,Lakini msichojua ni kwamba kuloweka huko hupunguza  aside ya Hyptic kwenye maharage  ambayo ni chanzo cha kiungulia kwa wengi,aside hiyo pia hutonesha vidonda vya tumbo na kuleta maumivu makali kwa wale wenye tatizo la vidonda vya tumbo.
Ulowekaji wa maharage kwa muda mrefu
Watu wengi wamezoea kuloweka maharage usiku na kuyapika siku inayofatia,ikimaanisha yanalowekwa kati ya masaa manane hadi kumi na nane.Ingawa kuloweka huku kumezoeleka kwa wengi.Tafiti  zinaonyesha kwamba,njia hii ya ulowekaji wa maharage ni hatari sana kwa afya kwani hutoa nafasi, mazingira sahihi na  muda mrefu kwa  vijidudu viletavyo magonjwa vipatikanavyo  kwenye maharage kuzaliana na kukua .Ingawa maharage hupikwa kwa muda mrefu na kwa moto mkali bado haitoshi kuuwa vijidudu vya aina yote,bakteria watengenezao sumu au spore mara nyingi hubakia hai na huweza kua chanzo cha magonjwa kwa  mlaji wa maharage hayo.Ukiamua kutumia njia hii,basi loweka maharage na uyaweke ndani ya friji ili kupunguza uwezekano wa vijidudu hao kuzaliana kwenye maharage.
Ulowekaji wa maharage kwa muda mfupi-Njia iliyo bora
Kuloweka maharage kwa muda mfupi ni njia nzuri na bora zaidi ya kupunguza asidi ya phytic kwenye maharage,kwani huipunguza kwa kiwango kikubwa na kwa haraka zaidi kuliko njia ya kuloweka maharage kwa muda mrefu.Njia hii fupi kwa upande mwingine haitoi nasafasi ya vijidudu viletavyo magonjwa kuzaliana kwenye maharage,na huokoa muda kwani huchukua muda mfupi.Ulowekaji huu huchukua kati ya saa moja adi manne na si zaidi,ni uamuzi wa mpishi kuchagua aloweke masaa mangapi,ata hivyo ni vyema kujua kwamba ukiloweka kwa masaa manne utatoa kiasi kikubwa cha phytic kuliko ukiloweka  kwa saa moja.
Njia.
1.Pima kiasi cha maharage unachotaka kuandaa/kupika,mfano:vikombe vinne.(nashauri utumie kikombe kupima)kariri idadi ya vikombe ulivyopima
DSC07038
2.Chambua maharage  ili kuondoa maharage mabovu,mawe na uchafu mwingine wowote
DSC07039
3.Osha maharage,adi yawe safi.
DSC07043
4.Kwa kutumia kikombe ulichopimia maharage ,pima maji mara mbili ya kipimo cha maharage na uwekekando.mfano:kwakua tumepima maharage vikombe vinne,tutapima maji vikombe nane.(vikombe vya maji,mara mbili ya vikombe vya maharage)
DSC07046
5.Katika sufuria weka maharage na kisha ongeza maji uliyopima
DSC07049
6.Bandika maharage jikoni yachemke kwa dakika mbili tu.Esabu dakika mbili kuanzia pale yanapoanza kutokota na sio dakika mbili kuanzia ulipoyabandika jikoni.Epua jikoni baada ya dakika hizo kuisha.
DSC07052
7.Acha  kwa kati ya saa moja adi manne(kutokana na muda ulionao)
Muonekano wa maharage baada ya masaa manne
Muonekano wa maharage baada ya masaa manne
8.Chuja maji yote kwenye maharage.
004
Maji yaliyochujwa kwenye maharage.maji haya yamebeba phytic iliyotoka kwenye maharage.
Maji yaliyochujwa kwenye maharage.maji haya yamebeba phytic iliyotoka kwenye maharage.
9.weka maharage kwenye sufuria, ongeza maji ,bandika jikoni  kisha chemsha adi maharage yaive.
Maharage yaliyoiva,baada ya kuchemshwa
Maharage yaliyoiva,baada ya kuchemshwa
Baada ya kuivisha maharage ,unaweza kuyapika au kuyaunga  katika namna upendayo.
Maelezo ya ziada.
Ingawa  njia hii hupunguza  phytic  kwa kiasi kikubwa sana na hutosha kufanya mtu asipate kiungulia au tumbo kujaa gesi,kuna wale wenzangu ambao hata iyo hyptic kidogo sana iliyobaki kwenye maharage inatosha kuwapa kiungulia.Ipo namna ya kukata nguvu ya hiyo phytic kidogo iliyobaki na kufanya maharage yawe mazuri zaidi.Nitakueleza hilo katika makala ijayo.

WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA USHAURI NA TIBA JUU TATIZO LINALOKUSUMBUA KIAFYA. PIA UWONAPO MAFUNDISHO YETU WAAMBIE WENZAKO PIA WAJIFUNZE KAMA WEWE. ASANTE

IJUE THAMANI YA GILIGILIANI: KIUNGO, DAWA, UREMBO.



Giligiliani (majani)
Giligiliani (majani)
Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.
Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium na Magnesium
Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi
Giligiliani (Mbegu)
Giligiliani (Mbegu)
Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi maana yake ni kwamba chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
  1.  Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza tumbo na huondoa gesi kwenye  utumbo mwembamba  ambayo mara nyingi husababishwa na vyakula tunavyokula hivyo hupunguza utoaji  gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana
  2.  Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa tumbo na kuhara.
  3. Inazuia Ugonjwa wa UTI.Yaani Urinary tract infection
  4. Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo
  5. Inaondoa gesi tumboni
  6. Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)
  7. Inapunguza  cholesterol mbaya mwilin
  8.  Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)
  9.  Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
  10. Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe (anti inflammatory)
  11. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi
Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa
  •  Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili.Chujakisha ongeza sukari kidogo.Kunywa ikiwa yamoto au vuguvugu
  •  Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha chai cha mbegu za giligiliani zilizosagwa  na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa ikiwa vuguvugu
  • Kushusha sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya giligiliani (mbegu) mara kwa mara,pia tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye chakula.
  • Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina majani ya giligiliani,chuja au kamua ili kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha ikauke kisha osha au nawa na majivuguvugu.Onyo:usisugue ngozi
  •  Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya vijiko 2 vya chai vya maji ya giligiliani na kikombe kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim
  •  Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza asidi tumboni 
Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.
Ni vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo tulivyonavyo majumbani ni tiba ya magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia hutokana na mimea,virutubisho huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa na Kemikali ili kutoa vidonge na madawa ya magonjwA mbalimbali.


WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA USHAURI NA TIBA JUU TATIZO LINALOKUSUMBUA KIAFYA. PIA UWONAPO MAFUNDISHO YETU WAAMBIE WENZAKO PIA WAJIFUNZE KAMA WEWE. ASANTE

FAHAMU UMUHIMU WA RATIBA YA KULA KATIKA FAMILIA -hata kula kwahitaji ratiba


Meza imeandaliwa tayari kwa familia kupata  kifungua kinywa.picha hii ilipigwa siku ya jumapili asubuhi
Meza imeandaliwa tayari kwa familia kupata kifungua kinywa.picha hii ilipigwa siku ya jumapili asubuhi
Ratiba ni kitu muhim sana katika maisha ya familia na hata kwa mtu binafsi.Tunajua familia kawaida huwa na watu wawili au zaidi,na pale mnapoishi wawili au zaidi kama familia ni muhim kuwa na ratiba za familia ili maisha na shughuli za familia ziwe katika utaratibu Fulani unaoeleweka.Kila familia huwa na ratiba zake
Ratiba ya muda wa kula ni ratiba muhim sana katika familia,lazima kuwe na utaratibu wa chakula,ijulikane chai ya asubui ,chakula cha mchana,chai ya jioni na chakula cha usiku vinaliwa saa ngapi au wakati gani.lazima kuwe na muda maalum kwa kila chakula,na muda huo unapofika basi chakula kitengwe mezani na watu wote wale kwa pamoja.
Familia katika mlo wa jioni(usiku)aliepiga picha hii aliniambia ilikua majira ya saa mbili na robo usiku
Familia katika mlo wa jioni(usiku)aliepiga picha hii aliniambia ilikua majira ya saa mbili na robo usiku
Kutokua na ratiba ya muda wa kula kunaleta shida ya upangaji wa matumizi ya chakula, kunaongeza gharama ya chakula na pia baadhi ya wana family huweza kukosa chakula.kila mtu anapokuja kula kwa muda anaotaka yeye,inamaana kila mtu atapakua kutoka kwenye sufuria,haijulikani nani amekula nani bado ,matokeo yake kuna watu wanaweza kosa chakula wakati huo huo garama ya chakula inaongezeka kwani ili kuweza kugawanya chakula ili mlaji aje ale kwa muda wake ni lazima upike chakula kingi,si rahisi kumpakulia mtu mboga ya majani kijiko kimoja ukamtunzia ,utataka utunza angalao robo bakuli.
Ratiba ya muda wa kula pia huipa familia muda wa kukaa pamoja na kufuraia chakula,kutaniana na hata kuongea mambo ya kifamilia kwani wana familia wote wanakua mezani.La msingi zaidi inawapa wazazi nafasi nzuri ya kuwafundisha watoto wao adabu za mezani na namna ya kula.zaidi inatoa mda na nafasi kwa mpishi kufanya shuguli zake zingine kwani anakua anajua ni saa ngapi atakua amemaliza kazi za jikoni
Ingawa Baadhi ya familia ni ngumu watu kula pamoja kutokana na ratiba zao za kazi,shule namengineyo.bado hii si sababu ya  kufanya kusiwe na ratiba ya muda wa kula, kwani kuna wale wanaobaki nyumbani nao lazima wafate ratiba,pia siku za weekend kwakua watu wapo nyumbani basi ratiba iwepo na ifatwe.Lakini pia  kila siku watu wapo nyumbani kwa ajili ya chakula cha usiku basi angalao chakula cha usiku familia ile kwa pamoja.
Nimeona familia nyingi sana zisizokua na ratiba ya chakula, na naweza kukwambia mambo machache juu ya familia hizi ambayo ni ya uakika: 1.chakula mara nyingi hakiwatoshi. 2.kuna tabia mbaya ya watoto kugombania chakula .3.chakula cha baba na mama kinatengwa pembeni mapema .4.Baba na Mama hula chakula kizuri kuliko watoto 5.chakula hakitengwi mezani. 6.watoto hawana adabu mezani na hawajui kula vizuri(kistaarabu).7.vyombo vichafu haviishi jikoni. 6.Dada wa kazi ndio mpishi mkuu wa familia.mambo ya aibu haya.
Nakupa mfano wa ratiba ya muda wa kula ya nyumbani kwetu,nikimaanisha kwa wazazi wangu.Nilizaliwa nikaikuta na imenikuza,hata leo ingawa siishi tena na wazazi bado ni ratiba  ninayoifuata.Zaidi ni kwamba kila mwanafamilia bado anafata ratiba hii,hata wale walio owa na kuolewa wanaitumia kwenye familia zao.
Ni ratiba rahisi tu,Kifungua kinywa saa mbili asubuhi,mid-morning bite inaweza kua juice au matunda au snack yoyote saa tano ,lunch saa saba kamili mchana,chai ya jioni saa kumi na moja kamili jioni,chakula cha usiku saa mbili kamili usiku.wakati mwingine kuna kuwahi au kuchelewa lakini  mara nyingi haitazidi nusu saa.
Kama familia yako haina ratiba ya muda wa kula basi wakati umefika wa wewe kuanzisha ratiba.Maisha lazima yawe na mpangilio,yawe na ratiba,Tukiwa watoto Mama yetu alipenda kutuambia kwamba mtu asiekua na mpangilio na ratiba katika maisha hawezi kufanikiwa kimaisha.
Anzisha ratiba ya chakula au kula Nyumbani kwako ili uboreshe maisha ya familia yako.

WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA USHAURI NA TIBA JUU TATIZO LINALOKUSUMBUA KIAFYA. PIA UWONAPO MAFUNDISHO YETU WAAMBIE WENZAKO PIA WAJIFUNZE KAMA WEWE. ASANTE.....!

SAYANSI YA CHAKULA,CHAKULA NI NINI?

Leo ninaongeza kipengele/category mpay hapa jikonoi,kipengele hiki ninakiita SAYANSI YA CHAKULA. Katika kipengele hiki  tutajifunza juu ya sayansi ya chakula  ili upate uelewa zaidi juu ya chakula na virutubisho kwa ujumla.
foods
Kuna ufaam mdogo sana juu ya chakula na sayansi ya chakula katika jamii,hii hufanya watu washindwe kula chakula bora kwani wengi hawajui wale nini na kwanini .Ongezeko la magonjwa yasababishwayo na chakula nalo limekua kubwa sana katika jamii yetu,idadi ya watu wenye uzito mkubwa (wanene) nayo inazidi kuongezeka haya yote huchangiwa na ufaham mdogoo juu ya sayansi ya chakula.
Katika makala hizi,nitajitahidi kutumia lugha rahisi ili kila moja aelewe.Ingawa nitaandika makala hizi katika lugha ya Kiswahili, lugha ya kiingereza pia nitatumia pale nitakapo lazimika kwani kuna baadhi ya maneno au vitu amabavyo  havina tafsiri katika lugha ya Kiswahili au laa nimeshindwa kupata tafsiri yake.
Masomo/makala hizi zitafundisha yale yanayompasa kila mtu kujua Juu ya vyakula na virutubisho.hayatakua na uchambuzi wa ndani sana.kwani lengo nikutoa utambuzi wa awali juu ya sayansi ya chakula.
Tutaanza kwa kujifunza juu ya chakula na virutubisho.
Chakula ni nini?
Chakula nikitu chochote kinacholiwa ambacho huupa mwili virutubisho na urutubisha mwili.kuna vyanzo vikuu viwili vya chakula navyo ni MIMEA NA WANYAMA.
A) Mimea - vyakula vitokanavyo na mimea vimegawanyika katika makundi  manne
  1. .Mizizi - karoti,viazi,Mihogo
  2. .majani na matawi – kisamvu,mchicha,sukumawiki
  3. .Matunda - Machungwa,maboga,maembe,ndizi
  4. .Mbegu - mchele,mahindi,maharage
vyakula vitokanavyo na mimea
vyakula vitokanavyo na mimea
B) Wanyama – vyakula vitokanavyo na wanyam ni
  1. .Nyama
  2. .mayai
  3. .Maziwa
vyakula vitokanavyo na wanyama
vyakula vitokanavyo na wanyama
Ladha
Vyakula vimegawanyika katika makundi manne ya ladha,binadam anapokula chakula chochote anapata moja kati ya ladha hizi
  1. Tamu - ladha hii husababishwa na uwepo wa  sukari  katika chakula
  2. Chungu - ladha mbaya na haipedwi
  3. Chachu - ladha inayosababishwa na uwepo wa asidi kwenye chaku
  4. Chumvi - husababishwa na uwepo ya alkalini kwenye chakula
Virutubisho vya chakula ni nini?
Virutubisho vya chakula ni vitu(substance) ambavyo hurutubisha (nourish) mwili,Virutubisho hujenga na kurekebisha seli za mwili.Virutubisho hivi  hupatikana kwenye vyakula vyote.
Virutubisho vya chakula
Virutubisho vya chakula
Virutubisho  vya chakula vimegawanyika katika makundi sita
  1. Wanga ,kazi yake kubwa nikuleta nguvu mwilini. mfano:mahindi,viazi,ngano ,mchele
  2. Protini - kazi yake kubwa ni kujenga mwili . mfano:Nyama,mayai ,maharage,njegere,maziwa
  3. Mafuta – kazi yake kubwa nikuleta joto mwilini. mfano:mafuta ya arizeti,siagi,mafuta ya samaki
  4.  Vitamini - kazi yake kubwa ni kulinda mwili. Mfano maembe,machungwa,nanasi,zabibu
  5. Madini mwili - Huusika sana katika kuwezesha mifumo ya mwili. Mfano:chumvi,aubuyu,dagaa,mboga zakijani (Vyanzo  vya baadhi ya madini)
  6. Maji - Huwezesha mifumo mbalimbali katika mwili.Mfano maji yakunywa
Ingawa nimetaja kazi kuu ya kila kirutubisho katika mwili,nivyema ujue kwamba hizo si kazi pekee za virutubisho hivyo.Tutachambua kila kirutubisho siku zijazo
Chakula na virutubisho
Vyakula vyote huwa nazaidi ya kirutubisho kimoja,virutubisho hivyo hotofautiana kwa wingi au kiasi.Mfano: Wali (mchele) una wanga asilimia 89,mafuta asilimia 4 na protini asilimia 7.
Ili mwili wa binadm hufanye kazi vizuri unaitaji kupata virutubisho vyote sita katika uwiano au kiasi sahihi,yani lishe bora.Uhitaji wa virutubisho hutofautina miongoni mwa watu wa makundi mbaimbalikama watoto, wazee,vijana,wajawazoito na wagonjwa wa magonjwa mbalimbali.Umri,jinsi na shughuli zako mtu zakila siku pia huchangia kuamua ale virutubisho katika uwiano gani.
Hitimisho
Huwezi kuongelea chakula bila kuongelea virutubisho vyake,wala huwezi kuongelea virutubisho vya chakula bila kuongelea chakula.chakula na virutubisho vyake ni vitu viwili visivyotengana.Hivyo basi,ili ukifahamu chakula ni lazima uvifahamu virutubisho,na ili uvifahamu virutubisho ni lazima ukifahamu chakula. Naamini  somo/makala hii imeleweka.katika makala zijazo,tutachambua kila kirutubisho kwa upana zaidi.