Feb
Ratiba ni kitu muhim sana katika maisha ya familia na hata kwa mtu binafsi.Tunajua familia kawaida huwa na watu wawili au zaidi,na pale mnapoishi wawili au zaidi kama familia ni muhim kuwa na ratiba za familia ili maisha na shughuli za familia ziwe katika utaratibu Fulani unaoeleweka.Kila familia huwa na ratiba zake
Ratiba ya muda wa kula ni ratiba muhim sana katika familia,lazima kuwe na utaratibu wa chakula,ijulikane chai ya asubui ,chakula cha mchana,chai ya jioni na chakula cha usiku vinaliwa saa ngapi au wakati gani.lazima kuwe na muda maalum kwa kila chakula,na muda huo unapofika basi chakula kitengwe mezani na watu wote wale kwa pamoja.
Kutokua na ratiba ya muda wa kula kunaleta shida ya upangaji wa matumizi ya chakula, kunaongeza gharama ya chakula na pia baadhi ya wana family huweza kukosa chakula.kila mtu anapokuja kula kwa muda anaotaka yeye,inamaana kila mtu atapakua kutoka kwenye sufuria,haijulikani nani amekula nani bado ,matokeo yake kuna watu wanaweza kosa chakula wakati huo huo garama ya chakula inaongezeka kwani ili kuweza kugawanya chakula ili mlaji aje ale kwa muda wake ni lazima upike chakula kingi,si rahisi kumpakulia mtu mboga ya majani kijiko kimoja ukamtunzia ,utataka utunza angalao robo bakuli.
Ratiba ya muda wa kula pia huipa familia muda wa kukaa pamoja na kufuraia chakula,kutaniana na hata kuongea mambo ya kifamilia kwani wana familia wote wanakua mezani.La msingi zaidi inawapa wazazi nafasi nzuri ya kuwafundisha watoto wao adabu za mezani na namna ya kula.zaidi inatoa mda na nafasi kwa mpishi kufanya shuguli zake zingine kwani anakua anajua ni saa ngapi atakua amemaliza kazi za jikoni
Ingawa Baadhi ya familia ni ngumu watu kula pamoja kutokana na ratiba zao za kazi,shule namengineyo.bado hii si sababu ya kufanya kusiwe na ratiba ya muda wa kula, kwani kuna wale wanaobaki nyumbani nao lazima wafate ratiba,pia siku za weekend kwakua watu wapo nyumbani basi ratiba iwepo na ifatwe.Lakini pia kila siku watu wapo nyumbani kwa ajili ya chakula cha usiku basi angalao chakula cha usiku familia ile kwa pamoja.
Nimeona familia nyingi sana zisizokua na ratiba ya chakula, na naweza kukwambia mambo machache juu ya familia hizi ambayo ni ya uakika: 1.chakula mara nyingi hakiwatoshi. 2.kuna tabia mbaya ya watoto kugombania chakula .3.chakula cha baba na mama kinatengwa pembeni mapema .4.Baba na Mama hula chakula kizuri kuliko watoto 5.chakula hakitengwi mezani. 6.watoto hawana adabu mezani na hawajui kula vizuri(kistaarabu).7.vyombo vichafu haviishi jikoni. 6.Dada wa kazi ndio mpishi mkuu wa familia.mambo ya aibu haya.
Nakupa mfano wa ratiba ya muda wa kula ya nyumbani kwetu,nikimaanisha kwa wazazi wangu.Nilizaliwa nikaikuta na imenikuza,hata leo ingawa siishi tena na wazazi bado ni ratiba ninayoifuata.Zaidi ni kwamba kila mwanafamilia bado anafata ratiba hii,hata wale walio owa na kuolewa wanaitumia kwenye familia zao.
Ni ratiba rahisi tu,Kifungua kinywa saa mbili asubuhi,mid-morning bite inaweza kua juice au matunda au snack yoyote saa tano ,lunch saa saba kamili mchana,chai ya jioni saa kumi na moja kamili jioni,chakula cha usiku saa mbili kamili usiku.wakati mwingine kuna kuwahi au kuchelewa lakini mara nyingi haitazidi nusu saa.
Kama familia yako haina ratiba ya muda wa kula basi wakati umefika wa wewe kuanzisha ratiba.Maisha lazima yawe na mpangilio,yawe na ratiba,Tukiwa watoto Mama yetu alipenda kutuambia kwamba mtu asiekua na mpangilio na ratiba katika maisha hawezi kufanikiwa kimaisha.
Anzisha ratiba ya chakula au kula Nyumbani kwako ili uboreshe maisha ya familia yako.
WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA USHAURI NA TIBA JUU TATIZO LINALOKUSUMBUA KIAFYA. PIA UWONAPO MAFUNDISHO YETU WAAMBIE WENZAKO PIA WAJIFUNZE KAMA WEWE. ASANTE.....!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni