Hivi karibuni tafiti zimeonyesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo.
Sasa kazi kwetu!! Tujitahidi kupunguza uwezekazo wa kupata magonjwa sugu. Pungunguza matumizi ya chumvi na vyakula vyenye chumvi nyingi. Yafuatayo yatasaidia kufikia lengo hilo:
- Punguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa kupika.
- Usiweke chumvi mezani (wengine huongeza hata bila kuonja chakula)
- Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa kutumia au kuongezwa chumvi
- wapo unanunua vyakula vilivyosindikwa, kama vya makopo au paketi, soma lebo kwa makini. Chagua vilivyoandikwa “hakuna chumvi iliyoongezwa”(“no salt added”)
- Tumia zaidi vyakula freshi unavyopika mwenyewe kwani unaweza kuthibiti kiasi cha chumvi unachotumia.
Kumbuka ni maisha yako na ufunguo wa kuingia katika mtindo bora wa maisha upo mkononi mwako. Jipende!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni