SOMA KWA UMAKINI MKUBWA HAPA....
Ni vema tukafahamu ugonjwa unaosumbua mwanadamu, na vilevile tukatambua aina ya vyakula ambavyo tukila vitatusaidia kuondokana na tatizo.
Mwili wa mwanadamu ulivyoumbwa: Mwili wa mwanadamu umeumbwa ukiwa mkamilifua, usiokuwa na tatizo lolote. Siku mtu anapozaliwa, wengi wetu tunazaliwa tukiwa hatuna tatizo lolote.
Kawaida mwili wa mwanadamu umeumbwa ukiwa mkamilifu kwa maana ya kwamba unatakiwa kujimudu wenyewe, pia kuwa na uwezo wa kujirejeshea afya ya mwili wake mwenyewe na kuweza kuishi maisha yasiyo na magonjwa.
Mwanadamu ameumbwa na anazaliwa na seli muhimu ndani ya mwili ambapo zina kazi kubwa ya kuhakikisha mwili upo sawa siku zote.
Seli hizi muhimu zinajulikana kwa jina la kitaalamu kama "adult stem cells"
Kadri tunavyokua hasa kuanzia miaka zaidi ya 25, uwezo wa mwili wa mwanadamu kuzalisha hizi seli hupungua. Hii husababishwa na stress (kimwili, kihisia, kimazingira) na lishe duni (vyakula na vinywaji vingi vimewekwa madawa kutoka mashambani hata viwandani).
Utumiaji wa dawa za magonjwa kwa muda mrefu, utumiaji wa sigara na vinywaji vikali huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu na kuua hizi seli.
Umwagaji wa damu kwa njia ya ajali au aina yeyote ile husababisha upotevu wa seli mwilini.
Seli hizi hutambulika kama "masta seli”ndani ya mwili wa mwanadamu ambazo baadae hubadilika jina kutokana na sehemu ambapo zimesafiri na kuweka makao. Kwa mfano zikifika kwenye ini zinaitwa “Liver cells”, kwenye ubongo zinaitwa “Brain Cells, kwenye macho zinaitwa “Eye cells… n.k
Bone Marrow:Seli hizi zinazalishwa na kiungo kijulikanacho kama bone marrow
Seli hizi kipingua kwenye kiungo cha ndani ya mwili husababisha kiungo hicho kutofanya kazi vizuri na kisha kiungo kupata tatizo. Mfano seli za kwenye kongosho zikifa au kupungua husababisha kongosho kutofanya kazi vizuri na hapo tatizo la sukari kwenye damu hutokea.
Kwa hiyo tukipata elimu ya vyakula itatusaidia kuwa makini na ulaji wetu ili tuishi mbali na magonjwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni