Jumamosi, 5 Aprili 2014

SHINIKIZO LA DAMU(HYPERTENSION)

Ni msukumo wa damu ulioko juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huitajika mwilini ili kusambaza chakula,oksijeni na kutoa uchafu.
Uanishaji wa shinikizo la damu

Uanishaji
Systolic BP
Diastolic BP
Kawaida (normal)
<120
<80
Prehypertension
120-139
80-89
Kali (mild hypertension)
140-159
90-99
Kali kiasi (moderate hypertension)
160-179
100-109
Kali sana (severe Hypertension)
≥180
≥110
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Aina ya kwanza: Asilimia 90-95 sababu huwa hazijulikani na kitaalamu huitwa primary or essential hypertension. Ingawa vitu vifuatavyo vimehusishwa kupelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu. Navyo ni:
  1. Uvutaji sigara
  2. Unene (visceral obesity)
  3. Unywaji wa pombe
  4. Upungufu wa madini ya potassium
  5. Upungufu wa vitamin D
  6. Kurithi
  7. Umri mkubwa
  8. Chumvi na madini ya sodium kwa ujumla
  9. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
  10. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Aina ya Pili: Asilimia 5 huwa na sababu dhahiri zinazopelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu na huitwa kitaalamu secondary hypertension. Na sababu hizi ni:
  1. Hali ya kukosa hewa usingizini (sleep Apnea)
  2. Kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu (Coarctation of Aorta)
  3. Saratani za figo (wilm’s tumor, renal cell carcinoma)
  4. Saratani ya tezi iliyo juu ya figo (pheochromocytoma)
  5. Ujauzito – wapo wakina mama wajawazito ambao hupata shinikizo la damu na huwa hatarini kupata kifafa cha mimba (eclampsia)
  6. Magonjwa ya figo (renal artery stenosis, glomerulonephritis)
Dalili
Mara nyingi huwa hamna dalili zozote, na kama zikiwepo mgonjwa huwa na dalili zifuatazo:
  1. Uchovu
  2. Maumivu ya kichwa
  3. Kuhisi mapigo ya moyo kwenda haraka
  4. Kichefuchefu
  5. Kutapika
  6. Damu kutoka puani
  7. Kutoweza kuona vizuri (blurred vision)
  8. Kusikia kelele masikioni
  9. Na mara chache kuchanganyikiwa 
Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu
  1. Kiharusi
  2. Moyo kushindwa kufanya kazi ( congestive heart failure)
  3. Madhara katika mshipa mkubwa wa damu ambapo ukuta wa ndani huchanika na damu hukusanyika katika ukuta wa mshipa huo(aortic dissection)
  4. Magonjwa ya mishipa ya damu
  5. Kushindwa kuona
  6. Athari katika ubongo 

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni