Leo hii tunaangalia maradhi ya fangasi aina ya hamira (yeast) yanayoshambulia kinywa na koo ambayo kwa kitaalam ,oral candidiasis.
Utando wa kinywa (Oral Candidiasis)
Utando huu wa kinywa ni maradhi yanayosababishwa na fangasi aina ya hamira ambao hushambulia eneo la ndani la kinywa na koo la kumezea chakula.
Fangasi hawa hushambulia kinywa na koo kwa hali ya kawaida na huwa na makazi yao kwenye maeneo haya pamoja na sehemu mbalimbali katika mfumo wa mmeng`enyo wa chakula na pia hupatikana kwenye ngozi.
Kinga ya mwili wa binadamu pamoja na vimelea vinavyokaa mwilini aina ya bakteria huzuia fangasi hawa wasiongezeke kiasi cha kugeuka na kuanza kushambulia maeneo hayo ya koo na kinywa.
Hata hivyo, inapotokea uwiano huu wa kinga ya mwili na bakteria kushindwa kuzuia ongezeko la fangasi, basi fangasi hao huongezeka na kuwa wengi na hapo ndipo husababisha utando ambao huonekana kwenye kinywa na hata koo la chakula la mgonjwa.
Sababu za maradhi
Idadi kubwa ya fangasi aina ya kandida (candida) katika maeneo ya kinywa na koo husababisha utando huu.
Jinsi na nani hushambuliwa
Maradhi haya ni kawaida kuonekana kwa watoto wachanga. Maradhi haya yanatokea zaidi kwa watoto wachanga kutokana na hali ya kutokuwa na uwiano sahihi kati ya kinga ya mwili wa mtoto, aina ya bakteria pamoja na fangasi hawa wanoitwa kandida.
Maradhi haya pia huweza kutokea kwa watu wazima na mara zote hutokea baada ya kutokea mabadiliko yaliyosababisha kuvurugika kwa uwiano kati ya kinga ya mwili, bakteria walioko kwenye eneo la kinywa na koo pamoja na vimelea vinavyosababisha utando huu, yaani kandida.
Viashiria hatarishi
Viashiria hatarishi vinavyomweka mtu kwenye hatari ya kupata maradhi haya vinafanana kabisa na sababu zinazomfanya mtu kupata maradhi haya.
Maradhi haya kwa kawaida kama nilivyoeleza hushambulia watoto wachanga, inapotokea yakatokea kwa mtu mzima basi mara nyingi lazima kuwe kuna viashiria hatarishi kama vifuatavyo:
-Watu wenye upungufu wa kinga kwa sababu yoyote ile wako kwenye hatari ya kupata maradhi haya. Mfano, watu wenye maradhi ya muda mrefu kama saratani, kisukari na yale yanayosababisha kinga kushuka kama Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).
-Wanawake wajawazito (Ujauzito huweza kusababisha kinga kushuka)
-Watu wanaokunywa dawa kwa muda mrefu, hususan dawa za antibaiotiki, dawa za kutibu saratani na dawa za maradhi mengine ya muda mrefu.
-Sonona na msongo wa mawazo wa muda mrefu (hushusha kinga pia)
Je, maradhi haya huambukiza?
Maradhi haya si ya kuambukiza ingawa mtoto mchanga mwenye maradhi haya huweza kusambaza maradhi kwenda kwenye titi la mama kwa njia ya kugusa moja kwa moja wakati wa kunyonya.
Alhamisi, 12 Desemba 2013
Jumapili, 8 Desemba 2013
KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI
Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.
Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.
Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi hufariki dunia nchini humo kutokana na kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.
Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.
Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari, hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya kwa siku zaidi ya 50 za aina zote una faida, ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani, kansa ya tezi dume ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali, pamoja na nyanya 50 kwa siku zilizoiva vizuri au kupata FOOD SUPPLIMENT ZINAZOTENGENEZWA KWA KIWANGO HICHO CHA NYANYA NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA MBALIMBALI.
Virutubisho kwa watoto umri Miezi 6 hadi Miaka 5
Kwasasa serikali imezindua kampeni ya virutubisho kwa watoto wenye umri wa miezi 6-miaka 5. Kampeni hii ambayo inafadhiliwa na USAID na Wizara ya Afya nia yake hasa ni kuhakikisha kwamba watoto hawa wanapata virutubisho muhimu kwaajili ya ukuaji wao.
Mapungufu yaliyopo::
• Sio wazazi/familia zote zinazomudu kuwa na mlo bora kila siku hivyo kumpelekea mtoto kukosa virutubisho muhimu kwaajili ya ukuaji wake.
• Watoto kwa kawaida yao hawapendi kula baadhi ya vyakula hivyo kuwafanya watoto wengi kuwa na viriba tumbo kwa kukosa baadhi ya virutubisho muhimu.
Umuhimu wa virutubisho hivi:
• Huongeza damu
• Huongeza hamu ya kula
• Huondoa unyafuzi na kiriba tumbo kwa mtoto
• Huondoa udumavu wa mwili na akili wa mtoto
• Huongeza akili kwa mtoto
• Huweka kinga ya magonjwa mbalimbali dhidi ya mtoto
• Kwa wale ambao wana immuno compromise basi virutubisho hivi huwafanya afya zao kuborea zaidi na hivyo kupunguza unyongevu.
• Hurutubisha ngozi, kucha na nywele
• Humfanya aweze kuona vizuri
• Hurutubisha mifupa ya mtoto na meno
• Huongeza antioxidants nmwilini hivyo kuweza kupunguza kiasi cha macromolecules ambazo ni sumu ndani ya mwili wa mtoto.
• Huongeza uchangamfu wa mtoto na kumfanya awe na mwonekano bora kiafya.
Watoto gani hasa wanaohitaji kupewa virutubisho hivi?
• Watoto wote wenye umri kuanzia miez6-miaka 5
• Watoto ambao wacoimmuno compromised
• Watoto wavivu wa kula
Namna ya kutumia virutubisho hivi:
Vvirutubisho hivi vina aina zaidi ya 12 za virutubish muhimu ndani ya mwili wa mtoto na vyote vimetengenezwa kwanamna ya teknolojia ya kisasa zaid na hivyo kuweza kufikia viwango vinavyotakiwa kitaalamu.
Jumamosi, 7 Desemba 2013
Umuhimu wa Calcium na Magnesium kwa mama Mjamzito na anayenyonyesha
Mama mjamzito au anayenyonyesha anahitaji 1600 hadi 2000 mg za calcium kila siku. Kwa sababu wanawake wengi hawali vyakula bora huwa wanaishia kupata 600mg kwa siku ambazo hazitoshi. Calcium ni muhimu sana kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Kwa mama
calcium inasaidia kuweka blood pressue sawa na kupunguza kupata magonjwa kama
preeclampsia ugonjwa unaoweza kumpata katika miezi ya mwisho ya ujauzito.
Calcium pia inamsaidia mama kuweza kupata usingizi mzuri usiku na kupunguza
kuuma kwa miguu. Hivyo ni vizuri kupata chakula chenye calcium kabla ya kulala.
Kwa mtoto
afya njema inapatikana pale anapopata mg 200 hadi 300 ya calcium kwenye
skeleton yake wakati wa trimester ya tatu. Pia kiwango hicho kinapatikana
kutoka kwenye maziwa ya mama pale atakapozaliwa na kunyonya. Mama akipata
kiwango kinachotakiwa cha calcium itamsaidia mtoto kusawazisha blood pressure
yake pindi atakapozaliwa.
Mwili wa
mama mjamzito unauwezo zaidi wa kuweka calcium kwenye mifupa na mwili kuliko mwanamke asie mjamzito. Hii
ni njia ambayo inamsaidia mwanamke mjamzito kuhimili mahitaji ya mtoto katika
trimester ya tatu na baada ya kujifungua anaponyonyesha. Kama mama ataweza
kupata calcium nyingi wakati wa ujauzito basi hata baadaye akizeeka anaweza
kujikinga na magonjwa ya osteoporosis(kulainika kwa mifupa) ambayo hutokea
katika miaka hiyo.
Magnesium
Magnesium
na Calcium inasaidiana kwa kiasi kikubwa katika kuendesha shughuli mbali mbali
za mwili. Kukosekana kwa Magnesium ya kutosha wakati wa ujauzito kunaweza
kusababisha kupata uchungu kabla ya muda, na kuongezeka kwa matatizo ya nerve
kwa mtoto kama ya cerebral palsy.
Vyakula
vyenye Calcium
Maziwa na
vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini na mitindi vina Calcium nyingi za
kutosha. Vyakula vingine ni pamoja ufuta, tuna, kale, mustard greens, maharage,
mayai, spinach na whole grains.
Vyakula
vyenye Magnesium
Mboga za
majani yenye rangi za kijani iliyokolea, whole grains, vyakula jamii ya karanga
na njegere. Pia kula vyakula na juisi ya machungwa itakupa vitamin c ambayo
itawezesha mwili kutumia Calcium, Iron na folic acid kwa ufanisi zaidi.
Kuliko
kutumia vitamin supplement za calcium na magnesium ni vizuri mama akijitahidi
kupata hivi virutubisho moja kwa moja kutoka kwenye chakula kwani baadihi ya
madawa yanauwezo kusababisha lead poisoning kama zikitumiwa kwa muda mrefu.
Mama kupata magnesium ya kutosha kutamsaidia mtoto
wakati wa labor. Mdundo wa moyo wa mtoto wakati wa labor unakuwa uko
sawa na pia kuzuia matatizo mengine kwa mtoto wakati wa labor.
Jumatano, 4 Desemba 2013
FAHAMU KWANINI MTOTO WAKO HAKUI KATIKA UWIANO ULIO SAHIHI
Kiafrika Familia hukamilika pale wanandoa wanapopata mtoto au watoto,na furaha huitawala nyumba.Watoto hupendeza na kua na afya nzuri na wenyefuraha pale wanapokula vizuri wakashiba na wakapata usingizi wakutosha .Leo nawamulika watoto wenye umri wa mwaka mmoja adi mine(1-4)
Katika pita pita yangu na kuishi katika jamii yetu ya
watanzania,nimegundua kwamba watoto wengi hawakui katika uwiano ulio
sahihi,nikimaanisha umri,urefu na uzito haviwi katika uwiano ulio
sahihi.wataalamu wa mambo ya afya wanakanuni zao za kupima uwiano
huu.chanzo cha tatizo hili ni Lishe mbaya kwa mtoto na mtoto kukosa
usingizi wakutosha.
Lishe mbaya kwa watoto husababiswa na ukosefu wa Elim na ufaham mzuri wa vyakula na lishe bora wa wazazi,lakini kwa upande mwingine hali ya wazazi kutokujali watoto wao kwa sababu moja au nyingine pia huchangia tatizo hili.Mtoto kukosa usingizi wakutosha au kushindwa kulala vizuri pia huchangiwa sana na njaa,mtoto asiposhiba vizuri hawezi kulala vizuri.Kelele,kumchelewesha mtoto kulala na kukosa ratiba ya mtoto kulala pia huchangia mtoto kukosa usingizi wakutosha.
Watoto wa mwaka mmoja adi mine(1-4)wanaitaji masaa 14 ya usingizi kila siku.wanatakiwa kupata usingizi wa mchana wa kati ya saa moja adi masaa matatu na nusu(1-3.5),usiku wanatakiwa kulala kati ya saa moja na saa tatu(1-3) na asubui waamke kati ya saa kumi na mbili na saa mbili (12-2) Ni kosa kabisa mtoto kua macho baada ya saa tatu,endapo mtoto wako huwa macho baada ya saa tatu ni kiashirio kwamba anashida au tatizo Fulani.
Asilimia kubwa sana ya watoto hawapati mboga na matunda yakutosha katika lishe zao.Watoto wenye ukosefu wa vitamin muhim,madini mwili,na aside mafuta za muhim (essential fatty acids) huwa na akili zilizozubaa na hawafanyi vizuri darasani na wana asili ya ukali,watoto wengine huwa na unene wa ziada ambao pia husababishwa na lishe mbaya,Lakini kubwa kabisa mtoto huyo hawezi kukua katika uwiano ulio sahihi.
Watoto wanapofikia umri wa kuanza kwenda madarasa ya awali ndio ule wakati ambao mtoto hurefuka na mwili wake huwa na nguvu nyingi,huu ndio wakati ambao wanaanza kujifunza kujitegemea na kutengeneza wasifu binafsi(personalities).Mtoto huanza kubagua chakula,na kuamua anapenda au apendi chakula kipi. Watoto wanaobagua chakula huwa kwenye hatari kubwa ya kukosa virutubisho maalum vinavyoitajika kuwezesha ukuaji wao,kwani virutubisho hivyo huchangia ukuaji bora wa akili,mwili,na hata hisia.
Ukuaji sahihi wa mifupa na meno kwa watoto umekua ni changamoto kubwa sana,kwani asilimia kubwa ya watoto hawapati vitamini muhim,madini mwili na asidi mafuta ya kutosha kuwezesha ukuaji wao.
Nini maana ya Lishe Bora(balanced diet)?ni lishe yenye virutubisho vyote kwa kiasi sahihi na uwiano sahihi ili kuwezesha afya bora.Virutubisho vyote sita lazima viwepo: wanga,protini, mafuta ,vitamin, madini mwili na maji.kwa ujumla hii ndio maana ya lishe bora,lakini kitaalam zaidi,wataalam wa afya husema lishe bora hutofautiana kati ya makundi mbalimbali ya binadam kutoka na uhitaji wa miili yao katika kipindi Fulani,wakimaanisha inayoweza kua lishe bora kwa mtoto mchanga haiwezi kua lishe bora kwa mtoto wa miaka kumi na mbili kwani miili yao inauhitaji tofauti,au kilicho lishe bora kwa mama mjamzito hakiwezi kua lishe bora kwa mgonjwa wa Moyo kwani wao pia miili yao inauhitaji wa tofauti.
Kwa mantiki hiyo basi ili lishe ya mtoto wa mwaka mmoja adi miaka minne iitwe lishe bora,ni lazima iwe na virutubisho vifuatavyo
Vitamini C
Mwili wa binadm hauwezi kujitengenezea vitamin C,hivyo ni lazima ipatikane katika lishe.Vitamini C huwezesha utendaji bora wa akili,huusika katika kuendesha hisia,pia huuwezesha mwili kunyonya madini joto.kila siku mpe mtoto juisi ya machungwa au apple(isiwe kali)na apate Nyama au samaki.Vitamini C hupatikana kwenye machungwa,mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo na Apples.
Vitamini A
Vitamin A hutengeneza Meno na Ngozi yenye afya nzuri na kufanya mtoto aone vizuri.inapatikana kwenye mayai,nyama,maziwa,cheese,karoti na mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.

Vitamin D
Vitamini D huwezesha mwili kunyonya calcium,bila calcium mifupa haiwezi kukua katika uwiano sahihi wala kuwa na nguvu hivyo mtoto anaweza kupata matege na kua na mifupa dhaifu.Vitamini D nyingi hutoka kwenye mwanga wa jua,si lazima liwe jua kali.Ingawa vitamin D inapatikana pia kwenye Mayai na samaki wenye mafuta ni vyema kuhakikisha mtoto anatoka nje kucheza kila siku ilia pate mwanga wa jua ambao utampa vitamin D ya kutosha.
Madini Chuma(iron)
Madini chuma hutengeneza seli za damu,hasa seli nyekundu ambazo hutumika kusafirisha oxygen katika mwili wa mtoto:bila oxygen yakutosha mtoto hawezi kucheza,kama mtoto wako anachoka wakati wote kuna uwezekano mkubwa wa kua na upungufu wa madini joto.Madini joto hupatikana kwenye nyama,samaki,mbegu za maboga,brown bread,maharage na mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.

Folate (asili yake familia ya vitamin B)
Huusika sana katika utengenezaji wa seli mpya,hutengeneza DNA,ni ya muhim sana katika ukuaji wa vichanga na watoto wadogo.Folate inapatikana katika mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo,maharage,karanga ,korosho,hata ivyo spinachi ndio chanzo kikubwa kabisa cha folate.
Asidi mafuta Muhim(Essential Fatty Acids-EFA’s)
Mwili hauwezi jitengenezea kirutubisho hiki,ni lazima kipatikane kwenye lishe,kuna familia mbili za EFA’s-Omega 3 na omega 6_ambazo zinaitajika kuwezesha utendaji mzuri wa ubongo,utendaji bora wa kinga za mwili,na kuwezesha afya akili kwa ujumla.hupatikana kwenye oily fish,na flax oil.Kama mtoto wako anashindwa kutulia darasani,anashindwa kukumbuka vitu,analala kwa shida au hapati usingizi vizuri basi kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kua na upungufu wa Omegas.Nashauri matumizi ya Suppliments(dawa zinazobeba virutubisho) kwani vyanzo vya omegas ni vichache.
Calcium
Madini ya calcium ni kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno na pia inaendesha mfumo wa mapigo ya moyo na inasaidia damu kuganda kwa haraka.Bila vitamin D,mwili hauwezi nyonya calcium.calcium inapatikana kwenye mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo,karanga,maziwa ya Ng’ombe,na vyakula venye asili ya mbegu na katika maji(hard water)
Fibre(Nyuzi nyuzi)
Fibre ni muhim sana katika usagaji wa chakula mwilini.watoto wengi hupata shida kupata aja kubwa (constipation )kwa ajili ya ukosefu wa fibre katika lishe zao.ili kuepuka tatizo hili,hakikisha mtoto anapata fibre ya kutosha katika lishe yake.Matunda,mboga za majani,unga usiokobolewa na karanga ni vyanzo vizuri vya Fiber.
Maji
Mtoto anatakiwa kunywa maji mengi,ili kuzuia constipation na kuepuka kuishiwa maji mwilini,apate kati ya glasi 6 adi 8 kwa siku.
Kwa ujumla matunda na mboga za majani na matunda ni vyakula muhim sana kwa afya na ukuaji bora wa mtoto.Fanya matunda na mboga za majani sehem kubwa ya mlo wake.badala ya kumpa mtoto biskuti na soda anapotaka kitu cha kula kula,mpe matunda,au juice au smoothie au supu ya mboga.kwa kufanya hivyo unamuweka mtoto wako salama.
Kwa kumalizia niwaseme wale wakinadada na kinamama wanajiita wa dot com, wanaodhani kumlisha mtoto chipsi na kuku,soseji,tambi,na vyakula vya makopo ndio uzungu.laaa!mnatia aibu.pika chakula kizuri na fresh nyumbani umpe mtoto,zingatia virutubisho ambavyo mtoto anaitaji.Pia niseme na wale kinadada na kinamama ambao wamekariri kua chakula cha mtoto ni uji,mtori,wali wa maziwa na maziwa.mtoto anapofikisha mwaka mmoja anakua katika uwezo wa kuanza kuonjeshwa vyakula vingine.Inashangaza pale unapomkuta mama bado anamsagia mtoto wa miaka mitatu chakula kama ndizi na viazi.Mpe mtoto chakula cha kawaida kabisa kama nyama,maharage,mayai,karanga,ugali,mboga za majani,ili mradi tu kiwe na virutubisho vyote mtoto anavyoitaji.
Ni hayo tu kwa leo,chukua atua mpe mtoto wako lishe bora.

- Wanga:ugali,wali,viazi,mkate
- Mboga za majani na matunda kwa wingi-lenga kumpa mara tano kwa siku
- Protini:nyama,samaki,mayai,maharagenjegere(angalao ale samaki mara mbili kwa wiki)
- Vyakula vyenye asili ya maziwa:maziwa,yoghurt,cheese (lazima ale kila siku)
- Mafuta.sio mafuta ya wanyama bali mafuta yatokanayo na mimea(saturated fats)

CHAKULA NA VIRUTUBISHO
Ndugu wapendwa ni mataumaini yangu kuwa mu wazima, poleni sana na mihangaiko ya hapa na pale ya kimaisha.
Leo ningependa kuleta mada ihusuyo vyakula tulavyo na virutubisho tuvipatavyo:
Chakula
hutupa nguvu na virutubishi ambavyo mwili huhitaji ili kudumisha afya
na maisha,kukua na kustawi, kusonga, kuchapa kazi kucheza na kujifunza.
Mwili huhitaji virutubishi vya aina nyingi - protini, wanga, mafuta, na madini - na hivi hutokana na vyakula tulavyo.
- Protini zinahitajika kujenga na kudumisha misuli, damu, ngozi na tishu na viungo mwilini.
- Wanga na
mafuta kimsingi hutupa nguvu, ingawa mafuta mengine pia huhitjika
kama vifaa vya ujenzi na kuusaidia mwili kutumia baadhi ya
vitamini.
- Vitamini na
madini huhitajika kwa viwango vidogo zaidi kuliko protini, mafuta
na wanga, lakini navyo ni muhimu kwa lishe bora. Vinasaidia mwili
kufanya kazi vizuri na kuwa wenye afya. Baadhi ya madini pia huwa
sehemu ya tishu za mwili, kwa mfano, kalisiamu na floridi ilyo
katika mifupa na meno na chuma hupatikana katika damu.
- Utembo na maji safi pia huhitaji kwa maakuli mazuri.
Vyakula vyote vina virutubishi lakini vyakula mbalimbali huwa pia na tofauti vya virutubishi mbalimbali.
- Vyakula vyenye wingi wa protini ni aina zote za nyama, kuku, samaki, maharagwe, dengu, maharagwe soya, njugu, maziwa, chizi, maziwa mgando na mayai.
- Vyakula vyenye wingi wa kabohidrati ni mchele, mahindi, ngano na nafaka, aina zote za viazi vikuu na mzizi yenye kabohidrati na sukari.
- Vyakula vyenye wingi wa Shahamu ni
mafuta, baadhi ya nyama na bidhaa za nyama, mafufa ya nguruwe,
siagi, samli na baadhi ya bidhaa za maziwa, siagi kutokana na ute
wa njugu, baadhi ya aina za samaki, vyakula vya jamii ya njugu nasoya.
- Vyakula vyenye wingi wa vitamini A ni mboga zenye kijani kilichokolea, karati, viazi vitamu vyenye njano iliyokolea, boga, embe, papai, mayai na ini.
- Vyakula venye kijani kilichokolea , jungu, maharagwe, mbaazi, nafaka, nyama, samaki na mayai.
- Vyakula vyenye wingi wa vitamini C ni matunda na kiasi kikubwa cha mboga, pamoja na viazi.
- Vyakula vyenye wingi wa ayani ni nyama, samaki, njugu, maharagwe, mbaazi, mboga zenye matawi ya kijani kilichokolea na matunda yaliyokaushwa.
Jumapili, 17 Novemba 2013
Lishe Nzuri Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Usahaulifu Uzeeni

Wataalamu
wameonyesha ushahidi zaidi kwamba chakula chenye mafuta ya samaki na
mboga mboga kinaweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya
usahaulifu baadaye katika maisha. Uchunguzi uliotolewa na jarida la
Marekani unaonyesha kwamba, 'vyakula vya Mediterania' au utumiaji wa
muda mrefu wa vyakula vyenye beta-carotene kunaweza kuzuia magonjwa
hayo.
Aina
zote hizo za vyakula vina antioxidanti ambazo ni chembe chembe
zinazozuia vitu au vyakula kuoza vinapoungana na oksijeni. Antioxidanti
huuepusha ubongo kuharibika. Taasisi ya Alzheimer imesema kuwa watu
wengi wanaweza kupunguza hatari ya magonjwa hayo kwa kula vyakula bora.
Uchunguzi
wa kwanza uliofanywa na jarida la Neurology umechunguza vyakula vya
watu 8,000 wasio na magonjwa wanawake na wanaume walio na umri wa zaidi
ya miaka 65.
Uchunguzi
huo umeonyesha kwamba, wale wanaokula vyakula vyenye mafuta yenye
omega-3, ambayo hupatikana katika baadhi ya mafuta na samaki, watu hao
wameonekana kuwa hawaweza kupata magonjwa hayo katika kipindi cha miaka
minne inayofuata.
Watu
wanaokula samaki kwa akali mara moja kwa wiki wana punguza uwezekano
huo kwa asilimi 40 huku wale wanaotumia mbogamboga mara moja kwa siku
hupunguza uwezekano huo kwa asilimia 35.
Beta-carotene ni kemikali ambayo huipa rangi karoti ambayo ni aina ya ant-oxidanti.
Beta-carotene ni kemikali ambayo huipa rangi karoti ambayo ni aina ya ant-oxidanti.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)