Jumapili, 6 Oktoba 2013

Faida za tikikiti maji kiafya




KWA UFUPI
  • Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi


Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi;  na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.
  Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha  lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
 Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Tikiti pia lina  amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa  peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.

SABABU ZINAZOWAPELEKEA WATU KUSHINDWA KUFANYA DIET.

Ni jambo lisilofichika kwamba watu wengi hujaribu kufanya diet pasipo mafanikio.Wengi huanza kwa nguvu nyingi na malengo makubwa lakini juhudi hizo hazifiki mbali.

031
Ukweli nikwamba kufanya diet ni ngumu,na kuna mambo mengi yanayochangia ugumu huo:
  1. kutokujua aina ya vyakula vinavyofaa – Wengi hushindwa kufanya diet kwa muda mrefu kwani hajui chakula gani humfaa zaidi,matokeo yake wengi hushinda njaa au laa hula matunda na mboga tu na mwisho wasiku njaa huwa kali,mwili hudhoofika na wanaacha diet.
  2. Gharama ya vyakula hivyo – Diet nyingi huwa na ratiba ya kula pamoja na aina ya vyakula unavyotakiwa kula kwa kila mlo.Mara nyingi vyakula hivi huwa na gharama kubwa au laa huongeza gharama katika familia na kufanya wengi washindwe diet hizo.
  3. Njaa kali – Diet nyingi huelekeza mtu ale chakula kidogo sana,na wakati mwingine vyakula hivi havishiki tumbo kwa muda mrefu au laa mtu hapati kushiba.hivyo huwa na njaa kali muda wote.hali hii uchosha na huwa kama mateso,wengi huacha diet kwa kushindwa kuvumilia hali hii
  4. Hamu ya kula vyakula wanavyokula wengine hapo nyumbani – Harufu nzuri na muonekanoo wa  chakula wanachokula wengine hapo nyumbani mara nyingi huleta hamu ya kula na pia huongeza njaa,hii ufanya wengi waharibu diet zao kwa kula vyakula hivyo ambavyo si sehem ya diet zao
  5. Ugumu wa kuacha vyakula unavyovipenda – Ni wazi kabisa kwamba ni ngumu sana kuacha kula vyakula unavyovipenda na ulivyovizoea.Ni ngumu zaidi kama kuna aina fulani ya chakula ambayo imekua kama kilevi kwako.Mfano kuna watu asipokunywa soda fulani au juice fulani basi siku kwake haijaisha.
  6. Kuvunjwa moyo na wanaokuzunguka – Mara nyingi watu wanaokuzunguka hukuvunja moyo kwa maneno yao,hasa pale unapofanya juhudi alafu wanakwambia hakuna mabadiliko au laa wengine hudiriki hata kukwambia wewe huwezi kupungua
  7. Kutaka matokeo ya haraka – wengi wanataka kupunguza mzito mkubwa kwa muda mfupi jambo ambalo si rahisi,Ingawa juhudi zako huchangia uaraka wa kupungua
  8. Uzito mkubwa  – uzito mkubwa sana unafanya Mtu aone  haiwezekani kupungua kwani inachukua muda mrefu kuona matokeo makubwa.Ni vyema kujua kua kila hatua ndogo unayochukua husaidia,na matokea huja baada ya muda
  9. Kero – mara nyingi marafiki na ndugu huwa kero kwa maneno yao hasa pale wanapotaka kukwambia fanya nini na uache nini ili upungue.Ni vyema kujua kwamba unapoona ndugu au rafiki ameamua kupunguza uzito basi anasababu za kufanya hivyoo na anajua ni nini afanye au asifanye ili apungue.Naamini kwamba pale anapoitaji msaada wako basi ataomba msaada.Wazungu husema STAY OUT OF OTHER PEOPLES BUSINESS
Ni haya na mengine mengi yanayochangia wengi kushindwa kufanya Diet.Mimi ni mmoja wa wale waliokumbana na hayo yote na kwa njia moja au nyingine yalinirudisha nyuma sana na kunikera.
Baada ya muda mrefu wa kutafuta namna ya kufanya diet endelevu ,kusoma vitabu vingi na kufuata program nyingi za kupunguza uzito atimae nilipata diet ambayo inaweza kukabiliana na changamoto hizo zote nilizozitaja.

LIKE, COMMENT, NA SHARE KAMA UMEJIFUNZA NA KUELEWA SOMO HILI.
KWA MAELEZO NA USHAURI ZAIDI PIGA SIMU +255713354389 / 0752133700

Kula zabibu usipatwe na ugonjwa wa moyo





Wadau msichoke na mimi kuzungumzia ugonjwa wa moyo, au nisiseme mimi, bali niseme wataalamu ambao kila siku wamekuwa wakifanya majaribio na kutuelewesha vyakula au njia zinazotuepusha na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu ugonjwa wa moyo kweli ni tishio duniani kote. Ni wiki iliyopita tu mfanyakazi mwenzangu ambaye nilikuwa naye kazini hadi nyakati za mwisho za kazi, siku ya pili nakuja kazini naambiwa kafariki dunia kwa mshituko wa moyo. Masikini baba wa watu!!, huku akiwa anayetegemewa na familia, akiacha mke na mtoto ameondoka kama utani tena kwa kufumba na kufumbua. Baada ya kutoka kazini alikaa juu ya kochi na kujiegemeza akisubiri atengewe msosi, lakini hapo hapo aliaga dunia. Msosi ulipotengwa na mkewe kumuamsha ale akidhani labda amepitiwa na usingizi, aliona haamki tena, na ndipo walipomkimbiza hospitalini. Huko waliambiwa ameshakufa zamaaani kutokana na mshituko wa moyo!.
Sasa hali ni hii, na hivi karibuni uchunguzi mpya umeonyesha kwamba kula zabibu au vyakula vyenye zabibu ndani yake kunapunguza shinikizo la damu, husaidia moyo kufanya kazi zake vyema na kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliotolewa kenye mkutano wa Majaribio ya Bayolojia huko California, zabibi zina uwezo wa kupunguza shinikio la damu, husaidia mwili uweze kuvumilia sukari (glucose tolorance) na kupunguza kiwango cha mafuta aina ya triglycerides mwilini ambayo ni chanzo cha matatizo ya moyo.



Wataalamu wanasema zabibu pia zinaweza kupunguza uvimbe, uharibivu unaotokana na free radicals zinazozalishwa mwilini na shinikizo la moyo. 
Kwa ujumla zabibi zinazuia hali inayoitwa Metabolic Syndrome suala ambalo linatokana na mada za phytochemicals zilizoko kwenye matunda hayo. 
Metabolic Syndrome ni mchanganyiko wa matatizo ya kitiba ambayo yanaongeza uwezekano wa kupatwa na maradhi ya mishipa ya damu pamoja na kisukari.
Hivyo wataalamu wanatushauri tule zabibi au kuongeza zabibu katika vyakula wanavyokula kila siku, ili tujikinge na ugonjwa wa Metabolic Syndrome, ugonjwa wa moyo na kisukari aina ya pili. 
Haya shime tule zabibu kwa ajili ya afya zetu!.

Ijumaa, 4 Oktoba 2013

Uzito mkubwa si sahihi kwa afya na urembo wako


KILA siku tunazungumzia masuala ya kuweka ngozi safi na sura bomba lakini mara zote huwa tunasahau kuzungumzia uzito ambao ama hakika ni kitu kibaya kuliko kitu chochote kile. Uzito ni sawa na uvutaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho. wataalamu wa afya na urembo wanasema wazi kuwa kuwa mnene kunapunguza siku namna ya kujiweka sawa katika masuala mbalimbali ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani. Wataalamu wanasema kwamba kuwa mzito kunapunguza maisha yako kwa miaka mitatu na haya yamesemwa na mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit ya chuo kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza. Uzito huu ni ule unaokuwa mara tatu ya uzito ambao unatakiwa mtu awe nao kutokana na urefu wake,umri na pia afya yake. Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150, mtu huyu anapunguza umir wake wa kuishi hapa duniani kwa miaka 10. Kwa maelezo mengine uzito wa aina hii ni sawa na uvutaji wa sigareti ambapo pamoja na kuchakaza ngozi pia hupunguza maisha ya mtu kwa miaka kumi. Ndio kusema katika urembo pamoja na kupiga vita sigareti uzito wa kuchusha nao lazima upigwe vita. Kwa waafrika kuwa mnene ni bomba, pamoja na ukweli wa kiutamadunikwamba kuwa mnene ni kutamu kwani unakuwa na nyama za kushikwa lakini ni vyema watu wakatambua kwamba uzito wa kuchusha yaani mara tatu ya ule unaostahili kuwa nao ni hatari kubwa kwa maisha yako. Onyo hili la wataalamu limefanywa baada ya uchunguzi kwa watu 894,576 waume kwa wake katika tafiti 57 zilizofanywa. ingawa tafiti hizi zilifanywa kwa watu wa Kaskazini mwa Marekani na Ulaya kwa watu wenye ujazo wa 25 (BMI) hata hapa nchini watu wanastahili kuangalia suala la uzito wao. Kwa taarifa yako uzito wa kuchusha huleta tatizo la figo, ini na aina kadha za kansa na pia hyuleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi. Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na pia kuleta mizania dhaifu ya rehemu na kusababisha shida katika mwenendo wa damu. Wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza hatihati ya kifo wakatiw nawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hati hati ya kifo kwa asiulimia 78.

Jumanne, 1 Oktoba 2013

Bamia: Ina umuhimu katika macho na ngozi yako.


Bamia inafahamika kwa wengi  katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo.
Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili.
Bamia ina majina lukuki, wengine huiita okra, kwa jina lisilo rasmi la Kiingereza huitwa, ‘lady finger’ au gumbo.
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’
Kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa mikavu kama Dodoma, Singida katika Tanzania.
Kwa kawaida huwa na rangi ya kijani iliyokolea na hukua hadi kuwa na urefu wa sentimeta tano hadi 15.

 Zijue faida za bamia kiafya:
Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi,  sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake.
Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi.  Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara kutaimairisha mwanga katika macho yako.
Wingi wa vitamini A huzuia maradhi  yatokanayo na virusi kama mafua.

Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi.
Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo.  Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Ugonjwa wa Moyo

Magonjwa ya moyo yamezidi siku hizi. Mishipa ndani ya moyo huweza kufungana(kuziba) kwa mafuta na kuleta mshituko wa moyo au kupooza.


Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa Moyo:
  • Matunda, maboga na nafaka.
  • Usile vyakula vyenye mafuta mengi. Hivi ni kama vyakula vimekaangwa ama vichopochopo vilivyo na mafuta ya nazi.
  • Usile chakula kilicho na cholestoral nyingi. Cholestoral ni mafuta ya nyama na inakuwa kwa vyakula kama nyama, mayai, siagi na mziwa ya krimu.
Ishara za ugonjwa wa Moyo
Jambo la huzuni ni kwamba, hutapata dalili zozote za ugonjwa wa Moyo mpaka wakati mishipa ya damu kwa moyo imezibika. Kwa hivyo, kuwa na ratiba ya kumuona daktari mara moja kwa mwaka ili akague moyo wako. Unapohisi uchungu kifuani hasa baada ya zoezi ngumu, haraka muone daktari.

Dharura! Labda unashambulizi la ugonjwa wa Moyo ukiwa na:
  • Uchungu kifuani
  • Maumivu ya kifua yanayo tambaa mikononi, mabegani, mgongoni na kadhalika
  • Shida kupumua
  • Kisunzi, kutapika na maumivu yanayosambaa tumboni.
WASILIANA NASI KWA 0713354389 / 0752133700 KWA USHAURI ZAIDI.

Jumatatu, 30 Septemba 2013

FAIDA ZA MAHARAGE YA SOYA


Maharage ya soya ni miongoni mwa vyakula maarufu nchini Tanzania, wengine wanavipenda na wengine hawavipendi, hiyo inatokana na mtu kujua au kutokujua umuhimu wa zao hili muhimu kiafya.

Nchini China, zao hili limekuwa sehemu ya mlo kamili wa wananchi wake kwa karne nyingi. Kama inavyojulikana, Soya ina faida nyingi za kiafya kutokana na kuwa na kiasi kingi cha protini na madini. Soya huweza kutumika ikiwa katika aina mbalimbali ya vyakula.

Soya ni zao lenye uwezo mkubwa sana wa kupambana na maradhi hatari mwilini, na inalifanya zao hili kuwa muhimu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha mchanganyiko wa virutubisho vingi vya madini, vitamini, ‘flavoids’, ‘isoflavones’, ‘polyphenols’, ‘terpenes’, ‘saponins’, ‘phytosterols’ na ‘phytate’.
Faida zingine za Soya
Husaidia kuzuia mtu asipatwe na saratani zitokanazo na homoni za mwili, kama vile saratani ya matiti na tumbo. Vile vile Soya ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa mifupa na matatizo ya wanawake baada ya kufikia ukomo wa hedhi (menopause).

Vyakula na vinywaji vyote vitokanavyo na soya vimethibitika kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta mabaya na kolestrol, hivyo kuwa chakula ama kinywaji chenye faida tupu kwa mtumiaji.

Kwa kawaida Soya hutumika kama zao la kuzalisha mafuta ya kupikia ambayo huwa ni mazuri sana kiafya. Soya imejipatia umaarufu kiasi hicho, baada ya kugundulika kuwa na madini, vitamini na virutubisho vingine vinavyopatikana kwenye samaki, nyama, mayai na maziwa. Kwa maana nyingine, mtu anayekula Soya ni sawa na yule aliyekula vyakula hivyo.

Virutubisho vya Soya aina ya protini na ‘isoflavones’ hushusha kiwango cha Kolestrol mbaya (LDL) mwilini, halikadhalika hupunguza ugandaji wa damu hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya mtu kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi. Vile vile Soya huboresha msukumo na mishipa ya damu mwilini.

Kumbuka kuwa, protini mwilini huongeza uwezo wa mwili kuhifadhi na kunyonya madini ya ‘calcium’ kwenye mifupa. Ni mlo safi kwa wagonjwa wa kisukari na wenye matatizo ya figo. Kamba lishe (fibre) iliyomo, hurekebisha kiwango cha sukari na uchujaji sumu wa figo.

Soya ni nzuri kwa watu wenye matatizo ya kuwa na macho mekundu, ukosefu wa choo na kusikia kiu kila wakati. Aidha tahadhari inatolewa kwa watu wenye matatizo ya kuharisha, tumbo kuuma, minyoo na kusikia kiuungulia, wasitumie Soya kwa wakati huo.

Kwa ujumla, Soya, iwe maharage au vinywaji vyake, ni muhimu kutumiwa mara kwa mara kwani ina faida nyingi katika kupambana na maradhi na kuimarisha afya zetu.