KILA siku
tunazungumzia masuala ya kuweka ngozi safi na sura bomba lakini mara zote huwa
tunasahau kuzungumzia uzito ambao ama hakika ni kitu kibaya kuliko kitu
chochote kile. Uzito ni sawa na uvutaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa
kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho. wataalamu wa afya na urembo wanasema
wazi kuwa kuwa mnene kunapunguza siku namna ya kujiweka sawa katika masuala
mbalimbali ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani.
Wataalamu wanasema kwamba kuwa mzito kunapunguza maisha yako kwa miaka mitatu
na haya yamesemwa na mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit
ya chuo kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza. Uzito huu ni ule unaokuwa
mara tatu ya uzito ambao unatakiwa mtu awe nao kutokana na urefu wake,umri na
pia afya yake. Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150, mtu
huyu anapunguza umir wake wa kuishi hapa duniani kwa miaka 10. Kwa maelezo
mengine uzito wa aina hii ni sawa na uvutaji wa sigareti ambapo pamoja na
kuchakaza ngozi pia hupunguza maisha ya mtu kwa miaka kumi. Ndio kusema katika
urembo pamoja na kupiga vita sigareti uzito wa kuchusha nao lazima upigwe vita.
Kwa waafrika kuwa mnene ni bomba, pamoja na ukweli wa kiutamadunikwamba kuwa
mnene ni kutamu kwani unakuwa na nyama za kushikwa lakini ni vyema watu
wakatambua kwamba uzito wa kuchusha yaani mara tatu ya ule unaostahili kuwa nao
ni hatari kubwa kwa maisha yako. Onyo hili la wataalamu limefanywa baada ya
uchunguzi kwa watu 894,576 waume kwa wake katika tafiti 57 zilizofanywa. ingawa
tafiti hizi zilifanywa kwa watu wa Kaskazini mwa Marekani na Ulaya kwa watu
wenye ujazo wa 25 (BMI) hata hapa nchini watu wanastahili kuangalia suala la
uzito wao. Kwa taarifa yako uzito wa kuchusha huleta tatizo la figo, ini na
aina kadha za kansa na pia hyuleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi.
Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na pia kuleta mizania dhaifu ya rehemu na
kusababisha shida katika mwenendo wa damu. Wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza
hatihati ya kifo wakatiw nawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hati hati ya
kifo kwa asiulimia 78.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni