Jumapili, 29 Septemba 2013

FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI KIAFYA.

Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, nitakueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.
1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.

2. Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya  oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis
 
3.Hupunguza msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.
aa-couple-in-bedroom4. Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).




5. H
upunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: 
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.
6. H
uongeza uwezo wa kunusa: 
Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa  na kutambua harufu (brain olfactory bulb).
7. H
upunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: 
Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.
8. H
uongeza kinga ya mwili: 
Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
black-women-beauty-central








9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke
Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa. 

10. Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida
Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.
11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.
12. Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): 
Na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na  maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ).
13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa 
damu mwilini
 Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.
14. H
uongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.
15. H
usaidia kuishi kwa muda mrefu
Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele.  DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.
16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.

17. Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: 
Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne.  

Jumamosi, 28 Septemba 2013

UGONJWA WA GAUTI NA MADHARA YAKE MWILINI MWAKO.



Kwa baadhi ya wanaume wanaugua ugonjwa huo kuliko wanawake
Ukitembea katika jamii hasa mijini utawasikia watu wengi hasa wanaume wanapokunywa bia na kula supu wakizungumzia ugonjwa huu wanaoutaja kama gauti. Unaweza kujiuliza, huu ni ugonjwa gani?
 Huu ni ugonjwa unaoathiri viungo  vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali aina ya uriki (uric acid) katika damu.
Ongezeko hilo la uriki husababisha madhara katika viungo vya mifupa, viungo ni sehemu ya mwili inapokutana, inapoungana mifupa miwili. Kwa kawaida, gauti inaweza kutokea ghafla au ikawa sugu.
Kwa ile inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri kiungo kimoja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri kiungo zaidi ya kimoja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye viungo.
Visababishi vyake
Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya uriki katika damu. Hali hii hutokea iwapo mwili  wa mgonjwa unatengeneza uriki nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa  tindikal ya uriki mwilini kama inavyotakiwa.
Ongezeko hili husababisha mrundikano wa tindikali ya uriki katika majimaji yanayozunguka viungo yanayoitwa synovial na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogovidogo vya tindikali ya uriki ambavyo husababisha viungo kuvimba na hatimaye kuathirika.
Vihatarishi
Ingawa chanzo halisi hakieleweki vyema, ugonjwa hutokea kuwapata baadhi ya watu walio wa familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi.
Aidha, unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa kama vile za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uriki katika damu.
Vihatarishi vingine ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliokithiri, upungufu wa damu unasababishwa na seli mundu  (sickle cell) au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).Pia, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa tindikali ya uriki mwilini.
Dalili za ugonjwa huo
- Dalili kwa kawaida huhusisha kiungo kimoja au vichache. Viungo vinavyoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa cha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
-Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla, hususan nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
-Viunganio katika mwili hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionyesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye kiungo chenye matatizo.
-Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, pia laweza kujirudia mara kwa mara.
-Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa. Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika viungo (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia viungo vyake.
Wagonjwa wa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka viungo vilivyoathirika. Vinundu hivi ni ishara ya muhimu kwa madaktari.
Ushauri:
-Tuache pombe
-Tupunguze ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya uyoga, spinachi. Dhibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo.

Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa. Kula kiasi kikubwa cha wanga. Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo.

Ijumaa, 27 Septemba 2013

Vyakula vya kuepukwa na wajawazito


Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.

Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

NYAMA MBICHI

Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.

‘SOSEJI’ NA ‘SANDWICHI’

Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

SAMAKI WENYE ZEBAKI (MERCURY)
Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira. Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa.

MAYAI MABICHI
Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ‘Ice Cream’ na ‘mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.

MAINI
Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha Vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.

MAZIWA MABICHI
Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama ‘Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa‘Pasteurized’ na siyo ‘Unpasteurized’.

KAFEINI (CAFFEINE)

Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba. Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa.

Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku. Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.

Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto ‘njiti’ na watoto wenye uzito mdogo. Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

POMBE
Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara, kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujauzito, hata kama ni kidogo.
Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).


Alhamisi, 26 Septemba 2013

Coca Cola huwafanya wanaume tasa!

Kinywaji cha coca cola kimeendelea kuwa maarufu duniani lakini utafiti mpya umeonyesha kuwepo uhusiano wa kunywa sana kinywaji hicho na matatizo ya uzazi kwa wanaume.

Kwa mjimu wa utafiti huo uliochapichwa kwenye Jarida la Epidemiology la Marekani, wanaume wanaokunywa zaidi ya lita moja ya coca cola kwa siku wanakabiliwa na hatari ya kuwa tasa. Wanaume waliotumia kinywaji hicho walikuwa na upungufu wa aslimia 30 ya mbegu za uzazi zilizohesabiwa, ikilinganishwa na wale ambao hawakutumia. Wanaume hao walionekana kuwa na matatizo ya uzazi zaidi kuliko wasiokunywa coca cola.

MADHARA SABA KWA WANAUME WAOPENDA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE



Leo tunageuza shilingi upande wa pili kuelezea madhara ya kuruka ukuta (kufanya ngono kinyume cha maumbile), baada ya kuona madhara ya wanawake kurukwa  na nini kifanyike. 
Wanaume wengi walinilaumu na kuniona sitendi haki kwa kuwaelezea wanawake tu wakati mchezo huwa una athari kwa mtenda na mtendewa.

Kama nilivyoelezea kwenye mada za wiki kadhaa zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’.
 
Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu.

Tulipoangalia upande wa wanawake, tuliona sehemu kubwa ya wanaopenda mchezo huu ni wanaume ambao wengine wamebatizwa majina ya ‘basha’, wakimaanisha mwanaume mpenda kuruka ukuta bila kuangalia ni wa mwanaume mwenzake au wa mwanamke.

Kwa vile nia ya kona hii ni kuelimisha madhara ya mtu kupenda kuruka ukuta ili aache mara moja, tunaendelea kutoa elimu ya bure ili mtu yakimkuta ajue yamempata kwa kiburi chake na kwa kupenda starehe ya kipuuzi.

Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo ni kama ifuatavyo:
 
Kwanza:
 Husababisha kusinyaa au kuweka makovu kwenye njia ya haja ndogo.

Pili: 
Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa.

Tatu: 
Kupata saratani (kansa) ya tezi za figo (prostate gland).

Nne: 
Kupata magonjwa sugu ya uti wa mgongo.

Tano: 
Kuharisha.

Sita: 
Maambukizi ya VVU ambapo mwisho wake ni Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Saba: 
Baadaye mhusika kupata msongo wa mawazo au sonona kwa kujutia tendo hilo.

Nina imani ndugu yangu umeona madhara mabaya sana ya tabia hiyo mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako na kuona raha lakini tumeona madhara yake, ambayo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.

Jiepushe kuiga mambo bila kujua faida na hasara zake pia usimtie mwenzako majaribuni kwa kumlazimisha kuingia kwenye mchezo huo. Wanawake wengi wamekuwa wakilazimishwa na wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa. 

Swali linakuja, kipi bora, kuharibiwa au kuachana?
Kumbuka baada ya kuharibikiwa, thamani yako hushuka na sifa yako ikiwafikia waharibifu wa watu, basi unageuzwa jamvi la mtaa na hatimaye unakufa kwa msongo wa mawazo au mateso ya ugonjwa utakaupata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.

Unaweza kushangaa baada ya kuelezea madhara yanayowapata wanaume nimehamia kwa wanawake. Ukweli mchezo huu umewaathiri sana wanawake ambao wengi wanaujutia.

12 Health Risks of Chronic Drinking

"Alcohol does all kinds of things in the body, and we're not fully aware of all its effects," says James C. Garbutt, MD, professor of psychiatry at the University of North Carolina at Chapel Hill School of Medicine and a researcher at the university's Bowles Center for Alcohol Studies. "It's a pretty complicated little molecule."It's no secret that alcohol consumption can cause major health problems, including cirrhosis of the liver and injuries sustained in automobile accidents. But if you think liver disease and car crashes are the only health risks posed by drinking, think again: Researchers have linked alcohol consumption to more than 60 diseases. 
Here are 12 conditions linked to chronic heavy drinking.

Heavy drinking can cause the number of oxygen-carrying red blood cells to be abnormally low. This condition, known as anemia, can trigger a host of symptoms, including fatigue, shortness of breath, and lightheadedness.

Cancer

"Habitual drinking increases the risk of cancer," says Jurgen Rehm, PhD, chairman of the University of Toronto's department of addiction policy and a senior scientist at the Centre for Addiction and Mental Health, also in Toronto. Scientists believe the increased risk comes when the body converts alcohol into acetaldehyde, a potent carcinogen. Cancer sites linked to alcohol use include the mouth, pharynx (throat), larynx (voice box), esophagus, liver, breast, and colorectal region. Cancer risk rises even higher in heavy drinkers who also use tobacco.

                  Cardiovascular Disease

Heavy drinking, especially bingeing, makes platelets more likely to clump together into blood clots, which can lead to heart attack or stroke. In a landmark study published in 2005, Harvard researchers found that binge drinking doubled the risk of death among people who initially survived a heart attack.
Heavy drinking can also cause cardiomyopathy, a potentially deadly condition in which the heart muscle weakens and eventually fails, as well as heart rhythm abnormalities such as atrial and ventricular fibrillation. Atrial fibrillation, in which the heart's upper chambers (atria) twitch chaotically rather than constrict rhythmically, can cause blood clots that can trigger a stroke. Ventricular fibrillation causes chaotic twitching in the heart's main pumping chambers (ventricles). It causes rapid loss of consciousness and, in the absence of immediate treatment, sudden death.

Cirrhosis

Alcohol is toxic to liver cells, and many heavy drinkers develop cirrhosis, a sometimes-lethal condition in which the liver is so heavily scarred that it is unable to function. But it's hard to predict which drinkers will develop cirrhosis. "Some people who drink huge amounts never get cirrhosis, and some who don't drink very much do get it," Saitz says. For some unknown reason, women seem to be especially vulnerable.

Dementia

As people age, their brains shrink, on average, at a rate of about 1.9% per decade. That's considered normal. But heavy drinking speeds the shrinkage of certain key regions in the brain, resulting in memory loss and other symptoms of dementia. 
Heavy drinking can also lead to subtle but potentially debilitating deficits in the ability to plan, make judgments, solve problems, and perform other aspects of "executive function," which are "the higher-order abilities that allow us to maximize our function as human beings," Garbutt says.
In addition to the "nonspecific" dementia that stems from brain atrophy, heavy drinking can cause nutritional deficiencies so severe that they trigger other forms of dementia.

Depression

It's long been known that heavy drinking often goes hand in hand with depression, but there has been debate about which came first -- the drinking or the depression. One theory is that depressed people turned to alcohol in an attempt to "self-medicate" to ease their emotional pain. But a large study from New Zealand showed that it was probably the other way around -- that is, heavy drinking led to depression.
Research has also shown that depression improves when heavy drinkers go on the wagon, Saitz says.

                               Seizures

Heavy drinking can cause epilepsy and can trigger seizures even in people who don't have epilepsy. It can also interfere with the action of the medications used to treat convulsions.

Gout

A painful condition, gout is caused by the formation of uric acid crystals in the joints. Although some cases are largely hereditary, alcohol and other dietary factors seem to play a role. Alcohol also seems to aggravate existing cases of gout.

High blood pressure

Alcohol can disrupt the sympathetic nervous system, which, among other things, controls the constriction and dilation of blood vessels in response to stress, temperature, exertion, etc. Heavy drinking -- and bingeing, in particular -- can cause blood pressure to rise. Over time, this effect can become chronic. High blood pressure can lead to many other health problems, including kidney disease, heart disease, and stroke.

Infectious disease

Heavy drinking suppresses the immune system, providing a toehold for infections, including tuberculosis, pneumonia, HIV/AIDS, and other sexually transmitted diseases (including some that cause infertility). People who drink heavily also are more likely to engage in risky sex. "Heavy drinking is associated with a three-fold increase in the risk of contracting a sexually transmitted disease," Rehmn says.

Nerve damage

Heavy drinking can cause a form of nerve damage known as alcoholic neuropathy, which can produce a painful pins-and-needles feeling or numbness in the extremities as well as muscle weakness, incontinence, constipation, erectile dysfunction, and other problems. Alcoholic neuropathy may arise because alcohol is toxic to nerve cells, or because nutritional deficiencies attributable to heavy drinking compromise nerve function.

Pancreatitis


In addition to causing stomach irritation (gastritis), drinking can inflame the pancreas. Chronic pancreatitis interferes with the digestive process, causing severe abdominal pain and persistent diarrhea --and "it's not fixable," Saitz says. Some cases of chronic pancreatitis are triggered by gallstones, but up to 60% stem from alcohol consumption.

Jumatano, 25 Septemba 2013

Ni alama gani za mwili wako zitakufahamisha Ovulation imewadia?




Wadau wa Kona ya Afya, niliahidi kuendeleza mada yetu ya namna ya kuzijua siku za kushika mimba kwa kuzungumzia baadhi ya alama za mwili zinazosaidia kutambua ni wakati gani Ovulation imewadia. Alama hizo za Ovulation si ngumu kuzitambua, iwapo utafahamu unatafuta alama gani. Kuna baadhi ya alama za mwili zinazokutahadharisha kwamba Ovulation iko njiani, hivyo kuweza kukusaidia kupanga vyema muda wa kujamiiana kwa ajili ya kupata mamba. Alama nyinginezo zinakufahamisha kwamba Ovulation imewadia au imeshapita. Ingawa alama hizo ziko nyingi na nitazungumzia baadhi ya hizo, lakini usifikiri kwamba unatakiwa utumie zote, kwani kufanya hivyo kunaweza kukuchanganya.
Iwapo hutoona alama zozote za Ovulation au iwapo siku zako za mwezi hazina mpangilio maalum, ni bora umuone daktari ambaye atakusaidia zaidi.
Mabadiliko ya joto lako la Mwili
Tunaweza kusema kuwa Joto lako la mwili au (Body Basal Temperature) ndio alama maarufu inayotumiwa na wanawake wengi ili kufahamisha kwamba Ovulation imewadia pale wanapotaka kubeba mimba. Hii ni kwa sababu joto lako la mwili huongezeka kwa kiasi kidogo na huendelea kuongezeka baada ya Ovulation. Ongezeko hilo la joto husababishwa na homoni ya progesterone, ambayo huongezeka sana punde baada ya Ovulation. Kwa kujipima joto lako la mwili na kuandika chati ya mabadiliko hayo unaweza kufahamu ongezeko hilo la joto lako la mwili. Unahitajia kipimamoto kwa ajili ya kufanikisha suala hilo. Zipo pimajoto maalum kwa ajili hiyo lakini unaweza kutumia pimajoto ya kawaida pia. Hakikisha unapima joto la mwili wako asubuhi baada ya kuamka na uhakikishe huna homa, hukukosa usingizi, hukunywa pombe, si mgonjwa wala huna wasiwasi na fikra nyingi. Ni bora ufanye hivyo kwa mizunguko kadhaa ya siku zako ili uweze kuijua vyema chati ya mabadiliko ya joto la mwili kwa mujibu wa mzunguko wako wa mwezi.



Ingawa njia hii haianishi moja kwa moja kuwa Ovulation imewadia, lakini joto la mwili huongezeka kidogo kabla yakipindi hicho na huongezeka kwa kwa degree 0.4 hadi 0.6 baada tu ya kumalizika Ovulation. Kuongezeka joto kwa kiasi kikubwa baada ya Ovulation huendelea hadi siku utakayopata siku zako ambapo hupungua na mzunguko wako wa mwezi huanza tena. Iwapo utakuwa umepata mimba joto lako la mwili litaendelea hivyo hivyo kuwa juu. Kwa kuwa mabadiliko ya joto hutokea wakati wa Ovulation iwapo unajaribu kubeba mimba, kufuatilia mabadiliko hayo kwa muda usiopungua miezi miwili ni jambo la dharura ili uweze kujua wakati wa Ovulation ambapo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba.
Mabadiliko ya majimaji ya ukeni
Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya ukeni hubadilika pia kwa kiasi na hali. Ikiwa hakuna Ovulation majimaji ya ukeni huwa yanayonata au kama kremu au hukosekana kabisa. Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya ukeni huongezeka na huwa katika hali ya majimaji na wakati mwingine huwa rangi nyeupe kama ya yai bichi. Iwapo utapima kwa vidole vyako huvutika kwa inchi au zaidi kati ya vidole vyako.
Ni bora nikumbushe hapa kwamba, kuan wakati unaweza kuwa na majimaji ya ukeni yanayofanana na ya wakati wa Ovulation hali ya kuwa huko katika Ovulation. Hali hiyo ni ya kawaida kwa watu wenye PCOS. Kutumia dawa za Clomid au Antihistamin huweza kufanya majimaji ya ukeni yakauke na hivyo kuwa vigumu kutumia njia hii ili kujua ni zipi siku zennye uwezekano mkubwa wa mimba. Njia hii huhesabiwa kuwa yenye itibari zaidi.
Ongezeko la Matamanio 
Inaonekana kuwa maumbile nayo hutusaidia kujua ni siku gani tunaweza kubeba mimba! Wataalamu wameonyesha (jambo ambalo pengine wengi wameshalihisi) kwamba wanawake wanapokuwa katika siku zenye uwezekano mkubwa wa kupata mimba, matamanio yao ya huongezeka. Hizo ni siku chache kabla ya kujiri Ovulation, ambapo ndio wakati unaofaa wa kujamiiana iwapo unataka kubeba mimba.
Hata hivyo njia hii si ya kutumainiwa sana kwani baadhi ya hali kama vile msongamano wa mawazo, fikra nyingi na wasiwasi huweza kupunguzaa matamanio. Au mtu anaweza akahisi matamanio katika muda wote wa mzunguko wa mwezi.
Mabadiliko ya Ukeni:
Kama ambavyo majimaji ya ukeni yanavyobadilika wakati wa Ovulation, uke nao (cervix) hubadilika wakati wa kukaribia Ovulation. Wakati huo uke husogea mbele, huwa laini na hufunguka zaidi.
Maumivu kidogo katika Matiti:
Baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia Ovulation au baada ya hapo matiti yao huwa na maumivu kidogo. Suala hili huhusiana na mabadiliko ya homini mwili ambazo hujitayarisha kwa ajili ya mimba. Hata hivyo njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani maumivu ya matiti huweza kusababishwa na masuala mengine. Pia maumivu ya matiti hutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumia baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.




Alama nyinginezo
Baadhi ya wanawake huhisi maumivu kidogo ya tumbo ambayo baadhi huyaita Middle Pain. Maumivu hayo kwa kawaida hutokea upande ule yai linapotoka yaani upande wa Ovulation. Maumivu hayo hutokana na mwendo wa yai wakati linapopenya kwenye mirija. Maumivu hayo si ya kuendelea na wala si makubwa na huisha haraka. Hali hiyo huweza kutokea mara kadhaa katika siku za Ovulation. Kuna baadhi ya alama kama vile baadhi ya wanawake huhisi kichefuchefu, gesi, kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kujamiina, hali ambayo haitokei kwa watu wengi. Pia kuna baadhi ya vifaa vinavyopaatikana katika madula ya dawa katika baadhi ya nchi ambavyo huweza kukusaidia kujua wakati wako wa Ovuation umewajia, vifaa hivyo hujulikana kama 'Ovulation Kit"
La muhimu ni kufahamu kuwa wanawake hutofautiana katika kupata alama hizi, kwani kuna baadhi wanaweza wakapata baadhi ya alama hizi na wengineo wakapata nyinginezo. Kuuelewa vyema mwili wako ni jambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijua siku zako la Ovulation na hivyo kuweza kujua siku zako za kubeba mimba.