Kinywaji cha coca cola kimeendelea kuwa maarufu duniani lakini utafiti mpya umeonyesha kuwepo uhusiano wa kunywa sana kinywaji hicho na matatizo ya uzazi kwa wanaume.
Kwa mjimu wa utafiti huo uliochapichwa kwenye Jarida la Epidemiology la
Marekani, wanaume wanaokunywa zaidi ya lita moja ya coca cola kwa siku
wanakabiliwa na hatari ya kuwa tasa. Wanaume waliotumia kinywaji hicho walikuwa
na upungufu wa aslimia 30 ya mbegu za uzazi zilizohesabiwa, ikilinganishwa na
wale ambao hawakutumia. Wanaume hao walionekana kuwa na matatizo ya uzazi zaidi
kuliko wasiokunywa coca cola.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni