Jumatatu, 28 Julai 2014

FAHAMU AINA ZA KIHARUSI (STROKE)




Kiharusi au kwa Kiingereza Stroke ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida.Kuna aina mbili za kiharusi, lakini kabla ya kuchambua hayo tuangalie, ni nini kinasababisha mtu kukumbwa na ugonjwa huu? 


Mtu anaweza kupata dalili za ugonjwa huu wa kiharusi na baada ya dakika chake zikaisha.
Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo unapopasuka. 

Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea, kwanza ni: 

1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalamu huitwa Ischemic stroke. (Ischemic ni neno la Kigiriki lenye maana ya kuzuia damu).
Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri. 

Hiki hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu, hali ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo. 

Hali hiyo pia hufanya damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo kitaalamu huitwa Cerebral thrombosis au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo kitaalamu huitwa Cerebral embolism. 

Lakini tatizo hili linaweza kutokea pale damu inapoganda sehemu nyingine ya mwili na kusafiri hadi kwenye mishipa ya ateri, hivyo kusababisha damu kwenda kwenye ubongo kukwama.
Hata hivyo, tatizo hili linaweza kusababisha kitu kinachoitwa Lacunar stroke, yaani vimirija vidogovidogo sana vya damu vilivyopo ndani ya ubongo, vinaziba. 

Hapo sasa binadamu huwa anakumbwa na kiharusi kinachojulikana kitaalamu Lacunar stroke japokuwa mara nyingi hii haiwaletei sana shida wagonjwa. 

KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE
Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar stroke, sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.
Aina hii ya kiharusi, mrija wa damu karibu ama kwenye ubongo hupata mpasuko, hivyo kusababisha damu kuvuja na kitendo hicho ndicho kitaalamu huitwa Haemorrhage. 

Kinachotokea ni kwamba damu inayovuja hukandamiza ubongo na kuuharibu, ubongo ni moja ya kiungo laini sana mwilini. 

Katika hali ya kitaalamu inayoitwa Intra cerebral haemorrhage, uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo wenyewe. Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa. 

Lakini kuna hali pia inayoitwa Subarachnoid haemorrhage ambapo mpasuko wa mshipa wa damu hufanyika karibu na eneo linalozunguka ubongo linaloitwa Subarachnoid. 

Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwilini, hali inayoitwa kitaalamu kama Atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis) hiyo.

BAADHI YA SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO

Moja ya matatizo yaliyoko katika jamii zetu na yamesababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, ni kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke. 

Sote tunafahamu kuwa, swala la mwanamke kupata ujauzito linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:


Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko (Menstrual cycle) katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni kuzalishwa katika wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito, pia tatizo la kuwa na uzito wa mwili mdogo sana au mkubwa sana pia huathiri hali nzima ya homoni na kupelekea kushindwa kupata ujauzito.

Umri, kwa wanawake uwezo wa kupata ujauzito unapungua kwa kadri umri unavyoongezeka, hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika wakati umri unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi.

Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), hii husababisha mbegu za kiume (sperms) zishindwe kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utokee. Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, matatizo katika kizazi au upasuaji. Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.

Ute ute katika kizazi (mucus problems), ute unaopatikana katika kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha. Kwa baadhi ya wanawake ute huu unakuwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kuweza kupita, na wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume, haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo ujauzito kutopatikana.

Uvimbe katika kizazi (fibroids), hii huchangia asilimia tatu (3%) katika mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, kwa namna moja au nyingine huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.

Matibabu ya kansa, kwa kutegemeana na aina ya matibabu, aina ya dawa au njia ya mionzi, hizi huweza kumuathiri mwanamke na kumsababishia kushindwa kupata ujauzito.

Ukomavu katika kizazi, kwa baadhi ya wanawake wanayo matatizo ambayo kizazi chao huwa hakijakomaa vizuri au katika kuzaliwa kwao walizaliwa na tatizo hili ambalo, kizazi hakiko sawa (abnormally developed uterus).

Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito yanayo tiba, kama unalo tatizo katika kupata ujauzito usikate tamaa, onana na wataalamu wa afya ili uweze kujua chanzo cha tatizo lako na kupatiwa msaada unaostahili.

Jumapili, 27 Julai 2014

NEW-LIFE AFYA CLINIC INAPENDA KUKUPA DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI SIKU YA LEO.



Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma. 

Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba. 

Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu, tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina. 

Saratani ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu,… 


Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma. 

Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba. 

Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu, tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina. 

Saratani ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu, anaachana naye anaishi na mwingine, yaani mara kwa mara hana msimamo, anabadilibadili wanaume, wanawake wanaofanya ngono na wanaume wasiofanyiwa tohara pia hupatwa na tatizo hili la saratani ya shingo ya uzazi. 

Saratani ya shingo ya uzazi pamoja na kuchangiwa na mambo yote hayo hapo juu, husababishwa hasa na kirusi kiitwacho ‘Human Papilloma virus’ au kwa kifupi ‘HPV’. Kirusi hiki huenezwa kwa njia ya ngono, mwanaume huwa hakimuathiri bali yeye hukibeba na kukisambaza kwa wanawake kwa hiyo mwanamke anayechanganya wanaume hajui wapi atakipata.

Ukubwa wa tatizo
Saratani ya shingo ya kizazi ina tabia ya kusambaa endapo haitagundulika na tiba haitafanyika mapema. Saratani husambaa katika kizazi, nyonga hadi katika mapafu. Ikishambulia nyonga, mwanamke hulalamika maumivu chini ya tumbo.

Saratani hii ina tabia ya kusambaa kwa kasi na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa husababisha kifo kwa mwanamke. Saratani huwa haiambukizi.

Dalili za awali za saratani ya shingo ya uzazi
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni na muwasho mara kwa mara. Tatizo hili hutibiwa na kujirudia tena mara kwa mara. 

Mwanamke hulalamika kwamba ametibiwa sana kwa dawa za kumeza na kuingia ukeni lakini hapati nafuu. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwishowe hutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa. 

Saratani inaposambaa na kushambulia shingo ya uzazi huathiri ukeni na kuumiza njia ya mkojo na kibofu.
Uke huvimba na kuonekana kuziba na mlango wa kizazi au ngozi ya ndani ya ukeni ikiguswa tu kidogo basi hutokwa na damu kwani huwa laini sana. Hii ni hatua mbaya na ya mwisho katika saratani inaposambaa.

Uchunguzi

Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi hufanyika katika vituo mbalimbali katika kampeni maalum dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi. 

Uchunguzi pia hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya katika kliniki za magonjwa ya kinamama ambapo vipimo mbalimbali hufanyika mojawapo ikiwa ni kuangalia mlango na shingo ya uzazi. 

Kipimo cha Ultrasound pia kitafanyika kuangalia athari katika kizazi. Majimaji ya ukeni yatapimwa kuangalia maambukizi na uchunguzi wa awali wa saratani utafanyika.
Endapo mlango wa uzazi utakuwa umeathirika sana, basi kinyama kitatolewa na kupimwa katika maabara kubwa kuthibitisha tatizo.

WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU +255713354389 KWA USHAURI NA SULUHISHO ZAIDI.

NEW-LIFE AFYA CLINIC INAKUPA ELIMU YA KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI (GALACTORRHEA)

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu. 

Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume. 

Chanzo cha tatizo
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini. 

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’. 
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.
Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone. 

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili. 

Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji. 

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo. 
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili. 

Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo. 

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu. 

Uchunguzi
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary. 

Ushauri
Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa. 
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.

WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU WHATSAPP +255713354389 KWA MAELEZO NA SULUHISHO JUU YA TATIZO HILI. WAHI MAPEMA KABLA UGONJWA HAUJAWA SUGU.

Jumatatu, 7 Julai 2014

JE UNAJUA MADHARA YA KUWA NA KITAMBI ?. BASI FAHAMU NA MBINU ZAKE ZA KUKIONDOA.


 
Operesheni ondosha vitambi kwa kina mama.
AKINAMAMA wengi siku izi ukikutana nao wanaonekana kama ni wajawazito, lakini si wajawazito, wana vitambi ama viriba tumbo kama wanaume, hii si hali ya kawaida, wengi wao hawajui kwanini wanakuwa na viriba tumbo hivyo na mbaya zaidi hawajui wafanyenini kuondokana na vitam

bi hivyo. Vitambi hivyo vina athari nyingi sana, za kiafya na kimaumbile.
Kiafya.


Kuendelea kuruhusu vitambi hivyo kukua pasipo kuchukua hatua sitahiki upelekea kupata matatizo mengi ya kiafya yakiwemo:-

· Mgandamano wa taka na sumu tumboni au Corprostasis
· Kukosa choo au Constipation.
· Kiharusi au Stroke
· Uzito uliozidi au Obesity.
· Matatizo ya moyo. Cardiovascular diseases
· Shinikizo la juu la damu au High blood pleasure
· Kisukari au Diabetes
· Saratani. Au cancer
· Kukakamaa kwa mishipa au arterioscelosis. Nk.


Haya ni baadhi tu ya magonjwa yanayoweza kumshambulia mtu iwapo hatachukua hatua kuakikisha anakuwa na mwili wenye afya kuwa kutorusu viriba tumbo. Hii ni kwa wanawake na wanaume pia, japo wengi wa wanaume wana fikra potofu kuwa kitambi ni afya au mafanikio Fulani, hiyo si kweli, bali ni matatizo.

Kimuonekano. 
Mwanamke anapokuwa na kitambi uwa anapoteza muonekano, avaapo nguo hapendezi kwa sababu tumbo ndio linatangulia, hii ni tofauti sana na tumbo la ujauzito, kwani lile uwa na kwa muda tu na uwa lina mavazi yake maalumu pia ambayo uwafanya baadhi yao kuonekana wanapendeza wanapokuwa atika hali hiyo.

Kiriba tumbo upoteza kabisa shape ama figure ya mtoto wa kike, matokeo yake ni kuwa hakuna nguo atakayovaa ikampendeza, hii imepelekea kinamama wengi kulazimika kuvaa madela tu kama wajawazito kwa kuwa hakuna nguo inayompendeza.


KAMPENI ONDOSHA KITAMBI.
Kampeni hii imekuja maalumu kwa ajili yako wewe mama ambaye unalazimika kuvaa madela muda wote kama mjamzito wakati huna mimba, weye ambaye upendi kuwa na kitambi na tena wakichukia lakini hujui ufanye nini, weye ambaye watamani kuwa na figure ipendezayo ambayo yavutia wengi.

Unahitaji kufata hatua nne muhimu za program hii ambazo ni rahisi sana kufikia kuwa na mwili au figure uipendayo na mwenye afya pia, kwani kwa kufata hatua hizo nne, utaondoa kiriba tumbo na kujikinga na maradhi yoote yaliyotajwa hapo juu na mengine mengi. Programu hii ya kuondosha kitambi ukiifuata sawasawa inakupa majibu ndani ya mwezi mmoja, ni salama na hakika.

Hatua hizo ni:
1. Kuondoa sumu mwilini.
Hii ni hatua muhimu sana kuelekea kwenye safari yako ya kuondosha kitambi. Ina safisha mfumo mzima wa mmengenyo wa chakula na kuondoa mgandamano wa taka tumboni. Kwa mfumo wetu wa chakula unapokuwa umefunga miili yetu hushindwa kufyonza virutubisho muhimu na kufanya sumu na taka kurundikana mwilini.


2. Kuchoma mafuta na kungarisha mwili.
Hii ni muhimu kwani ingawa miili yetu yahitaji mafuta kwa kutunza joto, mafuta hayo yanapozidi ni hatari na upelekea kuhatarisha mahisha, utagundua kuwa mafuta yachomwapo metabolism ya mwili nayo inaongezeka. 


3. Kusawazisha na kusafisha.
Hii usawazisha kiwango cha asidi na alkali miilini mwetu itokanayo na kula vyakula vyenye asidi nyingi na kupelekea kutokuwa na mlo kamili, pia yasafisha mfumo mzima wa damu na kongeza kiwango cha usambazi wa hewa ya oksijeni mwilini na zaidi ya yote kuuongezea mwili kinga ya kupambana na maradhi yoote.
4. Kurejesha – rejuvenation
Program hii yamalizia na kurejeza, kuuisha upya chembe hai za damu kwa kuupa mwili viondoa sumu,(anti oxidants) hii inafaida kubwa sana kwa mfumo wa damu na moyo pia, huongeza protein muhimu na hivyo kukufanya usizeeke upesi. (Anti aging properties).


"MAJIBU NDANI YAMWEZI MMOJA"Je wataka kuondosha kiriba tumbo?? call now +255-713-354-389 au +255-762-285-404

Jumapili, 22 Juni 2014

11 Lifestyle Diseases You Should Take Seriously



  1. Communicable diseases like malaria, cholera and polio have become manageable due to recent advancements in medicines. However a new breed of diseases has developed, called ‘Lifestyle diseases’ such as heart disease, some cancers and diabetes, which are no longer a problem just in wealthy nations. Globally 14.2 million people between the ages of 30-69 years die prematurely each year from these diseases. These diseases have emerged as bigger killers than infectious or heridetary ones. Risk factors for these diseases include tobacco use, unhealthy diets and physical inactivity. Today we will take look at the most common lifestyle diseases that you need to take seriously

  2. Default

     
    1. Obesity 


    Unhealthy eating habits, super-sizing meals, and reduced physical exercise all translate to obesity. A person with excessive weight suffers with breathing problems, blood pressure, cardiovascular diseases, diabetes, etc.

    The NFHS figures suggest that currently India ranks second with 155 million obese citizens and are increasing at 33-51% every year
    Reply With Quote
  3.  
    2. Type II diabetes 


    Obesity becomes the cause for other health problems such as Type II Diabetes which is the non-insulin dependent form, and generally develops in adults.

    The International Diabetes Federation suggests that India has the largest number of people who suffer with type 2 diabetes at around 40.9 million people

  4.  

    3. Arteriosclerosis


    This is a group of diseases that occur when the arterial blood vessel walls thicken and lose elasticity.

    Atherosclerosis is when fatty plaques deposit in the arterial walls and cause blood circulation disorders, chest pain, and heart attacks. It is linked with diabetes, obesity and a high BP.

    Around 30% to 40% of cardiovascular deaths happen in India among the age group of 34-64 years of age
    Reply With Quote

  5. Default

     
    4. Heart disease


    This refers to abnormalities that affect the heart muscle and blood vessel walls. The major factors involved in its development are smoking, diabetes and high cholesterol intake.

    India ranks No.1 in cardiac patients, around 50 million people in India suffer from heart problems
    Reply With Quote
  6.  
    5. High blood pressure


    When the reading is 140/90 or higher, the BP is considered to be high. Hypertension results from a variety of reasons like stress, obesity, genetic factors, overuse of salt in the diet and ageing.

    In India, more than 100 million people have high blood pressure
  7.  

    6. Swimmer's ear


    Swimmer's ear is inflammation, irritation, or infection of the outer ear and ear canal. Buzzing or ringing ears, or difficulty in understanding speech patterns are its symptoms.

    Swimmer’s ears results due to loud music and constant use of headphones.

    An estimated of 12.5% have suffered permanent damage to their hearing in India from excessive exposure to noise, and the number is growing each year.


    Reply With Quote

  8.  

    7. Cancer


    Cancer includes any hysterical, irregular cell growth. The types of cancer could include lung cancer due to prolonged smoking, skin cancer due to too much exposure to the sun etc.

    Cancer killed almost 5,56,400 people across the country in 2011
  9.  
    8. Stroke


    A stroke results when a blood vessel carrying blood to the brain has a blockage, thus creating an oxygen deficiency for the area of the brain it was carrying it to.

    Indian studies have shown that about 10% to 15% of strokes occur in people below the age of 40 years
    Reply With Quote

  10.  
    9. Chronic obstructive pulmonary disease


    This is a disease described by a progressive, permanent obstruction of the airways. Smoking and air pollution are factors as well as reasons for worsening of this condition.

    Percentage of adults diagnosed with COBD in the past year: 4.3 million


    Reply With Quote

  11.  
    10. Cirrhosis


    Cirrhosis refers to a group of liver disorders. Heavy alcohol consumption and chronic hepatitis may be listed as causes.

    In India, approximately 36,149 people die each year due to cirrhosis.
    Reply With Quote

  12.  
    11. Nephritis


    This includes kidney disease characterized by swelling of the kidneys and abnormal function.

    Around 39,480 deaths are estimated due to nephritis each year in India.

MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTIs)


Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia “naumwa U.T.I”. Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.
U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.
Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.
Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.
Visababishi
Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na ‘fungus’ na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.

Vihatarishi na Njia ya Maambukizi
a)Kwa wanawake
• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi

b)Kwa wanaume
• Matatizo ya tezi ya kiume(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
• Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi

c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi –kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji

Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo

b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika

Vipimo na matibabu
Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo

Madhala yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi
• Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
• Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni
• Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine
• Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo

Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa. Fanya yafuatayo
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu

Njia za Kujikinga na U.T.I
Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu

Kwa wanawake
Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini
Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi

Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
Kondom wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri


WASILIANA NASI KWA +255762285404 AU 0713354389 KWA USHAURI NA TIBA.