Jumatano, 30 Oktoba 2013

MAMBO YANAYOHARIBU AFYA YA BINADAMU





 
Mazingira ni jambo lingine linaloathiri afya. Iwapo maji tunayokunywa na kutumia ni safi na salama, iwapo hewa tunayovuta si chafu, maeneo tunayofanyia kazi ni salama na pia nyumba tunazoishi, basi afya zetu huwa salama zaidi ikilinganishwa na watu wanaoishi kwenye maeneo yasiyo na maji safi na salama au kuvuta hewa chafu na kufanya kazi kwenye mazingira ya hatari.


Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Zuyd nchini Uholanzi umeonesha kwamba, kuvuta hewa iliyochafuliwa kwa gesi za magari kwa lisaa limoja kunatosha kumpatia mtu mfadhaiko wa kifikra au stress katika ubongo wake.


Utafiti mwingine uliofanywa na chuo kikuu cha India cha Purdue umebainisha kuwa, sumu kali inayotokana na sumu ya risasi, inayoweza kuiingia mwilini mwa binadamu kutokana na kula vitu vilivyoingiwa na sumu hiyo, nchini Marekani huathiri maelfu ya watoto kuliko kiwango dhaifu cha sumu hiyo kinachoweza kuwepo katika vifaa vya kuchezea na mapambo yanavyosafirishwa.


Afya ya binadamu pia huweza kuathiriwa na watu wanaomzunguka.

Iwapo una familia unayoiangalia au marafiki katika jamii yako, basi una nafasi kubwa ya kuimarisha afya yako kuliko mtu ambaye anaishi pekee au hana familia na marafiki.


Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Washington nchini Marekani umegundua kuwa, ushirikiano wa kifamilia ni jambo zuri kwa mtu na hupunguza kesi za watu kujiua, hasa wale wanaopatwa na matatizo ya mfadhaiko wa kifikra au wanapokuwa na fikra ya kutaka kujiua. 


Vilevile tamaduni, mila na desturi za jamii na jinsi watu wanavyozithamini itikadi hizo, zina mafasi kubwa katika afya zao ingawa matokeo yake huweza kuwa mazuri au mabaya.


Kwa mfano mazoea na mila ya kuwakeketa au kuwatahiri watoto wa kike na wanawake ina madhara makubwa kama vile kuongeza kiwango cha maambukizo ya magonjwa na hata matatizo ya kiakili miongoni mwa wasichama na wanawake wanaofanyiwa jambo hilo.



 Urithi wa jenetiki ni suala jingine linaloathiri afya za watu. Kuishi muda mrefu, siha ya mwili kwa ujumla na kupatwa na baadhi ya magonjwa na hata kuzaliwa nayo, ni masuala yanayoainishwa na jinsi jeni zetu zilivyo mwilini tangu wakati tunapozaliwa.


Mambo mengine ni pamoja na vyakula tunavyokula, harakati zetu kifizikia, tabia na mazoea tofauti kama kuvuta sigara au kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya.


Pia jinsi tunavyoweza kuvumilia mfadhaiko wa kifikra au stress yote hayo yana nafasi muhimu katika uzima wetu kimwili na kiakili.


Suala jingine tunaloweza kulitaja hapa ni matumizi ya vituo vya afya na hospitali. Jamii ambayo ina vituo vya afya vya kutosha, vilivyo vizuri na vyenye kukidhi mahitaji ya watu wa jamii hiyo, watu wake wana nafasi zaidi ya kuwa na siha nzuri kuliko jamii au watu wanaoishi maeneo ambayo hayana vituo vya afya au hospitali.


Kwa mfano nchi zilizoendelea zenye vituo vya afya na hospitali za kutosha na nzuri, watu wa nchi hizo huishi maisha marefu zaidi ikilinganishwa na nchi masikini zenye upungufu katika sekta hiyo. 

Jinsia ya mtu pia huathiri afya yake. Kuna magonjwa yanayowapata wanawake zaidi na kuna magonjwa yanayowapata wanaume zaidi.


Hali ya miili ya wanawake hutofautiana na wanaume na hata kazi na shughuli wanazozifanya pia huweza kuathiri afya zao kwa ujumla. Kwa mfano, kubeba mimba na kujifungua, kansa ya ovari na kizazi huathiri afya ya wanawake katika hali ambayo wanaume hupatwa na kansa ya tezi kibofu na ya korodani. 

Wakati wa vita wanaume hushiriki kwa wingi kuliko wanawake na matokeo yake ni kuuawa au kujeruhiwa. Wanawake na wasichana huenda wakawa wahanga wa vitendo vya utumiaji mabavu dhidi yao na ukatili kuliko watoto wa kiume na wanaume.

Katika baadhi ya jamii watoto wa kike na wanawake huwa hawapewi fursa ya kupata elimu na kujiendeleza kama wanaume, suala ambalo huathiri afya zao pia. Tafiti nyingi zimeonyesha ubaguzi wa kijinsia katika utoaji huduma za afya hata katika nchi zilizoendelea.


Miongoni mwa mambo muhimu yanayoijenga afya ya mwanadamu ni kula lishe salama na mlo uliokamilika. Tunaposema lishe salama na mlo uliokamilika au healthy balanced diet kwa kimombo, tunamaanisha masuala muhimu mawili.

Moja ni kula kiwango kinachotakiwa cha chakula kwa mujibu wa harakati na hitajio la mwili wako, na pili ni kula aina tofauti za vyakula vinavyotakiwa ili kuijenga siha ya mwili.


Tunapaswa kufahamu kwamba, kula lishe bora ni suala muhimu linalochangia kuimarisha afya ya mwili. Lishe salama na iliyokami inamaanisha kula vyakula tofauti kutoka katika mafungu manne makuu ya vyakula na kupunguza baadhi ya vyakula katika milo tunayokula kila siku.


Aina ya vyakula vinavyopaswa kuwepo kwenye milo yetu ni pamoja na matunda na mboga kwa wingi.  Kiwango cha kutosha cha wanga kama vile mkate, wali, viazi, pasta na vinginevyo na ni bora viwe vinatokana na aina mbalimbali za nafaka kamili zisiokobolewa.

Maziwa na vyakula vinavyotokana na maziwa kama mtindi na jibini. Vyakula vyenye protini kama vyama, samaki, mayai, maharagwe na vinginevyo na vilevile kiasi kidogo cha sukari , mafuta na chumvi.


Ufuatao ni ushauri au vidokezo muhimu (tips) kuhusiana na namna ya kula vyema ili kuzilinda na kuziimarisha afya zetu.  Tunashauriwa mlo tunaokula uwe na kiasi cha kutosha cha wanga, kwani aina hiyo ya chakula huipa miili yetu nguvu.


Tunashauriwa kula matunda na mboga kwa wingi kila siku.

Baadhi wanasema, ni bora kula aina 5 za matunda tofauti na mboga kwa siku.


Pia tunashauriwa kula samaki kwa wingi kwa uchache mara mbili kila wiki na kama hatutoweza kufanya hivyo au kwa wale ambao samaki wanawadhuru na wale wasiokula nyama, wanapaswa kula virutubishi muhimu vinavyotupatia mada zinazopatikana kwenye samaki kwa ajili ya afya ya miili yetu.


Tunashauriwa kupunguza kwa kiasi kikubwa sukari na mafuta katika milo yetu.


Vilevile tunashauriwa kula chumvi kwa kiwango kidogo, isizidi gramu 6 kwa siku kwa watu wazima.


Tunapaswa kufahamu kuwa, baadhi ya vyakula tayari vina kiwango cha chumvi ndani yake kwani karibu theluthi moja ya chumvi katika milo yetu hutoka katika vyakula ambavyo tayari vimeshatengeneza kama supu iliyo tayari, sosi, mikate, asusa (snacks), pai, pizza vyakula vinavyosindikwa na kuhifadhiwa. Hivyo kuna umuhimu wa kula vyakula hivyo kwa kiasi kidogo.


Hii ni kwa sababu ongezeko la chumvi mwilini huweza kumfanya mtu apatwe na shinikizo la damu, hali ambayo huweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi.


Suala jingine tunalopaswa kuzingatia ni kunywa maji ya kutosha, tunashauriwa kila siku kunywa kiasi cha gilasi 6 hadi 8 za maji au vyakula vingine vya majimaji kama juisi na kadhalika, ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.


Maji yana faida nyingi na baadhi yake ni kuusaidia mwili kuondoa kwa urahisi sumu na mabaki yasiyotakiwa mwilini.

Kusaidia kulainisha macho na maungio ya mwili na pia hutusaidia wakati wa kumeza.


Jambo jingine tunaloshauriwa ni kuupa mwili harakati, mazoezi ya mara kwa mara na kuwa na uzito unaotakiwa kiafya.

Jengine ni kutoacha kula kifuangua kinywa.

Tunatakiwa kustaftahi kila siku kwa sababu chakula hicho cha asubuhi huupa mwili nguvu ya kuanzia siku na huamsha utendaji kazi wa mwili kwa ajili ya siku nzima.

MADHARA YA MKATE MWEUPE (WHITE BREAD)





KWA NINI USILE TENA MKATE MWEUPE KUANZIA LEO?
Mkate ndiyo chakula kikuu cha kila siku cha familia nyingi duniani, hasa sehemu za mijini na ndiyo chakula kinachotumika na watu wa rika zote, wakubwa kwa wadogo, lakini ni wangapi tunajua kuwa mkate mweupe, ambao ndiyo chaguo namba moja la familia nyingi, ni hatari kwa afya zetu?
Kuna msemo maarufu wa Kiingereza kuhusu mkate mweupe usemao: The Whiter the Bread, the Quicker You are Dead! kwa tafsiri isiyo rasmi, msemo huu unamaanisha kuwa ‘kadiri unavyopenda kula mkate mweupe, ndivyo utakavyokufa haraka!’ Amini, usiamini, mkate mweupe siyo mzuri kwa afya yako!
Inawezekana kabisa habari hii isikufurahishe, lakini kama kweli unataka kuboresha afya yako, unapambana na suala la kupunguza unene, unataka kujiepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (Type II), ugonjwa wa moyo au saratani ya tumbo, basi huna budi ya kuachana na mkate mweupe.
Kama tulivyosisitiza kila mara katika makala zetu nyingi za nyuma kuwa vyakula vyote vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa vina hasara zaidi kiafya kuliko faida, mkate mweupe nao ni miongoni mwa vyakula hivyo.

KWA NINI USILE MKATE MWEUPE?
Kama ujuavyo, mkate unatengenezwa kutokana na ngano na mkate mweupe unatokana na unga wa ngano iliyokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu vya asili ambavyo huwa muhimu katika uimarishaji wa mfumo wa usagaji na umeng’enyaji chakula tumboni (Digestive system and metabolism).
Ili unga uwe mweupe, ngano baada ya kukobolewa husafishwa kwa mashine maalumu kwa kutumia kemikali na joto kali, kitendo ambacho huondoa kabisa virutubisho vinavyoweza kuwemo kwenye nafaka na hivyo kuiacha punje ya ngano ikiwa nyeupe na kubaki makapi.
Makapi hayo, baadaye husagwa na kuwa unga safi na mweupe ambao hutayarishwa kabla ya kutengenezwa mkate kwa kupitia hatua mbalimbali, ikiwemo hatua ya kuwekewa hamira ili uumuke, kuongezewa sukari pamoja na chumvi ili kuongeza ladha.

MADHARA YANAYOWEZA KUKUPATA KWA KULA MKATE MWEUPE
Madhara ya kwanza unayoweza kuyapata kwa kupenda sana kula mkate mweupe ni ugonjwa wa kisukari. Utafiti unaonesha kuwa mkate au chakula chochote kilichotengenezwa kutokana na unga mweupe kina kiasi kingi cha wanga ambao husababisha kuongezeka sukari mwilini.
Madhara mengine yatokanayo na mkate mweupe ni kuongezeka kwa lehemu (bad LDL cholesterol) kwenye damu, hali ambayo inaweza kusababisha presha au magonjwa ya moyo yatokanayo na kusinyaa au kuziba kwa mishipa ya damu.
Madhara hayajaishia hapo, mengine yanayoweza kukupata ni tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu. Mkate mweupe huchangia kuvuruga mfumo wa umeng’enyaji wa chakula tumboni (metabolism). Mwili unapokuwa hauna virutubisho vya kutosha, usagaji na uondoaji wa sumu mwilini huwa wa shida na uchafu unaporundikana tumboni kwa muda mrefu bila kutoka, husababisha kansa ya tumbo!

ULE NINI BADALA YA MKATE?

Kuna aina nyingine ya mkate ambayo ndiyo unayopaswa kula, mkate huo ni BROWN BREAD au MKATE MWEUSI kama unavyojulikana na wengine. Mkate huu hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa hivyo kuwa na virutubisho vyake asilia vinavyohitajika mwilini na kuwa na faida zitakazokuepusha na kupatwa na madhara yaliyotajwa hapo juu. Mkate huu hauna sukari wala chumvi, hivyo kuwa bora zaidi kwa afya yako. Kama kweli unajijali, utaacha kula mkate mweupe na kuanza kula huu mweusi leo!

Jumanne, 22 Oktoba 2013

SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?

Habari za asubuhi wapendwa wafuatiliaji wa blog hii! kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuweza kuniamsha salama nikiwa na afya njema.


Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke  akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba, utupaji wa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25 kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35)

 Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi.

 NAMNA YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO.

Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata, kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 December basi hiyo ndio siku yako ya kwanza.

Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.

Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?
Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa24 hadi 48 baada ya kujamiiana hivyo kama utafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.

kwa leo tuishie hapo mpendwa mfuatiliaji ili kukuachia nafasi ya kuchangia zaidi na kuboresha yale ambayo sikuweza kuelezea hapo
.

Jumanne, 8 Oktoba 2013

UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)

Utangulizi 

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba. 

Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua. 




Pumu husababishwa na nini? 

Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu. 

Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu kama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio

Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi. 

Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo: 

-Vumbi 
-Mende 
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani 
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k 

Viwasho kama: 
-Moshi wa sigara 
-Uchafuzi wa hewa 
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula) 
-Msongo wa mawazo 
-Dawa kama Aspirin 
-Ugonjwa wa kucheua 
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali 
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k.

Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi. 

Vigezo hatarishi 

Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na: 

-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio 

-Kuvuta hewa iliyo na moshi 

-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki 

-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu 
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto. 

-Unene wa kupita kiasi (obesity) 

-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease) 

Dalili za Pumu 

Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo: 

-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri 

-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua 

-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani. 

-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu. 

-Kupumua haraka haraka 

Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu. 

Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku. 

Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea. 

Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku. 
Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa. 

MANUFAA YA KABICHI KIAFYA



Kabichi ni zao linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani. Mboga hii imekuwa ikiwekwa katika hadhi ya chini katika mboga, na hata watu huitumia pale tu wanapoona hakuna jinsi ya kupata mboga ya aina nyingine. Na hivyo utaona ikitumika katika sehemu za jumuiya kama vile shule, magerezani na vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo huweza kuhimili hali ya kuinunua kwa matumizi ya watu wengi. Mboga hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ni mpya ya kijani/nyekundu au hata zambarau na siyo ile iliyokaa sana sokoni hadi kusinyaa, hiyo haina manufaa. Mboga hii ina faida zifuatazo:

1. AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO

2. HUIMARISHA MFUMO WA MOYO

3. KINGA DHIDI YA SARATANI

4. INAUPA MWILI VITAMINI VIFUATAVYO: Vitamin K, Vitamin B12, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.




LIKE, COMMENT, NA SHARE KAMA UMEJIFUNZA NA KUELEWA SOMO HILI.
KWA MAELEZO NA USHAURI ZAIDI PIGA SIMU +255713354389 / 0752133700

Jumatatu, 7 Oktoba 2013

SARATANI YA TEZI DUME

Tatizo jingine linaloathiri tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume wa umri mbalimbali duniani. Aidha ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya miaka 40.
Nani yupo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume?
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:
  • Wanaume wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu
  • Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea
  • Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
  • Wanaume wanaokunywa pombe kupindukia
  • Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
  • Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali
  • Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
  • Wachimbaji wa madini hususani aina ya cadmium
  • Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
Pamoja na kwamba, tatizo la kukua na kuongezeka kwa tezi dume yaani BPH hutokea kwa wanaume wengi, hali hiyo haiongezi uwezekano/hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na
  • Kupata shida unapoanza kukojoa
  • Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na
  • Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
  • Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
  • Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
Saratani ya tezi dume inatibika?
Ndiyo! Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.
Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi, wakati kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu bila kumfanyia upasuaji au bila kumpatia tiba ya mionzi.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

LIKE, COMMENT, NA SHARE KAMA UMEJIFUNZA NA KUELEWA SOMO HILI.
KWA MAELEZO NA USHAURI ZAIDI PIGA SIMU +255713354389 / 0752133700

Jumapili, 6 Oktoba 2013

Faida za tikikiti maji kiafya




KWA UFUPI
  • Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi


Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi;  na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.
  Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha  lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
 Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Tikiti pia lina  amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa  peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.