Jumanne, 17 Septemba 2013

UJIEPUSHE NA KIHARUSI KWA KULA NYANYA.


SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote.

Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.
Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusukirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.
Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi hufariki dunia nchini humo kutokana na kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.
Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.

Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari, hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya za aina zote una faida, iwe ni ile inayopikwa pamoja na mboga au ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali.

Jumatatu, 16 Septemba 2013

Sababu ya kukoroma na jinsi ya kuzuia hali hiyo



Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?
Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:
• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma. 
• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma. 
• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.
• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.
• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa. 



Je, Dawa ya kukoroma ni nini?
Swali hilo limeuliwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa. 
Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:
1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.
2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.
3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.
4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.





Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:
 Punguza uzito
ü
 Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
ü 
 Wacha kuvuta sigara.
ü
 Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.
ü


Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile 
o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini
.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini. 
Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

Jumapili, 15 Septemba 2013

MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA.



Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400 zimegundulika kuwa na madhara makubwa katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa  mwaka. Hata hivyo, vitu vitatu hatari zaidi katika sigara ni:

1.     Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili. 
2.   Nicotine:   Hiki ni kitu chenye sumu ambacho kwa muda mrefu san akimetumiwa kama dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya. Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili wa binadamu. 
3.     Carbonmonoxide: Hii ni gesi inayopatikana katika moshi wa sigara. Madhara mbalimbali ya vitu vinayopatikana katika moshi wa sigara ni kama yafuatayo: 

1.    Kuharibika kwa utando mlaini katika njia za hewa: katika njia ambayo pumzi hupita kuna kama tabaka fulani ambalo ni laini limezunguka katika njia. Tabaka hili hufany akazi ya kuzuia vumbi vumbi linaloingia pamoja na hewa. Ile tabia ya uvutaji hufanya vile vitu vinavyopatikana katika moshi wa sigara kuganda katika utando huu na kusababisha njia kuwa nyembamba kwa kule kuongezeka kwa takataka na kemikali katika njia, hivyo kumfanya mvutaji apate shida ya pumzi hapo baadaye. 


2.   Vidonda vya tumbo: uvutaji wa sigara huchochea utengenezaji wa acid ambayo huweza kumletea mvutaji huyo vidonda vya tumbo. 


3.    Matatizo katika mfumo wa upumuaji:  wavutaji hupata shida katika koo na mapafu hivyo kupata kifua mara kwa mara na maumivu na mwishowe kupata madhara makubwa katika mfumo mzima wa upumuaji kutokana na kuharibika kwa mapafu kama tutakavyozungumzia katika pointi namba 7 hapo chini. Hali ya hewa huwaathiri sana wavutaji sigara kwani hupata pneumonia na asthma. 


4.  Udhaifu katika mifupa (Osteoporosis): katika moshi kuna metali ijulikanayo kama cadmium ambayo inaweza kusababisha matatizo katika mifupa, hii husababisha kupoteza asilimia 30 ya calcium katika mifupa. Kwa wanawake uvutaji wa sigara umeonekana kuzuia shughuli ya estrogen na kitu chochote kinachozuia estrogen kufanya kazi husababisha udhaifu katika mifupa (Osteoporosis) na hii huweza kusababisha maumivu ya mara kwa mara katika mifupa. 


5.   Kuwahi kumaliza kufikia mzunguko wa mwezi (Menopause): Menopause ni ile hali ya mwanamke kufikia mwisho wa mzunguko wake wa kila mwezi ambao humpelekea kushika ujauzito, hali hii huanza kutokea akifikia umri wa miaka 45 – 55, hutofautiana. wanawake wanaovuta sigara hufikia menopause miaka mitano mapema zaidi ya wasiovuta. 


6.   Athari kwa wenye mimba: wanawake wanaovuta sigara huwa katika hatari kubwa sana ya mtoto kutoka kabla ya siku zake (Abortion) au kuua mtoto tumboni. Au hata mtoto kufa mapema zaidi pindi atakapozaliwa.


7.     Kuharibika kwa Alveoli za mapafu (Emphysema):  ile harufu kali ya moshi huharibu alveoli ndogo ndogo katika mapafu. Hii kwa kiasi kikubwa sana hupunguza eneo ambalo Oxygen hukutana na damu na hivyo kusababisha  hali inayoitwa Emphysema. Hali hii hujitengeneza taratibu sana na kimya kwa muda mrefu. Wavutaji wote wana Emphysema kwa kiwango fulani Lakini kutokana na eneo kubwa wanaloishi ambalo hupatikana Oxygen, watu wengi hawajui kwamba wana hali hii. (watu wengi wana takriban alveoli milioni 300 katika mapafu yao) hivyo ni vigumu kugundua hali hii na baadhi hujijua pale wanapofanya mazoezi kwa mfano, na kuhisi ugumu wa pumzi.


8.      Upungufu wa uwezo wa kubeba oxygen katika damu: Carbon Monoxide (CO) inapatikana katika moshi. Uhusiano wa Carbon Monoxide kwa Haemoglobin ni mkubwa mara 200 zaidi ya Oxygen. Hivyo baadhi ya haemoglobin ya damu huzuiwa na Carbon Monoxide kwa wavutaji kwani haemoglobin badala ya kuchukua Oxygen huenda katika Carbon Monoxide na hivyo uwezo wa kubeba oxygen katika damu hupungua.


9.  Kansa/Saratani: Katika asilimia kubwa ya watu wenye kansa hupatikana kutoka kwa wavutaji wa sigara, saratani za ngozi, koo, utumbo, kibofu, mdomo n.k. vilevile saratani ya figo, kongosho, tumbo na kizazi imeonekana mara chache kwa wavutaji wa sigara.


10.Kupungukiwa na vitamin: Uvutaji wa sigara husababisha upungukiwaji wa Vitamin hasahasa Vitamin C. ule uvutaji wa sigara moja tu unaweza kupunguza kiasi cha Vitamin C ambacho kinaweza kulingana na ukubwa wa kutumia chungwa moja tu. Hivyo inashauriwa kula sana Vitamin C ili kurekebisha hali hii. 


11. Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha kisukari: Nicotine huchochea sukari katika damu kwa kuilazimisha au kuichochea Adrenaline na Non Adrenaline ambayo hufanya ini na misuli kupeleka sukari katika mishipa ya damu. Hii hufanya kongosho ifanye kazi ya kutoa Insuli mara kwa mara ili kudhibiti sukari kama kawaida yake na kutokana na kufanya kazi huku mara kwa mara hufanya kongosho ichoke haraka na kushindwa tena kudhibiti sukari, hivyo humsababishia mtu huyu kisukari. Kwa upande wangu hizo ndizo athari zinazotokana na uvutaji wa sigara, hivyo basi jaribu kulinganisha yale manufaa ya muda mfupi anayoyapata mvutaji na hasara zake. Hapo utaona kwamba uvutaji wa sigara ni hatari sana kwa afya yako, na ni bora ujitahidi sana uache ili kuboresha afya yako.


KWA USHAURI ZAIDI WASILIANA NA MTAALAM KWA 0713354389 / 0752133700

ZIJUE KANUNI ZA ULAJI SAHIHI


Tumeshaandika mambo mengi kuhusu umuhimu wa mtu kula matunda, mboga na vyakula vya nafaka, leo tunaandika muhtasari wa kanuni za ulaji sahihi ambazo zikizingatiwa na zikaenda sambamba na ulaji wa vyakula vinavyokubalika kiafya, kutakuwa hakuna shaka kuhusu ujenzi wa msingi imara wa afya bora.

USILE CHAKULA KINGI KUPITA KIASI
Kila mtu anakula chakula kulingana na mahitaji ya mwili wake. Mbeba zege, hawezi kula sawa na anayefanyakazi ya kukaa ofisini, kula kiasi ambacho kinalingana na mahitaji ya mwili wako. Kanunni ya kula inasema acha kula wakati bado hujashiba vizuri. Kwa kawaida, mahitaji ya chakula ya mwili ni kiasi cha ‘kalori’ 2000 kwa siku, ikitegemeana na umri, jinsia, urefu, uzito na kazi anazozifanya mtu.

KULA VYAKULA MCHANGANYIKO
Ulaji sahihi ni ule wa kula vyakula mchanganyiko vya aina tofauti, hasa mboga za majani, matunda, vyakula vya nafaka ambavyo huwa huvili mra kwa mara. Kwa kula vyakula mchanganyiko utapata faida ya kuwa na virutubisho tofauti mwilini na kuondoa upungufu wowote wa vitamini unaweza kuwepo mwilini bila wewe kujijua.

KULA SANA MATUNDA NA MBOGA
Ni kawaida ya watu wengi kutokula matunda kabisa katika staili yao ya maisha ya kila siku, ikitokea amekula tunda au mboga ni kwa bahati mbaya tu. Hili ni kosa kubwa sana unaloweza kuwa unalifanya katika afya yako ambalo baadae lina kukagharimu sana bila kujua chanzo chake ni kutokula matunda.
Hivyo hakikisha siku haipiti bila kula matunda na mboga. Kiwango kinachopendekezwa na Shirika la Afya Duniani, ni kwa mtu mmoja kula milo ya matunda na mboga mboga kati ya 4 – 6 kwa siku, mlo mmoja unaweza kuwa sawa na ujazo wa kisahani cha chai. Kama huna uwezo huo, basi hata tunda moja linakushinda?

KUNYWA MAJI MENGI
Kama kuna kosa lingine kubwa unaloweza kulifanya katika mwili wako ni kutokunywa maji. Haishangazi kuona mtu hana mazoea ya kunywa maji hadi pale anapopatwa na kiu na akinywa ni glasi moja tu.
Imeelezwa na wataalamu wetu kuwa asilimia 75 ya mwili wa binadamu ni maji. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku nayo ni sehemu ya ulaji sahihi. Maji ndiyo yanayosaidia kusafisha mifumo ya mwili na kutoa nje uchafu na sumu, hasa kwenye kibofu cha mkojo na figo. Watu wanaopatwa na matatizo ya viungo hivyo ni wale wenye tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.

PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI
Ili kuwa na afya bora, epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari au punguza kiwango cha sukari unachoweka kwenye vinywaji ama vyakula vyako unavyopika. Inaelezwa kuwa mtu akiwa anakunywa soda moja tu kwa siku, baada ya mwaka mmoja uzito wake unaweza kuongezeka kwa karibu kilo 10, kwani soda ni miongoni mwa vinywaji vyenye sukari nyingi.

KUWA HURU NA VYAKULA
Iwapo utazingatia ulaji sahihi, bila shaka utakuwa huru kula mara moja moja vyakula vingi, hata vya kukaanga bila kupata matatizo yoyote. Kwani chakula ni chanzo kizuri cha furaha na mtu mwenye furaha hujiepusha na magonjwa ya moyo pia. Hivyo zingatia ulaji sahihi ili uwe huru wa kula vyakula vya aina vyote katika kiwango kinachokubalika.

JISHUGHULISHE
Mwisho, ili lishe yako au ulaji wako sahihi ufanyekazi yake vizuri na kukupa afya njema, lazima ufanye mazoezi au ujishughulishe na kazi mbalimbali za kila siku. Kula vizuri bila kuushughulisha mwili, hakuwezi kuwa na faida kiafya. Aihda katika hili, mambo 3 hayana budi yazingatiwe, nayo ni Lishe Bora, Mazoezi na kupumzika.

KWA USHAURI ZAIDI PIGA SIMU 0752133700 / 0713354389

Jumatano, 11 Septemba 2013

SABABU ZINAZOPELEKEA MIMBA KUTOKA KABLA YA MDA.

Tatizo la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi. Kutokana na maombi ya wasomaji wetu, tutalijadili kwa kina tatizo hili ambalo kitaalamu huitwa Miscarriage.
MISCARRIAGE NI NINI?
Kwa kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.
Inapotokea kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.
Katika hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha kifo.
NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).

NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE? 
Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.

Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)
Hitilafu katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki 13.
Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya mtoto na kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.

2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency)
Homoni ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha ujauzito kuharibika na kutoka kabla ya muda wake.


TATIZO HILI LINATIBIKA KABISA. PIGA SIMU 0752133700 / 0713354389 KWA MAELEZO NA USHAURI.

Itaendelea wiki ijayo.

Jumanne, 10 Septemba 2013

LISHE BORA KWA AFYA YA UBONGO WAKO


Kama ilivyo ada, chakula hutoa majibu ya maswali mengi yanayotukabili katika ustawi wa afya zetu kila siku. Chakula pia kikitumiwa ipasavyo, huwa dawa kwa kila aina ya ugonjwa, kama ambavyo tumeshaona katika makala zetu nyingi zilizopita.
Katika makala ya leo, tunaangalia baadhi ya vyakula ambavyo vimetajwa kama tiba au ufumbuzi wa tatizo fulani, iwe kwa muda mfupi ama kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa habari iliyotolewa mapema mwezi huu na mtandao wa ‘Men’s Health’, kuna vyakula vikiliwa huongeza ufanisi wa ubongo!
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida moja la saikolojia nchini Uingereza, ingawa ubongo unawakilisha asilimia mbili tu ya uzito wa mwili wa binadamu, lakini unawakilisha asilimia 20 ya utowaji wa mahitaji ya nishati mwilini, hivyo ukiupatia chakula sahihi, unaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi na kufikia hata kiwango cha asilimia 200, bila kujali kama una umri wa mika 15 au 40!
KAHAWA
Ingawa kahawa si miongoni mwa vinywaji bora vyenye faida kubwa mwilini, lakini ikitumika kwa kiasi ina faida moja kubwa ya kuchangamsha ubongo na kuamsha kumbukumbu kwa muda mfupi. Katika utafiti mmoja uliofanywa nchini Uingereza, ulionesha kuwa kikombe kimoja cha kahawa husaidia kuchangamsha kumbukumbuka na mbinu za kutatua matatizo, ndiyo maana watu wengi hupenda kutumia kahawa kwa sababu hii.
Lakini tahadhari inatolewa kwamba unywaji wa kahawa usiwe mkubwa. Katika jitihada za kuchangamsha ubongo, ikiwa ni kimbilio la muda mfupi, hutakiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja kwa siku, vinginevyo utajitakia matatizo mengine ya afya.
MATUNDA
Kahawa itakusaidia kuchangamsha ubongo wako kwa muda mfupi, lakini suluhisho la muda mrefu na la kudumu katika kuufanya ubongo ufanye kazi yake sawasawa ni kula matunda ya aina mbalimbali, hasa bluberi (blueberry) ambayo yameonesha ufanisi mkubwa katika ubongo wa binadamu.
SAMAKI NA DAGAA
Samaki na dagaa wameorodheshwa katika kundi la vyakula vinavyomuongezea mlaji uwezo mkubwa wa kufikiri mambo kwa haraka, kiwango chake cha kuongeza uwezo wa kufikiri ni kikubwa sana.
Kwenye samaki hao kuna virutubisho aina ya ‘Omega -3’ na ‘Niacin’ ambavyo vinaaminika kuwa msingi wa ujenzi wa tishu za ubongo wa mwanadamu, hivyo kwa kula kwa wingi mara kwa mara, utaimarisha uwezo wako wa kufikiri.
MTINDI AU KARANGA MCHANGAYIKO
Ili kupunguza wasiwasi katika mazingira tofauti, pendelea kunywa mtindi usio na mafuta (low fat- yogurt) au pendelea kula karanga na korosho. Wana sayansi wa nchini Slovakia waliwafanyia utafiti wa kuzungumza wanafunzi kadhaa kwa kuwapa virutubisho maalum vinavyopatikana kwenye mtindi na karanga na matokeo yalionesha kuwa waliweza kutoa hotuba bila ‘presha’ tofauti na wale waliotoa bila kutumia virutubisho hivyo.
Wakati mtindi una sifika kwa kumfanya mnywaji kuwa mtulivu wa akili, unywaji wa soda kwa wingi (kiasi cha chupa mbili na nusu) kwa siku, kunamfanya mtu kuzubaa na wakati mwingine kupatwa na mfadhaiko wa akili, hii ni kwa mujibu wa jarida moja la Marekani linalotoa machapisho kuhusu masuala ya afya za watu (American Journal of Public Health). Hivyo mnaopenda kunywa soda kwa wingi kwa siku, jueni mna uchosha mwili.
MBOGA
Tabasamu au hasira huwa haiji tu hivihivi, bali wakati mwingine huchangiwa na homoni mwilini. Ulaji wa mboga za kijani pamoja na kabichi, utafiti unaonesha kuwa hutoa kiasi kikibuwa cha Vitamini B6 ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa homoni zinazomfanya mtu ajisikie vizuri na kuwa na tabasamu wakati wote (feel-good hormones). Utafiti unaonesha kuwa ukosefu wa Vitamin B6 mwilini, kunaweza kumsababishia mtu wasiwasi, hasira na hata mfadhaiko wa akili.

Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea.


KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.
Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.
AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili  ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano  wanasema kuwa hupata maumivu     makali.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
 Endometriosis: Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo
Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.
PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

TATIZO HILI LINATIBIKA KABISA. WASILIANA NA MTAALAM KWA +255752133700 / +255713354389
Itaendelea............