Jumanne, 10 Septemba 2013

LISHE BORA KWA AFYA YA UBONGO WAKO


Kama ilivyo ada, chakula hutoa majibu ya maswali mengi yanayotukabili katika ustawi wa afya zetu kila siku. Chakula pia kikitumiwa ipasavyo, huwa dawa kwa kila aina ya ugonjwa, kama ambavyo tumeshaona katika makala zetu nyingi zilizopita.
Katika makala ya leo, tunaangalia baadhi ya vyakula ambavyo vimetajwa kama tiba au ufumbuzi wa tatizo fulani, iwe kwa muda mfupi ama kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa habari iliyotolewa mapema mwezi huu na mtandao wa ‘Men’s Health’, kuna vyakula vikiliwa huongeza ufanisi wa ubongo!
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida moja la saikolojia nchini Uingereza, ingawa ubongo unawakilisha asilimia mbili tu ya uzito wa mwili wa binadamu, lakini unawakilisha asilimia 20 ya utowaji wa mahitaji ya nishati mwilini, hivyo ukiupatia chakula sahihi, unaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi na kufikia hata kiwango cha asilimia 200, bila kujali kama una umri wa mika 15 au 40!
KAHAWA
Ingawa kahawa si miongoni mwa vinywaji bora vyenye faida kubwa mwilini, lakini ikitumika kwa kiasi ina faida moja kubwa ya kuchangamsha ubongo na kuamsha kumbukumbu kwa muda mfupi. Katika utafiti mmoja uliofanywa nchini Uingereza, ulionesha kuwa kikombe kimoja cha kahawa husaidia kuchangamsha kumbukumbuka na mbinu za kutatua matatizo, ndiyo maana watu wengi hupenda kutumia kahawa kwa sababu hii.
Lakini tahadhari inatolewa kwamba unywaji wa kahawa usiwe mkubwa. Katika jitihada za kuchangamsha ubongo, ikiwa ni kimbilio la muda mfupi, hutakiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja kwa siku, vinginevyo utajitakia matatizo mengine ya afya.
MATUNDA
Kahawa itakusaidia kuchangamsha ubongo wako kwa muda mfupi, lakini suluhisho la muda mrefu na la kudumu katika kuufanya ubongo ufanye kazi yake sawasawa ni kula matunda ya aina mbalimbali, hasa bluberi (blueberry) ambayo yameonesha ufanisi mkubwa katika ubongo wa binadamu.
SAMAKI NA DAGAA
Samaki na dagaa wameorodheshwa katika kundi la vyakula vinavyomuongezea mlaji uwezo mkubwa wa kufikiri mambo kwa haraka, kiwango chake cha kuongeza uwezo wa kufikiri ni kikubwa sana.
Kwenye samaki hao kuna virutubisho aina ya ‘Omega -3’ na ‘Niacin’ ambavyo vinaaminika kuwa msingi wa ujenzi wa tishu za ubongo wa mwanadamu, hivyo kwa kula kwa wingi mara kwa mara, utaimarisha uwezo wako wa kufikiri.
MTINDI AU KARANGA MCHANGAYIKO
Ili kupunguza wasiwasi katika mazingira tofauti, pendelea kunywa mtindi usio na mafuta (low fat- yogurt) au pendelea kula karanga na korosho. Wana sayansi wa nchini Slovakia waliwafanyia utafiti wa kuzungumza wanafunzi kadhaa kwa kuwapa virutubisho maalum vinavyopatikana kwenye mtindi na karanga na matokeo yalionesha kuwa waliweza kutoa hotuba bila ‘presha’ tofauti na wale waliotoa bila kutumia virutubisho hivyo.
Wakati mtindi una sifika kwa kumfanya mnywaji kuwa mtulivu wa akili, unywaji wa soda kwa wingi (kiasi cha chupa mbili na nusu) kwa siku, kunamfanya mtu kuzubaa na wakati mwingine kupatwa na mfadhaiko wa akili, hii ni kwa mujibu wa jarida moja la Marekani linalotoa machapisho kuhusu masuala ya afya za watu (American Journal of Public Health). Hivyo mnaopenda kunywa soda kwa wingi kwa siku, jueni mna uchosha mwili.
MBOGA
Tabasamu au hasira huwa haiji tu hivihivi, bali wakati mwingine huchangiwa na homoni mwilini. Ulaji wa mboga za kijani pamoja na kabichi, utafiti unaonesha kuwa hutoa kiasi kikibuwa cha Vitamini B6 ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa homoni zinazomfanya mtu ajisikie vizuri na kuwa na tabasamu wakati wote (feel-good hormones). Utafiti unaonesha kuwa ukosefu wa Vitamin B6 mwilini, kunaweza kumsababishia mtu wasiwasi, hasira na hata mfadhaiko wa akili.

Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea.


KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.
Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.
AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili  ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano  wanasema kuwa hupata maumivu     makali.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
 Endometriosis: Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo
Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.
PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

TATIZO HILI LINATIBIKA KABISA. WASILIANA NA MTAALAM KWA +255752133700 / +255713354389
Itaendelea............

Jumatatu, 9 Septemba 2013

HABARI NJEMA SANA KWA WANAWAKE WASIO NA ASHKHI YA TENDO LA NDOA

Wanawake  wengi  nchini  na  duniani  kwa  ujumla  wanasumbuliwa  na  tatizo  la kukosa  hamu  ya  kufanya  tendo  la  ndoa  ( LACK  OF  LIBIDO ) pamoja  na  tatizo  la  kutofika  kileleni.  Inasadikiwa  kuwa, katika  kila  wanawake  kumi, angalau  wanne  kati  yao  wanasumbuliwa  na  tatizo  la kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa  na  kutofika  kileleni  wakati  wa  tendo

.

  SABABU  ZA  WANAWAKE  KUKOSA  HAMU  YA  TENDO  LA  NDOA.

Sababu  zinazo  changia  tatizo  hili  zimegawanyika  katika  makundi  makuu  mawili :  (  A  )  Sababu  za  Kisaikolojia { Psychological )  na  (  B  )  Sababu  za  Kimwili  {  Physical  }


A.  SABABU  ZA    KIMWILI  "  PHYSICAL"


1.  Anaemia  (   ugonjwa  huu  ni  very  common  kwa  wanawake  kwa  sababu  ya  kupoteza  madini   ya  chuma  wakati  wa   hedhi  )

2. Ulevi  Kupita  kiasi  (  Alcoholism  )
3. Utumiaji  wa  Dawa   Za  Kulevya  ( Kama  Vile  bangi  n.k  )
4. Magonjwa  makubwa  kama  vile  kisukari.

(  Sababu  zipo  nyingi  sana, hizi  ni  baadhi  tu  )

B :  SABABU  ZA  KISAIKOLOJIA  " PSYCHOLOGICAL "
1. Depression   
2. Stress  and  overwork
3Anxiety  "  Woga"
4. Kunyanyaswa  kijinsia  ama  kubakwa  wakati  wa  utotoni
5   Kuwa  katika  matatizo  makubwa  na  mpenzi  wako.
6. Kuishi  katika  mazingira  magumu  mfano  kushare  nyumba  ama  chumba  na  wazazi  wako, wakwe  zako  ama  watoto  wako.

HIZI  NI  BAADHI  YA  SABABU  ZINAZO  WAFANYA  WANAWAKE  WENGI  LEO  HII  KUKOSA  HAMU  YA  KUFANYA   TENDO  LA  NDOA NA  KUTOFURAHIA  TENDO HILO
.
Hata  hivyo  sababu  hizi  hazimuhusu  kila  mwanamke, wanawake  wengine  wanasumbuliwa  na  tatizo  hilo  tangu  walipo  vunja  ungo. 

KUSHINDWA  KUFIKA  KILELENI  KWA  WANAWAKE :  Hali  hii  husababishwa  na  sababu   nyingi  za  kimwili  na  kisaikolojia  kama  vile  kuwa  na  msongo  wa  mawazo, presha,woga, wasiwasi  wa  tendo  la  ndoa  ,kubakwa ama  kudhalilishwa  wakati  wa  utotoni, na/ama  kufanya  tendo  hilo  na  mwanaume  mwenye  uwezo  mdogo  wa  kiufundi.


 Ewe  mwanamke  unayesumbuliwa  na  tatizo  hili, usiendelee  kusumbuka,  na  tatizo  hili. Fika  katika  ofisi  za  NEW LIFE AFYA zilizopo  katika  eneo  la  SINZA PALESTINA karibu  na  HOSPITAL YA SERIKALI PALESTINA JIJINI DSM  au  tupigie  simu  0713354389 au 0752133700.

Unywaji wa soda husababisha kansa ya tezi kongosho

Mapema mwaka huu iliripotiwa na majarida kadhaa sehemu mbalimbali duniani kuwa, kwa mujibu wa utafiti mpya, unywaji wa soda angalau chupa mbili kila wiki huongeza uwezekano wa kupata kansa ya tezi kongosho.
Tezi kongosho lipo nyuma ya tumbo likiwa na kazi ya kuzalisha homoni ya insulin ambayo hufanya kazi ya kuchochea seli zinyonye sukari kutoka katika damu mara baada ya mtu kula au kunywa kitu chenye sukari. Pia hutoa vimeng’enyo ambavyo husaidia katika usagaji wa vyakula vyenye mafuta na protini.
Walio fanya utafiti huo wanasema kuwa watu wanywao chupa mbili au zaidi za vinywaji baridi kama soda kwa wiki wana uwezekano wa karibu asilimia 87 wa kupata kansa ya tezi kongosho ikilinganishwa na wale wasiotumia vinywaji vya aina hiyo. Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la Cancer Epidemiology, Biomarkers & Prevention linalomilikiwa na chama cha tafiti za saratani cha Marekani.
Hata hivyo makampuni yanayohusika na utengezaji wa vinywaji baridi wameupinga utafiti huo wakidai kuwa ulikuwa na walakini na makosa mengi, huku wakiegemea katika matokeo ya tafiti zilizowahi hapo kabla ambazo zilionesha kutokuwepo kwa uhusiano wowote kati ya unywaji soda na kansa ya kongosho.
Katika utafiti wa sasa uliojumuisha watu 60,524 wenye asili ya Singapore na China na ambao ulitumia karibu miaka 14 kukamilika (kuanzia mwaka 1993), watafiti walichunguza vyakula na vinywaji wanavyokula waliohojiwa na kama walipata kansa katika kipindi chote cha ufuatiliaji.
Watafiti waliuliza washiriki kuhusu vitu wanavyokula ikiwemo soda (ingawa hawakugusia kuhusu diet soda kwa vile kwa wakati huo matumizi ya diet soda nchini Singapore yalikuwa chini sana) na juisi na iwapo vinywaji hivyo vilikuwa vya kawaida au vilikuwa na vitu vya kuongeza ladha (utamu).
Washiriki waliwekwa katika makundi matatu, wale wasiokunywa kabisa vinywaji baridi (soda au juisi), wanaokunywa chini ya chupa mbili kwa wiki, na wale wanaokunywa chupa mbili au zaidi kwa wiki. Katika kipindi cha miaka 14 ya ufuatiliaji, watafiti wanadai walikuta washiriki 140 wakiwa na kansa ya tezi kongosho. Aidha watafiti wanadai kuwa, wale waliokuwa wanakunywa chupa mbili au zaidi kwa wiki walikuwa na hatari ya kupata kansa kwa karibu asilimia 87. Hata hivyo, hakukuwa na uhusiano wowote kati ya unywaji juisi na hatari ya kupata kansa ya kongosho.
Watafiti hao wanaamini kuwa sukari iliyomo katika soda husababisha ongezeko la homoni ya insulin kutoka katika tezi kongosho, hali ambayo hufanya tezi hilo kufanya kazi kupita kiasi na hatimaye kupata kansa.
Hata hivyo wanasayansi kutoka baadhi ya viwanda vya soda wamekosoa matokeo ya utafiti huo wakisema kuwa utafiti huo ulikuwa na mapungufu na udhaifu mwingi sana. Mojawapo ya mapungufu hayo, wanadai wanasayansi ni kuwa idadi ya watu waliogundulika kuwa na kansa ya kongosho ilikuwa ndogo mno na hata miongoni mwa hao 140 waliogundulika, bado washiriki 110 waliripotiwa kuwa katika kundi la wale wasiokunywa kabisa soda, 12 walikunywa soda chini ya mbili kwa wiki wakati ni watu 18 tu waliokuwa katika kundi la wanywaji soda mbili au zaidi kwa wiki. Hii inaonesha kuwa kulikuwa na idadi ndogo mno ya watu waliokutwa na kansa ikilinganishwa na umati ulioshiriki katika utafiti huo.
Utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2008 ulishindwa kuonesha uhusiano wowote kati ya matumizi ya soda na kutokea kwa kansa ya kongosho; wakati mtafiti mmoja kutoka kituo cha saratani cha Yale nchini Marekani alisema kuwa matokeo haya hayana budi kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa kwa kuzingatia idadi ndogo ya watu waliogundulika kuwa na kansa na kushindwa kwa utafiti huo kuonesha jinsi unywaji soda unavyoweza kusababisha saratani.
Hata hivyo pamoja na tafiti nyingi kutofautiana na matokeo ya utafiti huu, zipo baadhi ya tafiti ambazo zilitoa matokeo yenye kuonesha kufanana kiasi fulani. Kwa mfano mtafiti Laurence N. Kolonel kutoka Kituo cha Utafiti wa Saratani katika chuo kikuu cha Hawaii, Honolulu huko Marekani alisema kuwa matokeo ya utafiti huu kwa kiasi fulani yanafanana na ya utafiti wao wa mwaka 2007 ambapo waligundua kuwepo kwa uhusiano kati ya utumiaji wa vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose na saratani ya kongosho. Anasema kuwa kwa vile vinywaji baridi vingi vinatumia fructose kwa ajili ya kuongeza ladha, matokeo ya utafiti wao yanafanana sana na matokeo ya utafiti huu.
Tatizo jingine linaloonekana katika matokeo ya utafiti huu ni kushindwa kwa watafiti wake kuonesha ni kwa vipi walifikia hitimisho la kuwepo kwa uwezekano wa 87% wa mtu kupata saratani kutokana na unywaji wa soda, tukitilia maanani ukweli kuwa saratani ya kongosho ni ugonjwa unaotokea kwa nadra sana duniani kote (huwapata wastani wa watu 12 kwa kila watu 100,000).
Kwa maneno mengine ni kuwa matokeo ya utafiti huu hayawezi kutumika kutoa hitimisho kuwa unywaji wa soda unasababisha saratani ya tezi kongosho isipokuwa yanaonesha wanywaji wa soda huelekea kupata saratani ya kongosho zaidi ya wale wasio wanywaji.

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KIAFYA.

Umuhimu wa kufanya mazoezi
Iwe unafanya mazoezi kwa nia ya kuwa na umbo lenye muonekano mzuri, au kupoteza muda wa ziada ulionao, mazoezi ni zaidi ya unavyoweza kufikiria.
Ongezeko la tafiti katika eneo la mazoezi na magonjwa yahusianayo na mifumo ya maisha lililotokea ndani ya takribani miaka kumi iliyopita, limefumbua macho ya wengi juu ya umuhimu wa mazoezi katika kujikinga na kutibu magonjwa mbalimbali. Tafiti katika eneo hili zinaonesha kwamba mazoezi yanaweza kutumika kujikinga na magonjwa zaidi ya ishirini na kutibu magonjwa takribani kumi.
Ni jambo lililowazi kabisa kwamba babu zetu waliweza kuishi kwa miaka mingi zaidi ya kizazi tulichopo sisi. Ni dhahiri pia kwamba kizazi chetu kinashuhudia milipuko ya magonjwa ambayo babu zetu hawakuwahi hata kuyasikia. Pia mtakubaliana nami kuwa, kumekuwa na mambo mengi ya kimaendeleo yaliyotokea katika kipindi chote hiki, ambayo wanazuoni wamekuwa wakiyahusisha na milipuko ya baadhi ya magonjwa. Yapo mambo mengi katika mifumo yetu ya maisha ya kila siku yaliyo mazuri katika muonekano na hisia, lakini ukweli ni kwamba yaweza kuwa na athari kubwa kwa afya zetu.
Kila mtu anapenda kuendesha gari wakati wote anapohitajika kwenda sehemu, pia watu wengi wanafurahia kuketi na kuangalia vipindi wavipendavyo katika runinga muda wote wapatapo wasaa. Si ajabu pia watu wengi wanapenda shughuli zisizohitaji kutembea tembea au kutumia nguvu. Ukweli ni kwamba katika jamii zetu za kiafrika, mambo yaliyotajwa hapo juu ni vielelezo halisi vya mtu kuwa na maisha mazuri, na kinadharia hakuna mtu asiyependa maisha mazuri. Kinachosahauliwa ni kwamba mfumo huu wa maisha ambao mara nyingi huendana na upatikanaji mkubwa wa chakula, unatupelekea katika kushindwa kutumia miili yetu ipasavyo pamoja na virutubisho tunavyokula katika vyakula mbalimbali. Miili yetu imetengenezwa ili iweze tumika katika kiwango fulani, na kuitumia chini au juu ya viwango hivyo, husababisha magonjwa mbalimbali.
Kwa ufupi ni kwamba, magonjwa yanayohusishwa na mifumo ya maisha hutokea pale mwili unapotumiwa chini au juu ya kiwango chake, au pale mwili unapopokea virutubisho chini au juu ya viwango vinavyohitajika. Kwa mfano katika jamii tuliyopo sasa hususani mijini, kiasi cha watu wanaoweza kuwa na maisha mazuri kinaongezeka. Vilevile teknolojia inaongezeka hivyo kupelekea watu kula zaidi na kutembea kidogo, kwa maana ya kuendesha magari na kuketi kutizama runinga kwa muda mrefu. Hii inaufanya mwili kutunza virutubisho ambavyo kwa hali ya kawaida vingetumika kama mtu angetembea au kufanya kazi itumiayo nguvu kiasi. Mwili hauhitaji kiasi kikubwa cha virutubisho hivi na baada ya muda mrefu vinakuwa kama sumu na hivyo kusababisha magonjwa kama vile kisukari kisichotegemea insulini.
Kwa kufanya mazoezi, mtu anauwezesha mwili wake kutumia virutubisho ipasavyo, kwa maana ya kwamba hakuna kinachohifadhiwa mwilini kinyume na matakwa ya mwili. Ifahamike kuwa mazoezi si lazima yawe ya kwenda kwenye sehemu maalum za mazoezi kama gym. Tafiti zimeonyesha kuwa kutembea kwa saa moja zaidi ya shughuli zako za kawaida kwa siku tatu mpaka tano kwa juma, kunasaidia kujikinga na magonjwa kama kisukari kisichotegemea insulin, na magonjwa ya moyo. Wanasayansi katika chuo kikuu cha karolinska nchini Sweden, wameonyesha katika utafiti kwamba, kutembea kwa kawaida kwa muda wa angalau saa moja kwa siku kwa muda wa siku tano kunaweza kushusha viwango vya sukari vya wagonjwa wa kisukari kufikia kiwango cha kawaida kwa asilimia zaidi ya sabini. Tafiti zimeonyesha pia kwamba, mazoezi yaweza kumkinga mtu na magonjwa kama saratani na msongo wa mawazo.
Kuna ushahidi wa kutosha pia kuhusiana na uwezo wa mazoezi katika kutibu na kuzuia magonjwa ya viungo kama baridi yabisi.
Utafiti mkubwa uliofanywa na wanasayansi kutoka katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Muhimbili, Dar es salaam nchini Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Japani, kimeonyesha kwamba watu wenye tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara, wana kinga zaidi ya kutopata magonjwa ya kisukari na moyo, ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi kabisa.
Inafahamika pia kuwa babu zetu waliishi kwa kuwinda na kulima hivyo magonjwa kama kisukari kisichotegemea insulin, hayakuwepo kabisa. Na imeonekana pia kwamba jamii zinazoishi na kujulikana kama wawindaji na wakulima mpaka leo zina kiasi kidogo sana cha magonjwa kama ya kisukari, moyo na kansa ukilinganisha na jamii zinazoishi maisha tunayoyaita ya kisasa.
Baadhi ya magonjwa yanayoweza kuzuiwa au kutibiwa na mazoezi ni pamoja na Kisukari, unene wa kupindukia, magonjwa ya moyo, saratani na magonjwa ya viungo. Magonjwa mengine ni msongo wa mawazo, kisukari cha mimba, na magonjwa mengi ya mfumo wa homoni. Mazoezi yanatambuliwa kama dawa katika nchi mbalimbali.
Uzuri wa mazoezi kama dawa ni kutokana na uhalisi wake na ukweli kwamba mtu haitaji kununua. Pia hakuna madhara yaliyoripotiwa kwa kutumia mazoezi kama matibabu. Tujenge utaratibu wa kujifanyia mazoezi kwani mazoezi ni dawa halisi na rahisi.

VIEPUKE VYAKULA HIVI VINASABABISHA KISUKARI...

UTAFITI mbalimbali uliokwishafanywa unaonyesha kuwa ugonjwa wa KISUKARI (DIABETES MELLITUS) unatokana na vyakula tunavyokula kila siku katika maisha yetu. Katika siku za hivi karibuni, ongezeko la ugonjwa huu limekuwa kubwa kwa sababau vyakula vinavyosababisha ugonjwa huu, ndivyo vinavyoliwa sana kuliko vile vinavyozuia.

Wiki hii tunawaletea orodha ya vyakula vinavyoaminika kuongoza kwa kuwa chanzo cha ugonjwa huu hatari:
VYAKULA VYA KUKAANGA
Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.
VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI
Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage,  n.k
SUKARI
Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.
Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.
NYAMA ILIYOIVA SANA
Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.
POMBE
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.
NYAMA NA MAFUTA
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.




VYAKULA VYA UNGA MWEUPE
Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k
Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  NEWLIFE AFYA KWA  MSAADA  WA  VYOMBO  MBALIMBALI  VYA  HABARI  NA  MASHIRIKA  YA  AFYA  DUNIANI.

UGONJWA HUU UNATIBIKA KABISA KWA MAELEZO NA USHAURI ZAIDI PIGA SIMU +255752133700/ +255713354389

Jumapili, 8 Septemba 2013

Saratani ya tezi dume; adui wa walevi,wavuta sigara,wazee 50+



Tatizo jingine linaloathiri tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume wa umri mbalimbali duniani. Aidha ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya miaka 40.
Nani yupo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume?
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:
  • Wanaume wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu
  • Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea
  • Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
  • Wanaume wanaokunywa pombe kupindukia
  • Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
  • Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali
  • Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
  • Wachimbaji wa madini hususani aina ya cadmium
  • Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
Pamoja na kwamba, tatizo la kukua na kuongezeka kwa tezi dume yaani BPH hutokea kwa wanaume wengi, hali hiyo haiongezi uwezekano/hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?

Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na
  • Kupata shida unapoanza kukojoa
  • Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na
  • Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
  • Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
  • Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
Vipimo gani vitathibitisha kuwa nina saratani ya tezi dume?
Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu historia ya mgonjwa pamoja na familia yake, kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na kufanya vipimo kadhaa. Vipimo vinavyoweza kufanywa ni pamoja na
  • Digital rectal exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
  • Kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.
DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.
  • Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.
Kipimo kingine huitwa transrectal ultrasound ambacho husaidia kuonesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.
Ili kutambua kama saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili vipimo vya CT scan, MRI pamoja na PET navyo vyaweza kufanyika pia.

Saratani ya tezi dume inatibika?

Ndiyo! Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.
Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi, wakati kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu bila kumfanyia upasuaji au bila kumpatia tiba ya mionzi.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

UGONJWA HUU UNATIBIKA NA MTU ANAPONA KABISA TATIZO ALILONALO. KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA UGONJWA(TATIZO)HUU WASILIANA NA WATAALAM KWA KUPIGA SIMU +255752133700/ +255713354389