Jumapili, 8 Septemba 2013

TATIZO LA UDUMAVU KWA WATOTO

Asilimia kubwa ya watoto Tanzania wamekumbwa na tatizo la udumavu kwa sababu ya maisha tunayoishi. 

Hivi leo,kazi zimekuwa zinawasonga kina mama kiasi kwamba wanawaachia mabinti wa kazi kuandaa chakula cha mtoto mwisho wa siku mtoto anakuwa anakosa virutubisho vinavyotakia. 

Kasi ya tatizo hili inaongezeka sana kwasababu ya vyakula tunavyodhani tunawasaidia sana watoto wetu; mfano chips, baga, na sweets, lakini si kweli kwamba vinawapa mahitaji mwilini bali vinazidi kuwaongezea sumu mwilini. Hili limepelekea watoto kupatwa na magonjwa ya tabia kama kisukari,kansa...

Sambamba na tatizo hili, wakina mama wengi wanashindwa kuwanyonyesha watoto wao angalau kwa miezi sita ya mwanzo kwa sababu ya kazi tunazokuwa tunafanya na majukumu mbalimbali.

Hii inachangia sana tatizo la udumavu wa mtoto kwani virutubisho vingi vilivyopo kwenye maziwa ya mama si rahisi kuja kuvipata sehemu nyingine yoyote, hivyo mtoto akishavikosa anakuwa anapata upungufu wa kitu fulani kwenye mwili na akili yake. Pia huathiri ukuaji wake.

Mkinge mwanao kwa kumpatia virutubisho vinavyohitajika mwilini, hii itamuongezea na uwezo wa akili yake kufanya kazi.

Kwa ushauri wa jinsi ya kumsaidia mwanao ambaye hajanyonya kwa muda angalau wa mwaka mzima tutembelee "NewLife-Afya" kwa ushauri wa jinsi ya kumsaidia mwanao kwa kutuandikia:


e-mail: newlifecompany10@gmail.com 

AU TUPIGIE

+ 255 713 354 389 / +255 752 133 700

Soma andiko la Shirika la afya duniani (WHO) kuhusu tatizo la udumavu

Child growth indicators and their interpretation

In children the three most commonly used anthropometric indices to assess their growth status are weight-for-height, height-for-age and weight-for-age. These anthropometric indices can be interpreted as follows:
Low weight-for-height: Wasting or thinness indicates in most cases a recent and severe process of weight loss, which is often associated with acute starvation and/or severe disease. However, wasting may also be the result of a chronic unfavourable condition. Provided there is no severe food shortage, the prevalence of wasting is usually below 5%, even in poor countries. The Indian subcontinent, where higher prevalences are found, is an important exception. A prevalence exceeding 5% is alarming given a parallel increase in mortality that soon becomes apparent (2). On the severity index, prevalences between 10-14% are regarded as serious, and above or equal 15% as critical. Typically, the prevalence of low weight-for-height shows a peak in the second year of life. Lack of evidence of wasting in a population does not imply the absence of current nutritional problems: stunting and other deficits may be present (3).
High weight-for-height: "Overweight" is the preferred term for describing high weight-for-height. Even though there is a strong correlation between high weight-for-height and obesity as measured by adiposity, greater lean body mass can also contribute to high weight-for-height. On an individual basis, therefore, "fatness" or "obesity" should not be used to describe high weight-for-height. However, on a population-wide basis, high weight-for-height can be considered as an adequate indicator of obesity, because the majority of individuals with high weight-for-height are obese. Strictly speaking, the term obesity should be used only in the context of adiposity measurements, for example skinfold thickness.
Low height-for-age: Stunted growth reflects a process of failure to reach linear growth potential as a result of suboptimal health and/or nutritional conditions. On a population basis, high levels of stunting are associated with poor socioeconomic conditions and increased risk of frequent and early exposure to adverse conditions such as illness and/or inappropriate feeding practices. Similarly, a decrease in the national stunting rate is usually indicative of improvements in overall socioeconomic conditions of a country. The worldwide variation of the prevalence of low height-for-age is considerable, ranging from 5% to 65% among the less developed countries (4). In many such settings, prevalence starts to rise at the age of about three months; the process of stunting slows down at around three years of age, after which mean heights run parallel to the reference. Therefore, the age of the child modifies the interpretation of the findings: for children in the age group below 2-3 years, low height-for-age probably reflects a continuing process of "failing to grow" or "stunting"; for older children, it reflects a state of "having failed to grow" or "being stunted". It is important to distinguish between the two related terms, length and stature: length refers to the measurement in recumbent position, the recommended way to measure children below 2 years of age or less than 85 cm tall; whereas stature refers to standing height measurement. For simplification, the term height is used all throughout the database to cover both measurements.
Low weight-for-age: Weight-for-age reflects body mass relative to chronological age. It is influenced by both the height of the child (height-for-age) and his or her weight (weight-for-height), and its composite nature makes interpretation complex. For example, weight-for-age fails to distinguish between short children of adequate body weight and tall, thin children. However, in the absence of significant wasting in a community, similar information is provided by weight-for-age and height-for-age, in that both reflect the long-term health and nutritional experience of the individual or population. Short-term change, especially reduction in weight-for-age, reveals change in weight-for-height. In general terms, the worldwide variation of low weight-for-age and its age distribution are similar to those of low height-for-age.

UJUE UGONJWA WA PUMU




Utangulizi 

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba.

Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua.

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwa kama vile ugonjwa wa kisukari na moyo unavyoweza kudhibitiwa.


Aina za Pumu 

Kuna aina kuu mbili za pumu. Aina ya kwanza ni ile inayoanza mapema (early onset asthma) na aina ya pili ni ile inayochelewa kuanza (late onset asthma).
Kwa kifupi tutaenda kuangalia tofauti chache kati ya aina hizi za pumu.

Pumu inayoanza mapema 

Ni kawaida kwa aina hii ya pumu kuanza utotoni na kwa kawaida huwatokea waathirika ambao miili yao hutengeneza kingamwili (antibodies) za IgE.
Waathirika wa aina hii ya pumu hutambuliwa kwa vipimo maalum vya ngozi ambapo huonesha kuathirika kwa asilimia kubwa vipimo hivyo vinapofanywa.

Pia waathirika hawa huwa na matatizo mengine ya mzio (allergic disorders) kama mafua na ukurutu (eczema).

Pumu inayochelewa kuanza 
Aina hii ya pumu tofauti na iliyopita huanza katika umri wowote na asilimia kubwa ya waathirika ni watu wazima. Hakuna ushahidi wowote unaohusianisha vizio (allergens) vinavyotokana na mazingira na uwezo wa kusababisha aina hii ya pumu.

Pumu husababishwa na nini? 


Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu.

Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu kama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio.

Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi.

Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo: 

-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k

Viwasho kama: 
-Moshi wa sigara
-Uchafuzi wa hewa
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula)
-Msongo wa mawazo

Vingine ni kama: 
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k

Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi.

Vigezo hatarishi

Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na:

-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio

-Kuvuta hewa iliyo na moshi

-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki

-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto.

-Unene wa kupita kiasi (obesity)

-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease)

Dalili za Pumu 

Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:

-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri

-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua

-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.

-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu.

-Kupumua haraka haraka

Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.

Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku.

Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea.

Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.

Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa.

Uchunguzi 

Kipimo cha muhimu katika uchunguzi iwapo mtu ameathirika na pumu ni kuangalia jinsi mapafu yanavyofanya kazi.

Kipimo hicho kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamu kama spirometry hutathmini kiasi cha hewa mtu awezacho kukitoa baada ya kuvuta hewa kwa nguvu na kwa haraka kiasi gani.

Viwango huwa chini ya kawaida iwapo njia za hewa zina maumivu na zimesinyaa. Kipimo hicho cha spirometry pia hutumika kutathmini jinsi mgonjwa wa pumu anavyoendelea kupata nafuu au tatizo kuongezeka.

Hata hivyo kipimo hicho ni kwa ajili ya watoto wenye zaidi ya miaka mitano na watu wazima tu.

Baadhi ya vipimo vingine vinavyoweza kufanywa iwapo kipimo cha spirometry hakitaonesha tatizo ni:

Kipimo cha Kizio (Allergy test) 


Husadia kugundua iwapo kuna vizio mbalimbali vinavyoathiri mwili wako.

Kipimo cha Mazoezi 


Kugundua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika njia ya hewa kutokana na mazoezi.

Kipimo cha Ugonjwa wa Kucheua na Kiungulia

Kipimo hiki ni muhimu pia kutokana na uhusiano uliopo kati ya kiungulia, kucheua na ugonjwa wa pumu.

Kipimo cha Picha ya Mapafu (X-ray)

Kipimo hiki pia hutumika kuona iwapo kuna kitu chochote kilichoziba njia ya hewa au kama kuna maradhi yoyote katika mapafu au moyo.

Kutokana na vipimo daktari wako atapata picha ya ukali wa pumu yako na kukuanzishia tiba muafaka.

Ugonjwa wa pumu unadawa na mtu akizitumia dawa hizo basi anapona kabisa tatizo alilonalo na halito mpata tena.
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA WATAALAM KWA KUPIGA SIMU +255752133700/ +255713354389 

Ijumaa, 6 Septemba 2013

UKOSEFU WA USINGIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO

KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.

Madhara ya ukosefu usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalan, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine yafutayo:


HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA MOYO
Unapokosa usingizi, mfumo wa uzalishaji homoni huvurugika ambapo uzalishaji wa homoni za ‘stresi’ (stress hormones) huongezeka. Pia husababisha vidonda vya tumbo na hali ya kusikia njaa hata kama umetoka kula muda mfupi. Uko hatarini kusumbumbuliwa na hasira na ghadhabu kila mara.

ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU
Ukosefu wa usingizi huchangia pia ongezeko la shinikizo la damu, pia huchangia kuzeeka kwa mtu kutokana na kuvurugika kwa uzalishaji wa homoni za ongezeko la umri. Humfanya mtu kuonekana mzee ili hali bado ana umri mdogo.

KUZIDISHA TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO
Ukosefu wa usingizi huchangia pia tatizo la ukosefu wa choo na huweza hata kusababisha kifo kama tatizo likiwa sugu.

EPUKA KUTUMIA DAWA ZA USINGIZI
Kama unasumbuliwa na tatizo la ukosefu wa usingizi, jua kwamba hauko peke yako. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Taasisi ya Taifa ya Usingizi (National Sleep Foundation –NSF), umegundua kuwa kati ya watu 10, ni wanne tu hupata usingizi mzuri kila wiki.
Pamoja na kuonekana kwa athari nyingi za kukosekana kwa usingizi, lakini utakuwa unajiweka katika madhara na hatari zaidi iwapo utalazimisha kupata usingizi kwa kumeza dawa za usingizi, kwa sababu ni hatari na mara nyingi dawa hizo huwa hazisaidii kuondoa tatizo.


KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA TATIZO HILI. WASILIANA NA MTAALAMU KWA +255713354389/+255752133700

Alhamisi, 5 Septemba 2013

UJUE UGONJWA WA PRESHA NA JINSI YA KUTATUA TATIZO:

Hii ni hali ambayo moyo husukuma damu kwa hali ambayo si yakawaida,presha(shinikizo la damu) husaidia ktk msukumo wa damu,lkn presha ikiwa kubwa kubwa inaweza kuleta madhara ya kiafya na huweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.Watu wazima zaidi ya umri wa miaka 18 presha ya dystole inatakiwa kuwa kipimo cha juu cha 120 mm Hg na presha ya diastole ambacho ni kipimo cha chini kabisa inatakiwa kuwa 80mm Hg,presha ya dystole ni kipimo ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu ktk mishipa ya damu wakati moyo unadunda.Presha ya diastole ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu ktk mishipa ya damu wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo.Presha hupimwa ktk milimita za mercury,hapa ndipo tunasema presha inatakiwa kuwa 120/80 mm Hg



Ugonjwa huu anaweza kuupata mtu yeyote mkubwa au mtoto kulingana na maisha tunayoishi,Presha huathiri vitu vingi mfano Idadi ya maji mwilini,idadi ya chumvi,homoni mwilini,hali ya joto au hali ya baridi,hali ya hisia na hali ya mafigo,mfumo wa neva na mishipa ya damu.
Kama presha itakuwa juu na kuachwa kutodhibitiwa moyo na mishipa haitafanya kazi vizuri kama ipasavyo.Kwasababu neva na seli za mwili tayari zinakuwa zimeshaathiriwa na presha hapo ndipo mtu akitumia dawa zenye kemikali inakuwa ngumu sana kupona kabisa tatizo hilo.
Lakini usijali sasa utapona na utarudi kama kawaida kwa kufuata kile nitakachokuelekeza.
Kuna aina mbili za presha
1. Presha ya asili ambayo yenyewe amabayo chanzo chake hakifahamiki ,lkn tatizo la kigenetics na kimazingira kama,chakula,mazoezi zinanafasi kubwa ktk ugonjwa huu.
2. Presha inayosababishwa na tatizo kwenye mwili Mfano:Kupungua unene wa mishipa flani ya damu,Matatizo ya tezi,Matatizo ya figo,matumizi ya dawa ,madawa ya kulevya au kemikali,matumizi ya madawa ya kuzuia mimba


Hali zinazosababisha Presha

Hali ya unene wa kupindukia

Ulaji mwingi wa chumvi au sodium

Hali ya uvivu

Uvutaji wa sigara

Mazingira ya mifadhaiko ya hali ya juu

Ulaji wa vyakula visivyo vya afya

Historia ya kifamilia ya kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu

Jinsi Ya Kuzuia Ugonjwa Wa Presha

Acha uvutaji wa sigara

Pungua uzito kama ni mnene

Ongeza mazoezi ya viungo ili kuimarisha hali ya afya ya moyo

Punguza sodium iwe chini ya gramu 2.4 za sodium au chini ya gram 6 za chumvi kwa siku (chumvi kijiko kidogo kimoja na robo)

Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na kolestero

Punguza unywaji wa pombe ( tumia kinywaji kimoja au viwili kwa siku)

Ulaji wa kiwango kinachotakiwa cha kalsiumu, potasiamu, magnesiamu,

Dhibiti hali ya mifadhaiko na majonzi

Dalili za Presha

Kuumwa kwa kichwa

Uchovu

Matatizo ya macho

Hali ya kichefuchefu na kutapika

Hali ya woga

Hali ya kuchaganyikiwa

Kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi


KAMA UNATATIZO HILI BASI LIMEKWISHA WASILIANA NA 0713354389/ +255752133700 UPATE USHAURI NA MATIBABU USIJALI.PRESHA INATIBIKA.

Jumatatu, 2 Septemba 2013

JINSI YA KUONDOA CHUNUSI

Chunusi husababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa Testosterone hormone na mafuta yamwili wakati wa mabadiliko ya kimwili pia husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia.

Product kama HERB SOAP, ALOE SOFTGEL, and PEARL BEAUTY  ni vitu vya kihalisi vinavyo weza kutibu chunusi na kuna baadhi ya product hazishauriwi kutumiwa na mtu kama unaujauzito au unatatizo la kiafya hivyo unatakiwa kuwasiliana na dactari kabla ya kutumia kwa ushauri. Kabla ya kuoga ponda nyanya changanya na asali na maji ya roses na paka nyanya kwenye uso wako kaa nayo kwa muda wa dakika 20 kabla ya kuosha. Usiku kabla ya kulala paka mchanganyiko wa cream, glycerine, and lemon juice kwenye uso wako na kaa nayo kwa muda wa dakika chake kabla ya kuosha. Pia jambo la muhumu kwa mtu anayesumbuliwa na chunusi ni kunywa maji kwa angalau lita 3 kila siku pia ni muhimu sana kwa ngozi yako, matunda fresh na mboga za majani kwenye diet yako. Vitu unavyotakiwa kuepuka ni kugusa uso wako mara kwa mara, epusha nywele kugusa uso wako na kutumbua chunusi kiholela. Pia epuka kupaka make up nyingi usoni ni vizuri kutopaka make up kabisa ukiwa na tatizo la chunusi.

Jumapili, 1 Septemba 2013

UVIMBE KATIKA KIZAZI UNAOWATESA WANAWAKE


 
Katika siku za hivi karibuni,wanawake nchini wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokwenda kujifungua basi hukutwa na uvimbe katika nyumba ya uzazi.


Uvimbe huo,ambao si saratani, umekuwa ni tishio kwa maelfu ya wanawake nchini jambo linalosababisha wengi wao kuondolewa vizazi vyao.


Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa kitengo cha Pathologia wa Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili,Henry Mwakyoma akinukuliwa na Mwandishi wa Makala haya Bi.Florence Majani,anauelezea Ugonjwa huu na kusema kuwa fibroids kwa kitaalamu ‘leimyoma’ ni uvimbe unaowapata asilimia 25 ya wanawake wa kiafrika na asilimia 50 ya Wazungu.


“Nasisitiza kuwa ,uvimbe huu si saratani,unaojitokeza ama katika ukuta wa kati, wa nje au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi,”anasema.


Anasema; ”uvimbe huu huwa katika umbile la misuli myembamba na laini na ukua siku hadi siku,” anabainisha Dk.Mwakyoma na kuongeza kuwa,sababu kuu ya ugonjwa huu,bado haijajulikana.


Anafafanua kuwa,pamoja na kuwa sababu kuu haijajulikana,lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha mwanamke kupata uvimbe wa fibroids.


“Sababu  inayopewa kipaumbele zaidi  ni wingi wa vichocheo vya ‘estrogen’ ambavyo vipo katika miili ya wanawake.” Anasema.


Dk.Mwakyoma anafafanua kuwa ,vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.


“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu,huwa ni wanawake walio katika balehe au ambao tayari wamevunja ungo,kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni,”anabainisha mtaalamu huyo.


Lakini,pia  anasema kuwa endapo inatokea mwanamke akapata matibabu ambayo yatamtaka kuongezewa vichocheo hivi,huwa katika hatari ya kupata uvimbe huu.


Aidha,daktari huyu anabainisha kuwa,ndiyo maana wanawake walio katika kikomo cha hedhi(menopause) na watoto hawawezi kupata uvimbe huu.


Anazitaja sifa kuu za ugonjwa huu na kusema ,huwa ni nyingi kwa sababu ni uvimbe ambao asili yake ni mishipa midogo midogo na inapokuwa  huweza kufikia urefu wa sentimeta tano na zaidi na uzito wa kilogramu 10.


Anaongeza kuwa,uvimbe huu unaweza kutokea katika kuta zote za 
kizazi cha mwanamke na kumsababishia mwanamke ang’olewe kizazi chake.


“Hata hivyo, wanawake wengi hupata uvimbe huu katika ukuta wa ndani kabisa wa kizazi,”anasema.


Anataja sifa  nyingine za uvimbe huu ni kuwa na tabia yake ya kubadilikabadilika sana.


Kwa mfano,fibroids huweza kubadilika rangi na kuwa ya njano,ikabadilika na kuwa katika hali ya kimiminika,baadaye kuwa ngumu au kuwa laini yenye kutomasika.


 



Dalili za Fibroids

Dk.Mwakyoma anazitaja sababu za ugonjwa huu na kusema kuwa,ni vigumu mwanamke kubaini au kuhisi dalili zake.


“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa ,wengi hugundulika wakati wa kujifungua,na ujauzito au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi,basi huweza kutokwa damu kwa wingi,”Anasema.


Anasema: ”Hata hivyo,asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,”


Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi.


Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.”Asilimia 30 ya wanawake wanaopata maumivu na damu nyingi wakati wa hedhi huwa na uvimbe wa aina hii”anasema.


Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.
 
“Nina mifano hai,wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito,wakakosa kabisa siku zao za hedhi,wakapata dalili zote za ujauzito na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,”anasema.


Anasema,mara nyingi uvimbe unaojitokeza katika ukuta wan je wa kizazi na kuning’inia,ndiyo hucheza na kuleta dalili za ujauzito.

Mwanamke huweza kuvimba miguu kwa sababu  uvimbe huu husababisha damu isitembee.


Anataja dalili nyingine kuwa ni mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.


Wakati mwingine ,fibroids hukua na kuzuia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusababisha mwanamke avimbiwe.

Vile vile, uvimbe huo uweza kuzuia kibofu cha mkojo na kumfanya 
mwanamke apate haja ndogo kwa taabu, au akatokwa na uchafu ukeni.


“Hatari kuu ya uvimbe huu ni ugumba,asilimia 27 hadi 40 ya wanawake wanaopata uvimbe katika kuta zote za kizazi, hushindwa kupata watoto,”anafafanua DK.Mwakyoma.


Hatari nyingine ni kwa wanawake wajawazito wenye uvimbe huu ambao wengi hufanyiwa upasuaji kwani fibroids huweza kuzuia mlango wa kizazi na mwanamke kushindwa kujifungua.

Imebainishwa kuwa, asilimia 30 ya wanawake hutolewa vizazi mara baada ya kujifungua kutokana na uvimbe huu.


Mtaalamu huyo anatahadharisha  kuwa, wanawake walio katika umri wa kuzaa lakini hawazai wapo katika hatari ya kupata maradhi haya.

“Hii ni kwa sababu vichocheo vya estrogen hukua kwa wingi na kusababisha misuli ya fibroids kukua, lakini vichocheo hivyo huacha kukua wakati wa ujauzito,”anasema.


Anataja walio katika hatari hii ni watawa ambao hawatakiwi kuzaa au wale wanaopitiliza umri wa kuzaa.


Matibabu ya maradhi haya mara nyingi ni kufanyiwa upasuaji na kuondoa uvimbe huu au kutolewa kabisa kizazi.


“Hii inategemea na na umri wa mgonjwa,idadi ya watoto na maamuzi yake binafsi.”anasema.


Wataalamu mbalimbali wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi ambayo mengine yanaweza kutibika au kuzuilika.

Jumatano, 21 Agosti 2013

TAMBUA UMUHIMU NA FAIDA YA KULA MATUNDA NA MBOGA MAJANI


  APPLES Protects your heart, prevents constipation, Blocks diarrhea, Improves lung capacity Cushions joints

APRICOTS Combats cancer, Controls blood pressure ,Saves your eyesight ,Shields against Alzheimer's ,Slows aging process

 ARTICHOKES Aids digestion, Lowers cholesterol, Protects your heart, Stabilizes blood sugar Guards against liver disease

AVOCADOS Battles diabetes, Lowers cholesterol, Helps stops strokes, Controls blood pressure Smoothes skin

 BANANA Protects your heart, Quiets a cough, Strengthens bones, Controls blood pressure, Blocks diarrhea

BEANS Prevents constipation, Helps hemorrhoids, Lowers cholesterol, Combats cancer, Stabilizes blood sugar

 BEETS Controls blood pressure, Combats cancer, Strengthens bones, Protects your heart, Aids weight loss

 BLUEBERRIES Combats cancer, Protects your heart, Stabilizes blood sugar, Boosts memory , Prevents constipation

BROCCOLI Strengthens bones, Saves eyesight, Combats cancer, Protects your heart, Controls blood pressure

CABBAGE Combats cancer, Prevents constipation, Promotes weight loss, Protects your heart, Helps hemorrhoids

CANTALOUPE Saves eyesight, Controls blood pressure, Lowers cholesterol, Combats cancer Supports immune system

CARROTS Saves eyesight, Protects your heart, Prevents constipation, Combats cancer, Promotes weight loss


Baada ya utambulisho wa umuhimu na faida ya kula matunda na mboga kwani kila mboga na kila tunda vina nafasi tofauti ya kujenga na kulinda mwili. Watoto wengi wanasumbua sana kwenye kula hasa mboga majani asilimia kubwa sio wapenzi angalu upande wa matunda watoto wengi hupenda matunda lakini kwa kuchagua sio matunda yote watapenda kula tabia hii hujitokeza kwa kila mtoto hakuna aliekamilika nakumbuka hata mimi nilipokua mtoto nilikua nasumbua sana kula kiasi ikapelekea kua na afya dhaifu wakati wa kukua kwangu mpaka nilipobadili tabia na kuanza kula bila ya kufatiliwa.

Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini
.




Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usalama sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni mahindi mabichi ya njano kabla huifadhiwa katika kopo tayari kwa matumizi, karoti iliyokwaruzwa, Lime stone lettuce, chicory, Radish iliyokwaruzwa, zucchin iliyokwaruzwa, rollo nyekundu, rollo ya kijani, matango yaliyokatwa, celeriac salad, curly endive, chicory nyekundu.



Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa  ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na  radish nyeupe

Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara nusu sahani tu kama mduara wa nusu mwezi kati kati acha nafasi kiasi.

Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chini utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.

Kisha liweke juu ya zile mboga mboga pembei yake kata kipande cha tikiti maji rangi yeyote ile kama ni la kijani, jekundu au rangi ya chungwa pamba kama invyoonekana katika picha.

Kisha kata slice nyembamba ya chungwa katikati yake weka tunda lolote dogo la mviringo kama zabibu au strawbery chomeka toothpick ili ishikilie chungwa juu ya tikiti maji.

Salad hii unaweza mwagia dresing yeyote ile mfano italian dressing, french dressing au siki na chumvi inatosha salad hii unaweza kula na kipande cha kuku, samaki wakuchemsha au wa kukaanga na unakua umekula mlo safi kabisa bila stach kwa watu wanaofanya dayati hapa ni mahala pake mvuto na muonekano wa sahani utamfanya mlaji avutie hata kama si mpenzi wa mboga na matunda.



Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usafi sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni nanasi iliyopikwa katika sukari, embe mafuta, cappers, vitunguu vidogo vya kopo,  chopped chives, chopped onion, olives nyeusi, asparagus, matango machanga yaliyosindikwa, olives zakijani, Nyanya



Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe.

Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara kuzunguka sahani yote katikati acha nafasi.

Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chi utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.

Kisha liweke pembeni ya zile mboga mboga katikati ya sahani unaweza weka mchanganyiko wowote ule wa nyama ya kuku, ngo'mbe, samaki au sausage iliyochemshwa ikapoa.

Kata saizi ya kuweza kuingia mdomoni kisha changanya na vitunguu vilivyochopiwa safi pamoja chives.

Mchanganyiko huo unaweza malizia na chaguo lako la dresing yeyote uipendayo kisha unamwagia kati kati ya sahani mwisho kata nyanya kipande weka pamoja na tango dogo la kopo na olive moja ya kijani na moja nyeusi kwa kupamba salad yako.




Kwa upande wa mlo kamili baada ya kupika chakula chako kikaiva kama ni ugali au wali

Chemsha njegere zisiive sana

Kisha kata vitunguu vidogo sana kaanga katika siagi dakika 1 tu

Kisha weka hizo njegere zilizoiva katika sufuria kwa dk 2 usiasahau chumvi kisha zitoe

Chukua nyanya nzuri ngumu iliyokwisha iva kata nusu pia kata kidogo katika kitako ili iweze kukaa katika sahaki

Kisha toa mbegu zote katikati ya nyanya tumia kijiko kuchota na jaza zile njegere kwanye nyanya

Kisha save nyanya hiyo yenye njegere kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku.

Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.




Sasa hapa ndio utawakamata kweli kweli wasiopenda kula mboga za majani,

Chukua maharage mabichi yachemshe kiasi yasiive sana yabaki na rangi yake nzuri ya kijani

Kisha unachukua bacon slice zipo aina mbili zipo bacon za nguruwe na bacon za ng'ombe chaguo ni lako mlaji.

Kisha chukua maharage hesabu kumi na tano kisha zungushia bacon katika maharage hayo weka katika ubao wa kukatia kata ncha za mwisho ili kuweka usawa na muonekano mzuri zaidi.

Ukishamaliza weka kikaango kwenye jiko la moto wa wastani tu weka mafuta kiasi katika kikaango yakishapata moto weka maharage yaliyozungushiwa bacon kaanga kiasi tu ili ile bacona ikauke.

Kisha toa tayari kwa chakula pia sevu kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku. Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.
 
KWA KUFATILIA MAELEZO HAYA YOTE UTAKUA UMEFANIKIWA KUMREKEBISHA KAMA NI MUME AU MTOTO ASIEPENDA KULA MBOGA ZA MAJANI AU MATUNDA IKIWA UMESHAFAHAMU PIA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO KWA BINADAMU





Nashukuru sana mdau aliezungumzia upatikanaji wa bacon ya ng'ombe, nikweli kwa ulaya kupata bacon ya ng'ombe ni adimu sana ila hapa kwetu Tanzania zinapatikana kwa wingi ukienda katika supermaket kubwa au maduka makubwa ya nyama utapata.

Endapo umekosa basi chukua mboga hiyo hapo juu inaitwa leeks kata jani lake lisafishe vizuri kisha zungushia vizuri maharage yako hatua za upishi ni zile zile unaikaanga kidogo tu itaiva na italeta harufu nzuri sana kwahiyo kwa asie kula kabisa nyama atakua nae kafaidika.