. Uangalizi mzuri
wa Ngozi ikiwemo kulinda ngozi na Mwanga wa Jua pamoja na kuiosha kwa
utaratibu itafanya ngozi yako kuwa na Afya na kuishi kwa ubora miaka yote.
Je? Hauna muda wa kuitunza ngozi yako? Jitahidi kufata misingi bora. Utunzaji
wa ngozi yako na kujichagulia mfumo mzuri wa Afya katika maisha yako kunaweza
kukusaidia kuchelewesha mchakato wa ngozi yako kuzeeka mapema na pia kulinda
matatizo mbalimbali ya ngozi.
Fuata hizi Dondoo tano (5). :
1.
Jilinde kutokana na Jua. Moja ya njia bora zaidi ambazo unatakiwa kuzifanya ni
kulinda ngozi yako na mwanga wa Jua. Mwanga wa jua huweza kukusababishia
mikunjo mikunjo, madoa madoa hasa ya uzee na matatizo mengine mengine ya ngozi
– vilevile kuweza kukusababishia Saratani ya Ngozi. Ulinzi bora zaidi wa jua katika
ngozi yako ni kama ifuatavyo: Tafuta kivuli. Epuka mwanga wa Jua pale
inapofikia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni, muda huu huwa jua linakuwa kali
sana hivyo uwezekano wa kuathiri ngozi yako ni rahisi sana. Vaa nguo
zenye kuilinda ngozi. Funika ngozi yako kwa shati ya mikono mirefu ya kitambaa
kisichoruhusu joto (hasa nguo za kufuma), suruali ndefu na kofia yenye upana wa
kuweza kuzuia mwanga wa jua hasa pale unapotoka nje au kwenda sehemu yoyote ile
wakati mwanga wa jua ni mkali.
2. Usivute
sigara. Uvutaji wa
sigara hufanya ngozi yako kuzeeka na kutengeneza mikunjo. Uvutaji wa sigara
hukondesha vishipa vidogo vipatikanavyo katika tabaka la juu ya ngozi, ambayo
hupunguza upitishaji wa damu. Hali hii huinyima ngozi Oxygen na virutubisho
muhimu. Uvutaji wa sigara pia huharibu vinyweleo ambavyo vinaipa ngozi nguvu na
kuifanya iwe nyororo. Kwa nyongeza tu ni kwamba kile kitendo kinachoendelea
endelea kila siku unachokifanya usoni pale unapovuta sigara, kama vile kutanua
mashavu wakati wa kutoa au kuingiza moshi na kufinya finya macho hufanya ngozi
ya uso kujikunja kwani mwili wa binadamu hujiweka vile unavyouzoesha. Kama unavuta
sigara, basi njia bora ya kuilinda ngozi yako ni kuacha. Muombe daktari wako
akupe dondoo na matibabu ya kukusaidia kuacha kuvuta sigara.
3.
Itunze ngozi yako kwa upole kabisa. Uoshaji wa kila siku na kunyoa kunaweza
kuharibu ngozi yako. Kuifanya nyororo fuata haya yafuatayo:
I. Jaribu kupunguza muda wa
kuoga. Ninaposema hivi haina maana kuwa usioge, kuoga ni katika usafi na
ni afya ila usikae muda mrefu bafuni. Maji ya moto na kuoga kwa muda mrefu
huondoa mafuta katika ngozi yako, jitahidi kupunguza muda wa kukaa bafuni na
tumia maji yaliyopoa ili kusaidia kuwa na afya katika ngozi yako.
II. Epuka kutumia sabuni ngumu.
Sabuni kama hizi au sabuni za dawa kali huondoa mafuta mafuta katika ngozi.
Badala yake, tumia sabuni zilizo laini.
III. Nyoa kwa uangalifu. Kulinda na
kuifanya ngozi yako iwe na mafuta tumia Shaving Cream, losheni au Gel kabla ya
kunyoa. Na kwa unyoaji wa kuondoa nywele kabisa kabisa tumia kiwembe kikali na
hakikisha unanyoa kuelekea kule nywele au ndevu zinapoelekea na si kinyume
chake.
IV. Kausha. Baada ya kuosha au kuoga,
kwa utaratibu kausha ngozi yako kwa kutumia taulo ili baadhi ya unyevu kubakia
ndani ya ngozi.
V. Lainisha ngozi kavu. Kama ngozi
yako ni kavu, tumia dawa za kulainisha (moisturizer) ambayo inaendana na aina
ya ngozi yako. Kwa matumizi ya kila siku, tumia moisturizer ambazo zima SPF.
Ukitaka kununua jaribu kuulizia hili. Daily cleansing and shaving can take a
toll on your skin. To keep it gentle:
4. Kula vyakula vyenye Afya.
Mlo kamili na wenye Afya bora husaidia kujiona vizuri na kujisikia vile
utakavyo. Kula matunda sana, mboga za majani, nafaka nafaka pamoja na protini
kidogo. Uhusiano baina ya mlo na chunusi hauko wazi – lakini baadhi ya utafiti
unapendekeza kwamba mlo unaoleta vitamin C na wenye Fat kidogo na Carbohydrate
iliyotengenezwa vizuri inaweza kufanya ngozi yako kuonekana mpya kila siku.
5. Jitahidi kuepuka mfadhaiko au mawazo. Mawazo uliyoshindwa
kuyakabili na kuyaondoa yanaweza yakafanya ngozi yako kuwa na urahisi wa
kutokeza chunusi na matatizo mengine. Kuboresha Afya ya ngozi yako na
hali ya fikra ya afya yako – chukua hatua za kuzuia mawazo. Tengeneza njia za
kukuwezesha kuzuia hili, tengeneza ratiba ya kufanya vitu ambavyo unafurahia
kuvifanya na usikae peke yako bila kazi yoyote. Matokeo yake yanaweza kuonekana
kama ndoto kuliko ulivyotegemea. Ni tumaini langu kuwa umefurahia dondoo hizi
chache ambazo ukuzifuata zinaweza kukusaidia katika kuboresha Afya ya Ngozi
yako. Ikiwa una la ziada, jisikie huru kuacha maoni yako hapa ili sote
tunufaike katika kuelimishana juu ya jambo hili.
Nakutakia kila la kheri katika kutafute kile bora unachohitaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni